杏MAP导航

Tafuta

2025.08.08 Ujjumbe wa wawakilishi wa kisiasa na watu mashuhuri kutoka Ufaransa. 2025.08.08 Ujjumbe wa wawakilishi wa kisiasa na watu mashuhuri kutoka Ufaransa.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:”msiongope kukuza mafundisho ya Kanisa,ni wokovu”

Papa Leo XIV amekutana na ujumbe wa wawakilishi wa kisiasa na watu mashuhuri kutoka Ufaransa na ameonya dhidi ya "ulei usioeleweka wakati mwingine" na kuelekweka kama "ukoloni wa kiitikadi."Mafundisho ya Kanisa ni fundisho la wokovu;hatupaswi kuogopa kuyakuza,kutia moyo kushughulikia masuala makuu ya kijamii kwa nguvu ya upendo,kwa niaba ya manufaa ya wote.Ukristo sio ibada ya kibinafsi,bali hujitolewa kwa ahili ya Ulimwengu wa kidugu zaidi."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 28 Agosti 2025,  aliwakumbusha kwa uwazi wajumbe arobaini kutoka  ujumbe wa wawakilishi wa kisiasa na watu mashuhuri wa kiraia wa Val de Marne, katika Jimbo Katoliki la  Créteil la Ufaransa wakiwa wamefika katika hija jijini Roma, akianza Hotuba yake kwa Lugha ya Kifaransa  na kutoa salamu kwa Askofu Dominique Blanchet  na wote alioambatana nao. Nina furaha kukukaribisha katika safari yako ya imani: kurudi kwa ahadi zenu za kila siku mkiwa mmeimarishwa na tumaini, thabiti zaidi katika kufanya kazi ili kujenga ulimwengu wa haki zaidi, wa kibinadamu zaidi, zaidi wa kidugu, ambao unaweza tu kuwa ulimwengu uliojaa Injili zaidi. Tukikabiliwa na mielekeo mbalimbali inayoathiri jamii zetu za Magharibi, sisi, kama Wakristo, hatuwezi kufanya vizuri zaidi kuliko kumgeukia Kristo na kuomba msaada wake katika kutekeleza majukumu yetu.

Papa alikutana na Ujumbe kutoka Ufaransa
Papa alikutana na Ujumbe kutoka Ufaransa   (@VATICAN MEDIA)

Hii ndiyo sababu safari yenu, zaidi ya kujitajirisha kibinafsi, ni ya umuhimu mkubwa na ya manufaa makubwa kwa wanaume na wanawake mnaowahudumia. “Na ni jambo la kusifiwa zaidi kwa sababu huko Ufaransa, kutokana na kutoeleweka kwa dini wakati mwingine, si rahisi kwa kiongozi aliyechaguliwa kuchukua hatua na kuamua kwa upatano na imani yake katika utekelezaji wa majukumu ya umma. “Wokovu ambao Yesu aliupata kupitia kifo na ufufuko wake unajumuisha nyanja zote za maisha ya mwanadamu, kwa kuweka ndani utamaduni, uchumi, na kazi, familia na ndoa, kuheshimu utu na uhai wa binadamu, na afya, pamoja na mawasiliano, elimu, na siasa. Ukristo hauwezi kupunguzwa katika ibada ya kibinafsi tu, kwa sababu inahusisha njia ya kuishi katika jamii iliyo na alama ya upendo kwa Mungu na jirani, ambaye, katika Kristo, si adui tena bali ni ndugu.

Eneo lao kwa hiyo , mahali pa ahadi zao, lazima lishughulikie masuala makubwa ya kijamii kama vile vurugu katika baadhi ya vitongoji, ukosefu wa usalama, hatari, mitandao ya madawa ya kulevya, ukosefu wa ajira, kutoweka kwa urafiki ... Ili kushughulikia masuala haya, viongozi wa Kikristo hupata nguvu kutokana na fadhila ya upendo ambayo imekaa ndani yao tangu ubatizo wao. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, "nguvu inayoweza kuhamasisha njia mpya za kushughulikia matatizo ya ulimwengu wa leo na kufanya upya miundo, mashirika ya kijamii, na mifumo ya kisheria kutoka ndani."

