杏MAP导航

Tafuta

Papa LeoXIV  aliondoka Castel Gandolfo  usiku wa tarehe 19 Agosti 2025 kurudi mjini Vatican. Papa LeoXIV aliondoka Castel Gandolfo usiku wa tarehe 19 Agosti 2025 kurudi mjini Vatican. 

Papa kwa Ukraine:"Kuna matumaini,lakini lazima tufanye kazi kwa bidii na kuomba sana"

Papa alijibu maswali ya waandishi wa habari usiku wakati anatoka Castel Gandolfo kwamba:"Ni lazima kweli tutafute njia ya kusonga mbele,kupata amani!”Ni katika muktadha wa vita vinavyoendelea huko Ucraine:Papa aliondoka Villa Barberini muda mfupi kabla ya 3:00 usiku aliwasalimia baadhi ya watu waliokuwa wamekusanyika kusubiri kuondoka kwake.Na kuhusu siku zake 100 za kwanza za upapa, alisema:Zimekuwa baraka kutoka kwa Mungu na ninapokea sana."

Na  Campisi, Daniele Piccini  na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alijibu waandishi wa habari kuwa:"Kuna matumaini, lakini bado tunahitaji kufanya kazi kwa bidii, kuomba kwa bidii, na kutafuta kweli njia ya kusonga mbele, ili kupata amani,” kuhusu mazungumzo ya kumaliza mzozo wa Ukraine, kabla ya kurejea mjini Vatican, waliokuwa wakimsubiri nje ya Villa Barberini huko Castel Gandolfo. Papa aliondoka kwenye makazi yake majira ya saa 3:00 usiku tarehe 19 Agosti 2025. Saa moja kabla ya hapo, alikuwa ametokea kuwasalimia watu wengi waliokuwa wamekusanyika barabarani wakisubiri kuondoka kwake. Tayari kulikuwa na giza wakati alipopita kwenye lango la Villa Barberini na kusimama ili kuzungumza na baadhi ya waamini waliokuwa wakimsherehekea. Muda mfupi baadaye, Papa hakukwepa maswali ya waandishi wa habari, na kuhusu uwezekano wa mikutano na viongozi fulani, alisema kwamba "mtu fulani" alikuwa akiwasiliana naye mara kwa mara. “Tuombe na tutafute njia za kusonga mbele,” aliongeza.

Il Papa mentre esce da Villa Barberini

Papa akitoka katika Makao ya Barberini

Kuhusu swali la kukaa kwake Castel Gandolfo, Papa alijibu: "Kuwa hapa ni baraka; nimefurahishwa sana na kukaribishwa na watu." Pia alikumbuka ziara yake ya  kwenye "Madhabahu ya Mama Yetu, ambapo Papa Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili pia alitembelea." Hatimaye, alipoulizwa kuhusu siku zake 100 za kwanza za upapa, alisisitiza kwamba zimekuwa "baraka kutoka kwa Mungu." "Nimepokea sana, ninaamini sana neema za Bwana, na ninashukuru sana kwa ukaribisho huu nilioupata. Nawashukuru wote," alimalizia kabla ya kulifikia gari lililomrudisha mjini Vatican.

Il Papa mentre si allontana in auto

Papa akiwa anaondoka kwenye gari

Likizi ya Pili ya Castel Gandolfo

Papa Leo XIV alihamia Castel Gandolfo kwa kipindi cha pili cha mapumziko, tarehe 13 Agosti, baada ya kukaa zaidi ya majuma mawili huko  mwezi Julai. Alikuwa na mikutano minne na waamini katika siku hizi saba. Tarehe 15 Agosti, katika Maadhimisho ya Kupalizwa kwa Bikira Maria, Papa aliadhimisha Misa Takatifu katika Parokia ya Kipapa ya Mtakatifu Tommas wa Villanova, karibu na Villa Barberini, makazi yake majira ya kiangazi. Katika mahubiri yake, alikazia kwamba:  “ndiyo” ya Maria.  “bado  ni hai na ingali inapinga kifo” katika wale ambao leo hii wanashuhudia “imani,” “haki,” “upole,” na “amani.” Katika sala ya Malaika wa Bwana kwa njia hiyo  kwa kuangalia matukio ya kimataifa ya sasa, aliwataka watu si kujiuzulu wenyewe kwa "kueneza mantiki ya migogoro na silaha."

Siku na Maskini na Wasio na Makazi wa Albano

Dominika iliyopita, tarehe 17 Agosti  2025 ilikuwa siku iliyojaa mikutano. Awali ya yote asubuhi, Papa aliongoza ibada ya Misa kwa ajili ya maskini wa eneo hilo, wasio na makazi, wageni wahudumu wa mapokezi na nyumba za familia katika jimbo, katika Madhabahu ya Maria wa Rotonda huko Albano. Wahudumu  wa Caritas na wahudumu wa vituo vya kusikiliza, wakipendekeza kwamba walete ulimwenguni "si moto wa silaha, au hata ule wa maneno yanayowachoma wengine," lakini ule wa "upendo, unaojishusha na kutumikia, ambao unapinga kutojali kwa uangalifu na kiburi kwa upole; moto wa wema, ambao haugharimu kama silaha, lakini huifanya upya ulimwengu kwa uhuru."

Karibu katika mitaa ya mji wa Lazio kabla ya sherehe, Papa Leo XIV  pia alitembelea maonesho ya: "Ishara za Matumaini" yaliyoandaliwa na Caritas Jimbo.  Baadaye alirudi Castel Gandolfo kwa ajili ya Sala ya Malaika wa Bwana. Na baada ya sala ya Maria aliomb "ili jitihada za kumaliza vita na kuendeleza amani ziweze kufanikiwa; kwamba, katika mazungumzo, manufaa ya watu wote daima huja kwanza."

Wakati mzuri uliotazamiwa sana ulikuwa ni chakula cha mchana katika eneo la Borgo Laudato si' pamoja na takriban watu mia moja maskini, wasio na makao, na wenye mahitaji wakisaidiwa na Caritas Albano. Mwanzoni mwa mlo, Papa Leo XIV  alikumbusha umuhimu wa kushiriki "ishara hiyo, muhimu sana kwetu sote, ambayo ni kumega mkate, kumega mkate pamoja, ishara ambayo tunamtambua Yesu Kristo kati ya watu wake."

Kutembelea Madhabahu ya Mentorella

Hatimaye, asubuhi ya  tarehe 19 Agoti alifanya ziara ya faragha kwa Madhabahu ya Mama Yetu, Mama wa Neema, Mentorella, huko Guadagnolo, kitongoji kidogo cha Capranica Prenestina, katika Jimbo la  Palestrina. Hapo, Papa alisimama katika sala, akawasha mshumaa chini ya sanamu ya Bikira, akionesha ombi maalum kwa amani ya ulimwengu. Pia alitumia muda kukaa pamoja na Watawa wa Ufufuko, ambao wamekabidhiwa uchungaji wa mahali hapo patakatifu na kula chakula cha mchana pamoja nao. Kisha akarudi Villa Barberini, kabla ya usiku kurudi mjini Vatican.

Papa arudi Vatican 19 Agosti

20 Agosti 2025, 08:37