杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo X: Agosti 22 ni kufunga na kusali kwa ajili ya amani na haki!

Papa Leo XIV alitangaza tarehe 22 Agosti 2025 katika ukumbusho wa kiliturujia wa Bikira Maria,Malkia wa Mbingu kuwa "siku ya kufunga na kuomba ili kuomba amani katika Nchi Takatifu,Ukraine na sehemu nyingine za dunia zilizoharibiwa na migogoro."Mpango wa Papa Leo XIV ni mwendelezo wa mapapa waliomtangulia.

Vatican News

"Wakati ardhi yetu ikiendelea kujeruhiwa na vita katika Nchi Takatifu, Ukraine, na katika maeneo mengine mengi ya dunia, ninawaalika waamini wote kutumia tarehe 22 Agosti katika kufunga na kusali, tukimsihi Bwana atujalie amani na haki na kukausha machozi ya wale wanaoteseka kwa sababu ya migogoro ya silaha inayoendelea." Kwa maneno haya, katika hitimisho la Katekesi ya Papa Leo XIV mnamo tarehe 20 Agosto 2025 aliwataka waamini kuomba zawadi ya upatanisho katika ulimwengu unaozidi kuharibiwa na vurugu. Siku ambayo Kanisa linaadhimisha kumbukizi ya Bikira Maria, Malkia wa Amani, Baba Mtakatifu amehimiza kila mtu kumwelekea yeye ambaye “anaitwa pia Malkia wa Amani,” ili kwa maombezi yake, watu wapate njia ya upatanisho.

Kuwa wanaume na wanawake wote wa upatanisho

Mpango huo ulioanzishwa na Papa Leo unafuatia ule wa mtangulizi wake Papa Francisko, ambaye, katika kipindi cha miaka kumi na miwili ya upapa wake, alitoa wito mara kwa mara kuwepo kwa amani, hasa Mashariki ya Kati na "Ukraine inayoteswa na kwingineko." Kurudi nyuma tayari mnamo Septemba 2013, miezi sita baada ya kuchaguliwa kwa upapa, Papa Francisko alitangaza Siku ya Sala na Kitubio ili kuomba kutoka kwa Mungu "zawadi kuu" ya amani kwa Syria, Mashariki ya Kati, na dunia nzima. Mkesha wa Sala ulifanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro tarehe 7 Septemba, katika kumbumbukizi ya  Kuzaliwa kwa Maria, Malkia wa Amani, na katika mahubiri yake, Papa Francisko anahimiza kila mtu kuwa "wanaume na wanawake wa upatanisho na amani."

Vita ni wazimu

Kwa nyakati nyingine mbili, Papa Francisko aliwaalika watu kusali kwa ajili ya Mashariki ya Kati, ambapo tarehe 27 Oktoba 2023, siku ishirini baada ya kuzuka kwa mgogoro kati ya Israeli na Palestina, saa moja ya sala na ibada ya Ekaristi iitwayo Pacem in terris, iliyopewa jina la Waraka wa  kihistoria wa Papa Yohane XXIII uliochapishwa miaka 60 baadaye, tukio lilifanyika katika Kanisa Kuu la Vatican. Papa aliomba kuwa "Mama hii ni saa ya giza." Na katika saa hii ya giza, tunajizamisha katika macho yako yenye mwanga na kujikabidhi moyoni mwako, ili iweze kuwafundisha wanadamu kukataa upumbavu wa vita, ambao hupanda kifo na kufuta yajayo.” Mwaka mmoja baadaye, tarehe 6 Oktoba 2024, Papa Francisko alitembelea Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu ili kutoa ombi la amani; zaidi ya hayo, alianza siku maalum baada ya mzozo uliofuata mwaka mmoja baadaye maombi na kufunga.

Maombi kwa Bikira Maria, Malkia wa Amani

Papa Francisko kisha alihimiza maombi kwa ajili ya Ukraine siku ya Jumatano ya Majivu, mamo  Machi 2022. Juma moja baada ya mashambulizi ya Moscow dhidi ya Kyiv, Papa Francisko alimwomba Bikira, Malkia wa Amani, kuihifadhi dunia kutokana na upumbavu wa vita." Ombi hili lilirejewa mnamo tarehe 25 Machi iliyofuata, wakati, katika Basilika ya Mtakatifu Petro, Papa  Francisko alikabidhi Ukraine na Urusi kwa Moyo Safi wa Bikira Maria kwa kumaliza mzozo."

Amani iliyotulia inajengwa juu ya haki.

Mipango ya upatanisho duniani kote pia imekuwa ukihamasishwa na warithi wa hivi karibuni wa Mtume Petro, kwa mfano  kunako tarehe 23 Julai , 2006, katika kukabiliana na hali mbaya zaidi katika Mashariki ya Kati, Papa Benedikoto XVI alitangaza Siku maalum ya Sala na Kitubio "kuomba kutoka kwa Mungu zawadi ya thamani ya amani." Hatimaye, kumbukumbu ya pamoja imesalia ya Siku ya Kufunga na Kuomba iliyoitishwa na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili mnamo tarehe 14 Desemba 2001, miezi mitatu tu baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 kwenye Minara Pacha huko New York, nchini Marekani, ambapo mpango uliolenga kuomba kwa bidii kwa Mungu ili aipe dunia amani dhabiti, ambayo msingi wake ni haki."

Kwa hiyo tarehe 14 Desemba 2001, Papa Yohane Paulo II aliwataka Wakristo kuadhimisha siku ya kufunga na kuomba kwa ajili ya amani na urafiki wa kiroho kati ya waamini. Mwaliko huu ulifuatia wito wake wa awali, wa tarehe 9 Desemba 2001, kwa binadamu kuhamasisha nguvu zake dhidi ya vurugu na chuki katika hali tata ya kimataifa, akisisitiza maombi, kufunga, na ishara madhubuti za upendo kama nyenzo za kufikia amani.

22 Agosti 2025, 10:23