Papa alikutana na ujumbe kutoka Ufaransa
Papa alikutana na ujumbe kutoka Ufaransa   (@VATICAN MEDIA)

Kwa mtazamo huo Baba Mtakatifu Leo amesisitiza kuwa , upendo unakuwa upendo wa kijamii na kisiasa: upendo wa kijamii hutufanya kupenda wema wa wote na kutafuta kwa ufanisi mema ya watu wote" ( Hati ya Mafundisho Jamii ya Kanisa kifungu,207). Ndiyo maana viongozi wa Kikristo wamejitayarisha vyema kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa leo, kiasili kwa kadiri wanavyoishi na kutoa ushuhuda wa imani itendayo kazi ndani yao, uhusiano wao binafsi na Kristo anayewaangazia na kuwapa nguvu hii. Yesu anaeleza kwa nguvu: “Maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote” (Yh 15:5); kwa hivyo, haishangazi kwamba ukuzaji wa "maadili" - hata kama ya kiinjili - lakini "yakiwa yameachwa" na Kristo, mwandishi wao, hayana uwezo wa kubadilisha ulimwengu. Kwa hiyo, Papa alisema kwamba Askofu Blanchet alimuomba ushauri. Papa alisema kuwa ushauri wa kwanza na wa pekee: "ningewapa ninyi kuungana kwa ukaribu zaidi na Yesu, kuishi kulingana naye na kutoa ushahidi kwake. Hakuna utengano katika utu wa mtu na umma: hakuna mwanasiasa wa upande mmoja na Mkristo kwa upande mwingine. Lakini kuna mwanasiasa ambaye, chini ya mtazamo wa  Mungu na dhamiri yake, anaishi ahadi na wajibu wake kwa njia ya Kikristo!”

Kwa hiyo wao wameitwa kujiimarisha katika imani, kuimarisha uelewa wao  wa mafundisho—hasa Mafundisho ya kijamii, ambayo Yesu alifundisha Ulimwengu, na kuyaweka katika vitendo katika utekelezaji wa majukumu yao  na katika kuandika sheria. Misingi yake kimsingi inapatana na asili ya kibinadamu, sheria ya asili ambayo kila mtu anaweza kuitambua, hata wasio Wakristo, hata wasioamini. Kwa hiyo, hatupaswi kuogopa kuipendekeza na kuitetea kwa usadikisho: ni fundisho la wokovu linalolenga mema ya kila mwanadamu, katika ujenzi wa jamii zenye amani, upatano, ustawi na maridhiano.

Papa akutana na ujumbe kutoka Ufaransa
Papa akutana na ujumbe kutoka Ufaransa   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alieleza anavyojua vyema kwamba “kujitolea kwa uwazi kwa Mkristo kwa kiongozi wa umma si rahisi, hasa katika jamii fulani za Magharibi ambako Kristo na Kanisa lake wanatengwa, mara nyingi kupuuzwa, wakati mwingine kudhihakiwa. Papa pia alisema anavyofahamu shinikizo, maagizo ya vyama, na "ukoloni wa kiitikadi" - kuazima usemi unaofaa kutoka kwa Papa Francisko - ambao wanasiasa wanatibiwa. Lazima wawe na ujasiri: ujasiri wa kusema "hapana, siwezi!" wakati ukweli uko hatarini. Hapa pia, panahitaji muungano tu na Yesu-Yesu aliyesulubiwa!-ambaye atawapa ujasiri wa kuteseka kwa jina lake. Aliwaambia wanafunzi wake: "Ulimwenguni mtakuwa na dhiki, lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu!"(Yh 16:33 ).”

Papa Leo XIV aliwashukuru kwa ujio wao na  kuwahakikishia faraja yake ya dhati wanapoendelea na kazi yao ya kuwatumikia wananchi wao. “Dumisheni tumaini la Ulimwengu bora; dumisha uhakika kwamba, ukiunganishwa na Kristo, juhudi zenu zitazaa matunda na kupata thawabu.” Papa kwa kuhitimisha aliwakabidhi wao na  nchi yao kwa ulinzi wa Mama Yetu wa Kupalizwa, na kwa moyo mkunjufu alitoa Baraka yangu ya Kitume.

Papa akutana na Ujumbe kutoka Ufaransa
28 Agosti 2025, 12:48