杏MAP导航

Tafuta

2025.08.15 Sala ya Malaika wa Bwana huko Castel Gandolfo 2025.08.15 Sala ya Malaika wa Bwana huko Castel Gandolfo  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV,Sherehe ya Kupalizwa B.Maria:Mungu alikuja kukutana,alijivika mwili wetu!

Mama Kanisa akiadhimisha sherehe ya Kupalizwa kwa Mama Bikira Maria Mbinguni,Papa Leo XIV ametoa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana akiwa mbele ya Jengo la Kipapa huko Castel Gandolfo,Agosti 15:Katika safari ya maisha,hatima ni Mungu, Upendo usioisha na wa milele,utimilifu wa maisha,wa amani,furaha na kila wema.Moyo wa binadamu unavutiwa na uzuri kama huo na hauna furaha hadi unapata;kwa hakika kuna hatari ya kutopata ikiwa anapotea katika mtumishi wa giza) na wa ubaya.

Angella Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Leo XIV, wakati Mama Kanisa anasheherekea Kupalizwa Mbinguni  kwa Bikira Maria, tarehe 15 Agosti 2025 aliongoza Sala ya Malaika wa Bwana akiwa huko Castel Gandolfo, makao ya Kipapa wakati wa likizo. Kabla ya sala hiyo, alitoa tafakari yake ambapo alianza kwa kuwatakia sherehe njema kaka na dada! Papa alisema, Mababa wa Mtaguso wa II wa Vatican, walituachia andiko zuri sana juu ya Bikira Maria, ambaye ninapenda kusoma pamoja  nanyi  leo hii, wakati tunaadhimisha sherehe ya Kupalizwa kwa Utukufu mbinguni. Mwishoni Hati hiyo kuhusu Kanisa, Mtaguso unasema hivi: “ Mama wa Yesu, kama alivyo mbinguni, ambaye tayari ametukuzwa kwa mwili na katika roho, anaunda sura na mwanzo wa Kanisa ambalo linapaswa kuwa katika utumilifu wa siku zijazo, kama alivyo duniani anang’aa mbele ya wanahija watu wa Mungu ambao ni ishara ya uhakika wa tumaini na wa faraja, hadi Bwana atakapokuja siku ile (taz 1Pt 3,10)”LG 68).

Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana   (@VATICAN MEDIA)

Papa alisema, Maria ambaye Kristo Mfufuka alimchukua kwake katika utukufu wa mwili na roho, anang’aa kama picha ya matumaini kwa wanae, wanahija katika historia. Jinsi gani ya kufikiria mashairi kadhaa ya Dante, katika wimbo wake wa mwisho kuhusu Mbinguni? Katika sala aliyoweka katika mdomo wa Mtakatifu Bernardo, anaanza hivi: “Bikira Maria, Mwana wa Mwanao (XXXI,1),” Mshairi anasifu Maria kwa sababu hapa dunia, kati yetu hasiyekufa, ni “ kisima cha tumaini hai,”  yaani kisima hai, kinachobubujika matumaini. Kwa njia hiyo Papa Leo aliongeza kusema kuwa: “ukweli huu wa imani yetu ni mkamilifu sanjari na mada ya Jubilei ambayo tunaiishi: ‘Wanahija wa matumaini, ’ Mwanahija anahitaji dira inayomwelekeza safari yake: yaani hatima nzuri inayovutia, ambayo inamwongoza hatua zake na kuuisha wakati wa uchovu na kumpatia  ari daima katika moyo wake shauku na matumaini.

Waamini wakati wa sala ya malaika wa bwana , Castel Gandolfo
Waamini wakati wa sala ya malaika wa bwana , Castel Gandolfo   (@VATICAN MEDIA)

Katika safari ya maisha, Papa aliendelea, "hatima hiyo ni Mungu, Upendo usioisha na wa milele, utimilifu wa maisha, wa amaini furaha na kila wema. Moyo wa binadamu unavutiwa na uzuri kama huo na hauna furaha hadi unapata; kwa hakika kuna hatari ya kutopata ikiwa anapotea katika  ya (mtumishi wa giza) wa ubaya na wa dhambi."  Papa alikazia kuzema kuwa “Lakini basi tazama neema: Mungu alikuja kukutana, alijivika mwili wetu, uliofanywa na udongo na kuupeleka kama tusemavyo ishara ya mbingu yaani Mungu. Ni fumbo la Yesu Kristo, aliyefanyika mwili, akafa na akafufuka kwa ajili ya wokovu wetu na hasiyetenganishwa naye, na hata fumbo la Maria, mwanamke ambaye Mwana wa Mungu alichukua mwili na wa Kanisa, mwili wa fumbo la Kristo. Hili ni fumbo la kipekee la upendo na hivyo la uhuru.”

Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Kama Yesu alivyoitikiaNdiyo na Maria alisema ndiyo, tazama mimi hapa, aliamini katika Neno la Bwana. Na maisha yake yote yalikuwa ya hija ya matumaini pamoja na Mwana wa Mungu na mwanae, hija ambayo kwa njia ya Msalaba na ya Ufufuko, aliweza kumfikisha kwa Baba, katika mikono ya Mungu.  Kwa sababu hiyo wakati tunatembea kama binafsi, kama familia, na katika jumuiya, hasa wakati mawingu yanakuja, na njia isiyo na uhakika, na nguvu, tuinue mtazamo, tutazame Yeye, Mama Yetu, tutapata tumaini ambalo halikatishi tamaa.

Sala ya Malaika wa Bwana huko Castel Gandolofo 15 Agosti 2025
Papa Leo katika sala ya Malaika wa Bwana

 

15 Agosti 2025, 14:53