Papa awaombea watu wa Pakistan,India na Nepal walioathiriwa na mafuriko makubwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV , mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana akiwa katika lango la jengo la kipapa huko Castel Gandolfo, Dominika tarehe 17 Agoati 2025, aliwaelekea waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja huo, kwa kusema kuwa: “ Wapendwa kaka na dada niko karibu na watu wa Pakistan, India na Nepal walioathiriwa na mafuriko makubwa. Ninasali kwa ajili ya waathiriwa na familia zao, na wote wanaoteseka kutokana na msiba huu.”
Tuombeee jitihada za kuleta amani
Na zaidi aliongeza Papa: “Tuombe kwamba jitihada za kumaliza vita na kuendeleza amani zifanikiwe; kwamba, katika mazungumzo, manufaa ya pamoja ya watu daima yatatangulia.
Mipango ya upendo ya kiutamaduni na uinjilishaji
Papa akigeukia sehemu nyingine alisema: “Wakati wa kiangazi hiki, ninapokea habari za mipango mingi na tofauti ya kiutamaduni na ya uinjilishaji, ambayo mara nyingi hupangwa katika maeneo ya likizo.” Na kwa njia hiyo “ni vizuri kuona jinsi shauku kwa Injili inavyochochea ubunifu na kujitolea kwa vikundi na vyama vya kila kizazi.” Katika mutadha huo, Papa alisema: “Ninafikiria, kwa mfano, kuhusu misheni ya vijana iliyofanyika hivi karibuni huko Riccione(Italia). Nawashukuru waandaaji na wote walioshiriki kwa namna mbalimbali katika matukio haya.”
Salamu mbalimbali kwa mahujaji
Papa Leo XIV hakuwasahau wanahija na waamini kwamba walifoka huko Castel Gandolfo kuwa: “ Ninawasalimuni nyote mliopo leo hapa Castel Gandolfo. Hasa, nina furaha kuwakaribisha kikundi cha AIDO kutoka Coccaglio, kuadhimisha miaka 50 ya kujitolea kwa maisha, wafadhili wa damu wa AVIS waliokuja kwa baiskeli kutoka Gavardo (Brescia), vijana kutoka Casarano, na watawa Wafransiska wa Mtakatifu wa Antoni. Na zaidi wanahija wengi katika madhabahu ya Maria ya huko Piekary, nchini Poland.” Papa Leo XIV alihitimisha kwa kuwatakia wote Dominika Njema!
Makala kuhusu Jubilei ya vijana iliyofanyika kuanzia tarehe 28 Julai hadi tarehe 3 Agosti 2025.
Katika makala ya I ni Vijana wawili kutoka Jimbo kuu la Dar Es Salaam na Jimbo jipya la Bagamoyo, nchini Tanzania ambayo wanayo mengi ya kutueleza. Usikose kufuatilia makala hizi. lakini kwa sasa bonyaza hapa kusikiliza sehemu ya kwanza: