Papa Leo XIV:Nosiglia,Mchungaji karibu na wanyonge zaidi
Vatican News
Miaka themanini ya maisha na huduma, “mingi na mikali sana kiasi kwamba hahitaji kuiwakilisha, ndivyo,” Askofu Mkuu wa wa Torino, Kardinali Roberto Repole, alimkumbuka mtangulizi wake katika Kanisa kuu lililokuwa na watu wengi, Askofu Mkuu Cesare Nosiglia, aliyefariki tarehe 27 Agosti 2025. Wakati wa Misa ya mazishi, Askofu Mkuu Repole alirejea ujumbe uliotumwa na Papa Leo XIV ambao ulionesha Mchungaji aliyefariki kama "mchungaji mpole na mwenye busara, mwaminifu kwa watu kila wakati na msikivu kwa walio hatarini zaidi." Mamlaka nyingi za kiraia na kijeshi pia zilihudhuria mazishi hayo, akiwemo Meya wa mji mkuu wa Piemonte Stefano Lo Russo, na Mkuu wa Mkoa wa Piemonte, Alberto Cirio. Askofu mkuu Repole alisisitiza kuwa Askofu Mkuu wa Torino tangu 2010 hadi 2022 na aliyewahi kuwa Makamu rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia tangu 2010 hadi 2015, Askofu Mkuu Nosiglia, bado ni mtu anayependwa sana, na Kanisa hili kuu linaonesha hisia kubwa ya shukrani kila mmoja wetu kwa maisha na huduma yake."
Baraza la Maskofu Italia:salamu zake za rambi rambi
"Tunatoa rambirambi zetu kwa kuondokewa na Monsinyo Cesare Nosiglia, Askofu Mkuu Mstaafu wa Torino na aliyekuwa, Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, Katibu wa Tume ya Maaskofu ya Elimu Katoliki (1995-2000), ambayo alikuwa Rais wake kuanzia 2000 hadi 2015. Katika ujumbe wa Baraza la Maaskofu, uliotiwa saini na Kardinali Matteo Zuppi Rais wa CEI na Katibu Mkuu Monsinyo Giuseppe Baturi, Askofu Mkuu Nosiglia anaelezwa kuwa ni mtu wa hali ya juu ya kiroho ambaye "alitumikia Kanisa nchini Italia kwa kusoma alama za nyakati, akisikiliza mahitaji yaliyokuwa yanajitokeza kwa miaka mingi, kwa jicho la makini kwa wasio na ajira na watu wa Sinthi na Warom."
Maisha kwa Kanisa
Kwa kujitolea hasa, kwa katekesi tangu miaka ya 1970, alikuwa miongoni mwa waendelezaji wa hati ya msingi Upyaishaji wa Katekesi (1970), ambayo baadaye iliunga mkono mpango wa Katekisimu za Kanisa la Italia. Ahadi hii ilihitimishwa na mwelekeo wake wa kuwa mkuu ya Ofisi Kitaifa ya Katekesi kutoka 1986 hadi 1991, ambayo tayari alikuwa naibu mkurugenzi. Mchango wake kwa Kanisa la Roma, ambalo alihudumu kama msaidizi na makamu, ulikuwa muhimu pia, kama mshiriki mwenye bidii wa Kardinali Camillo Ruini."
Mtu Mwenye Imani kali
"Tumeshuhudia imani yake kubwa,katika hafla ya Maonesho ya Sanda Takatifu, hasa Jumamosi Takatifu 2020 (Aprili 11) katikati ya janga la UVIKO-19. Maneno yake: 'Sanda hiyo, mbali na kuwa kioo cha Injili, haitupatii tu mwili wa Yesu ulioteswa katika ishara za ibada yake ya Injili ambayo inakumbukwa katika siku hii ya Pasaka, Ufufuko.' Maisha yake yalishuhudia hili hadi mwisho,” ujumbe huo unaelezea. Askofu Mkuu Mstaafu Nosiglia pia atakumbukwa huko Susa, ambapo alikuwa msimamizi wa kitume, na misa ya kumbukumbuka itafanyika trahe 31 Agosti 2025 alasisri saa 9:30 masaa ya Ulaya katika sherehe ya Ekaristi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Giusto, inayoongozwa na Monsinyo Alfonso Badini Confalonieri na Jimbo kuu la Roma litaadhimisha kumbumubuka kwa Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Bernadette mjini Lourdes, wakati wa hija ya Jimbo hilo inayoendelea hadi tarehe 1 Septemba.