杏MAP导航

Tafuta

2025.08.23 Papa na Washiriki wa mikutano mikuu ya Mashirika mbali mbali ya kitawa. 2025.08.23 Papa na Washiriki wa mikutano mikuu ya Mashirika mbali mbali ya kitawa.  (@Vatican Media)

Papa kwa mashirika 4 ya kitawa:Hata leo,kuna uhitaji mkubwa wa familia kuungwa mkono na kutiwa moyo!

Papa Leo XIV alikutana mjini Vatican na washiriki wa Mikutano mikuu ya Mashirika 4 ya kitawa ya kike,aliwashauri wapyaishe jitihada:Endeleeni na kazi mliokabidhiwa kwa kufanya familia kuwa karibu na watu mnaowahudumia kwa sala,kuwasikiliza,kuwapa ushauri,msaada,kukuza na kueneza hali nyingine mnayojikita nayo kwa roho ya nyumba ya Nazareth."

Na Angella  Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana mjini Vatican, Jumamosi tarehe 23 Agosti 2025 na Washiriki wa Mikutano Mikuu ya Mashirika ya kitawa ya kike manne: wamisionari wa Familia Takatifu ya Nazare, Shirika la Mabinti wa Nazareth, Taasisi ya Kitume ya Familia Takatifu na Watawa wa Upendo wa Mtakatifu Maria wajulikanao kama Washauri Jema. Kama kawaida yake, Papa alianza kwa ishara ya Msalaba: "Kwa ajina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amani iwe kwenu. Habati za Asubuhi ninyi nyote." Aliongeza kwa kuwashuru uvumilivu wao wa asubuhi. Papa alisema kwamba Mikutano yao mikuu ni wakati wa neema, zawadi kwa ajili ya Kanisa zaidi ya kuwa kwa ajili ya mashirika yao. Papa aliwasalimia Wakuu wa Mashirika waliokuwapo, wengine wapya, halafu wale ambao  wamemaliza muda wao.  Papa alibainisha jinsi ambavyo "Mikutano yao mikuu imefanyika wakati wa Jubilei ya Matumaini. Tumaini, kama Mtakatifu Paulo asemavyo, halikatishi tamaa; ni tunda la wema uliothibitishwa na huhuishwa na upendo wa Mungu unaomiminwa ndani ya mioyo yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu (rej. Rm 5:5)."

Papa akutana na watawa wa mashirika manne ya kike
Papa akutana na watawa wa mashirika manne ya kike   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu alingeza kusema kuwa "Maneno haya yanafaa sana kuelezea utajiri waliouleta hapo, katika ukumbi huo mahali walipokuwa wamekaa mjini Vatican na kwamba wameleta zawadi ya karama ambayo Roho Mfariji aliwahi kuwapatia Waanzilishi wao,na ambayo inaendelea kufanywa upya;" Wai wanaleta uwepo wa Bwana mwaminifu na waliojaliwa katika historia za Taasisi zao; wanabeba wema wa wale waliowatangulia, mara nyingi wakivumilia majaribu makali, waliitikia zawadi za Mungu. Haya yote yanawafanya wao kuwa mashuhuda bora, mashuhuda wa matumaini: hasa wa matumaini hayo ambayo yanatuhitaji tujitahidi daima kuelekea baraka zijazo na ambazo, kama watawa wanaitwa kuwa ishara na unabii(Fil 3,13-14; LG, 44)."

Misingi yao ya mashirika, Papa alisema, ina asili mbalimbali, inayohusishwa na maisha ya wanaume na wanawake wa Mungu ambao walijibu kwa ujasiri "ndiyo" kwa wito kama vile: Josep Manyanet, María Encarnación Colomina, Maria Luigia Angelica Clarac, Giuseppe Guarino, Carmela Auteri, Teresa Ferrara, na Agostino wa Montefeltro. Kwa wote, Roho Mtakatifu alitoa zawadi maalum kwa ajili ya manufaa ya wote, pia kwa msukumo wa shule kuu za kiroho, kama vile shule za Wafransiskani na Wasalesian. Walakini, kuna sifa moja ambayo wengi wao  wanafanana ile “hamu ya kuishi na kuwapitishia kaka na dada zao maadili ya Familia Takatifu ya Nazareti, makao ya sala, malezi ya upendo na kielelezo cha utakatifu na kwa njia hiyo,  Papa Leo XIV alipenda kutafakari juu hilo.

Papa akutana na mashirika manne ya kitawa
Papa akutana na mashirika manne ya kitawa   (@Vatican Media)

Mtakatifu Papa Paulo VI, wakati wa Ziara yake katika Nchi Takatifu, akizungumza na waamini katika Kanisa kuu la Kupashwa Habari alieleza matumaini yake kwamba, kwa kuwatazama Yesu, Maria na Yosefu, mtu anaweza kuzidi kuelewa umuhimu wa familia, ushirika wake wa upendo, uzuri wake rahisi na usio na uchungu, tabia yake takatifu na isiyoweza kukiukwa, ufundishaji wake wa upole na utendaji wake wa asili na usioweza kurejeshwa katika jamii. ( Hotuba katika Basilika ya Kupashwa habari, huko Nazareth, 5 Januari 1964).

Hata leo,  Papa Leo XIV aliongeza kusema: “kuna uhitaji mkubwa wa haya yote. Katika siku zetu, familia zinahitaji kusaidiwa, kukuzwa, na kutiwa moyo zaidi kuliko hapo awali: kupitia maombi, mfano, na hatua za haraka za kijamii, tayari kukidhi mahitaji yao. Ushahidi wao wa karama na kazi yao kama wanawake waliowekwa wakfu inaweza kufanya mengi katika suala hili."

Papa akutana na mashirikia manne ya kitawa wakiwa katika mkutano mkuu
Papa akutana na mashirikia manne ya kitawa wakiwa katika mkutano mkuu   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo Papa ametoa mwaliko, kutafakari juu ya yale Taasisi zao zimefanya kwa muda kwa ajili ya familia nyingi—wavulana, wasichana, mama, baba, wazee, na vijana—na pia kufanya upya kujitolea kwao  ili, kama liturujia inavyosema, “fadhila zile zile na upendo uleule wa Familia Takatifu” uweze kusitawi katika nyumba zetu (tazama Misale ya Roma, Misa ya Familia). Papa aliwahimiza waendelee na kazi walizokabidhiwa kwa "kujenga familia" na kukaa karibu na watu wanaowahudumia, kwa maombi, kusikiliza, ushauri na usaidizi, ili kukuza na kueneza, Roho ya ya Nyumba ya Nazareth katika mazingira mbalimbali ambayo wanafanyia kazi. Papa Leo XIV aliwashukuru kwa kazi wanazofanya sehemu nyingi sana za dunia. Amewapongeza katika Bwana kwa sala, na kuwakabidhi kwa maombezi ya Mama wa Mungu na Mtakatifu Joseph, na amewabariki kutoka moyoni mwake. Baada ya baraka aliwashukuru tena wote  na kuwatakia Mkutano mkuu mwema.

Salamu za Papa kwa watawa wa Mashirika menne ya kike
Salamu za Papa kwa watawa wa Mashirika menne ya kike   (@Vatican Media)
Hotuba ya Papa kwa watawa Agosti 23
23 Agosti 2025, 13:38