Papa Leo XIV,chakula cha mchana:sisi ni viumbe wazuri waliombwa kwa sura ya Mungu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu mara baada ya misa asubuhi, katika Madhabahu ya Maria wa Rotonda huko Albano, na kurudi kuendelea na Tafakari ya Malaika wa Bwana Dominika tarehe 17 Agosti 2025, kilichofuata kushiriki akiwa katika uzuri wa kazi ya uumbaji kwenye Bustani za Laudato si katika Majengo ya Kipapa ya Castel Gandolfo chakula cha mchana na Maskini wanaohudumiwa na Caritas, jimbo la Albano. Kwa njia hiyo kabla ya chakula hicho, Papa alipenda kutoa salamu kwa ufupi bila maandishi kwamba: “ labda maneno mawili tu. Wengi wenu tayari mmenisikia asubuhi ya leo kwenye Misa Takatifu, lakini inanijia akilini. Ningependa kwanza kushirikisha kabla ya ishara hiyo, muhimu sana kwetu sote, ambayo ni kuumega mkate, kuumega mkate pamoja, ishara ambayo kwayo tunamtambua Yesu Kristo kati ya wafuasi wake. Ni Misa Takatifu, lakini pia ni kuwa pamoja kuzunguka meza, tukishiriki zawadi ambazo Bwana ametupatia.
Papa aliongeza kusema: “Ninawashukuru wote wa Caritas Jimbo, Mwadhama kwa ukaribisho huu, nafasi hii ya kushiriki hata katika sehemu nzuri sana ambayo inatukumbusha uzuri wa asili, wa uumbaji, lakini pia inatufanya tufikiri kuwa kiumbe mzuri zaidi ni yule aliyeumbwa kwa sura, na kwa mfano wa Mungu, ambaye ni sisi sote.” Na kila mmoja wetu anawakilisha, kwa maana hii, sura hiyo ya Mungu, na jinsi ilivyo muhimu kukumbuka daima kwamba tunapata uwepo huu wa Mungu katika kila mmoja wetu.” “Na kwa hiyo, pia, tukiwa tumekusanyika hapa alasiri ya leo, kwenye chakula hiki cha mchana, tunaishi pamoja na Mungu, katika ushirika huu, katika udugu huu. Shukrani nyingi kwa wote mliopo hapa.”
Baada ya kusema hayo Papa aliongeza kuwa “ sasa tuombe baraka za Bwana juu ya zawadi tutakazopokea, kwa wale wote ambao wamefanya kazi ya kutuletea chakula hiki cha mchana, zawadi tunazoshiriki katika Borgo Laudato Si’ na nyingine nyingi, ambazo zinafanya sherehe hii nzuri iwezekane.” Kwa hiyo Papa alibariki chakula kwa kuanza na ishara ya Msalaba: “Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina. "Bwana, utubariki na zawadi hizi tunazopokea kutoka kwa Utoaji wako. Utusaidie kuishi siku zote umoja katika upendo wako, wewe unayeishi na kutawala milele na milele. Amina. Mlo mwema kwa wote!"
Kardinali Baggio:Borgo Laudato si' inafungulia wanaohitaji
Katika salamu zake kwa Papa na wale waliohudhuria, Kardinali Fabio Baggio, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Juu cha Laudato si' na Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo ya Kibinadamu, alikumbuka kwamba "leo tunaona ndoto ya kinabii ya Baba Mtakatifu Francisko ikitimia. Borgo Laudato si’ si mahali tu, bali ni mtindo wa maisha wa kiinjili unaofungua milango yake kwanza kabisa kwa wale wote wanaohitaji: kwa maskini, na wale wote waliotengwa.” Kabla ya hotuba hizo, hata hivyo alikuwa amesisitiza kuwa: “ushirikiano wa kidugu huja kwanza, kwa sababu ‘ukarimu wa kiinjili huanzia na maskini." Kardinali Baggio hatimaye alifafanua kwamba: “hakuna Ikolojia halisi bila haki ya kijamii: hili ndilo fundisho kuu la Laudato si’ na Mafundisho Jamii ya Kanisa. Upendo wa Kikristo unakamilisha na kuzidi haki, ukiigeuza kuwa upendo thabiti.”
Askofu Viva: Uzuri wa Injili kugeuzwa maisha thabiti
Kabla ya chakula cha mchana, Askofu Vincenzo Viva wa Albano pia aliwasalimu wageni, akiwatambulisha kwa Papa Leo XIV kuwa: "Tukitazama nyuso za wale walioketi kwenye meza hizi leo, hii tunaona uzuri wa Injili ukitafsiriwa katika maisha halisi na ushuhuda wa kuwa kwetu Kanisa la Albano." Na akaongeza: "Hakuna ile ya 'sisi' na 'wao,' hakuna wafadhili na wanufaika: kuna watu wanaoshiriki mkate na, pamoja nao, historia zao, mapambano yao, na matumaini yao."