杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo XIV atakuwa na vijana wa Amerika kwa njia ya mtandao Novemba 21. Papa Leo XIV atakuwa na vijana wa Amerika kwa njia ya mtandao Novemba 21.  (@Vatican Media)

Novemba 21 Papa Leo XIV atafanya mkutano wa kwanza wa kidijitali na vijana wa Marekani

Kama sehemu ya kikao cha mawasilisho cha Baraza la Kitaifa la Vijana wa Kikatoliki(NCYC),saa 4:15 asubuhi masaa ya Marekani mashariki mnamo Novemba 21,Papa Leo XIV atashiriki katika kikao cha moja kwa moja kitakachoshirikisha takriban vijana 15,000 waliosajiliwa kwa sasa,wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18,kutoka vyama vya vijana Kikatoliki nchini kote.Papa atashirikiana nao moja kwa moja katika mazungumzo ya moja kwa moja kwa dakika 45.

Vatican News

Tarehe 21 Novemba 2025, Papa Leo XIV atashiriki katika mkutano wa moja kwa moja na Shirikisho la Kitaifa la Huduma ya Vijana wa Kikatoliki(NFCYM) wakati wa kikao cha mawasilisho ya Baraza la Kitaifa la Vijana wa Kikatoliki (NCYC) nchini Marekani. Muunganisho wa kwanza wa aina yake, kwa Papa Leo XIV, utafanyika saa 4:15 asubuhi (Saa za Mashariki mwa Marekani).

Papa atahutubia vijana 15,000 wa Marekani

Shirikisho lilikaribisha tangazo hilo kwa "heshima kubwa." Papa anatarajiwa kuhutubia takriban vijana 15,000 waliojiandikisha, wenye umri wa miaka  kati ya 14 hadi 18, kutoka vyama vya vijana Kikatoliki  nchini kote na kushiriki nao moja kwa moja katika mazungumzo ya moja kwa moja ya dakika 45. "Itakuwa ni fursa muhimu, kulingana na taarifa kutoka shirika, kwa vijana kupata uzoefu wa Kanisa la Ulimwengu, kushirikisha  wasiwasi na umakini kwa sauti zao, uzoefu, na matumaini." Christina Lamas, mkurugenzi mtendaji wa NFCYM, alisisitiza kwamba uwepo wa Papa "ni ukumbusho wa kina kwamba vijana ndio kiini cha Kanisa na kwamba sauti zao ni muhimu." Tukio hili linafuatia Jubilei  ya kwanza ya Washawishi wa Dijitali, ambayo ilifanyika tarehe 28 na 29 Julai  jijini  Roma ndani ya muktadha wa Jubilei ya Vijana (18 Julai -3 Agosti 2025.

Askofu Mkuu Pérez: 'Kama Papa Francisko, Papa Leo XIV anajali Vijana'

Askofu Mkuu Nelson J. Pérez, Askofu Mkuu wa Philadelphia,nchini Marakani ambaye ni Mshauri wa Maaskofu, na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NFCYM, alisema kuwa "ni kielelezo cha ukaribu wake kwa Wakatoliki vijana, akifuata nyayo za mtangulizi wake, Papa Francisko, ambaye aliwaita vijana 'sasa wa Mungu.' Kikundi teule cha vijana kitashiriki katika mazungumzo ya moja kwa moja na Papa Leo XIV wakati wa kikao. Mtandao wa Televisheni ya Neno la Milele (EWTN) utakuwa mshirika wa kipekee wa utangazaji na utiririshaji. Mkutano huo utaleta pamoja maelfu ya vijana Wakatoliki, viongozi wa wachungaji, mapadre, na watu wa kujitolea kutoka Marekani yotre kwa siku tatu za maombi, malezi, jumuiya na sherehe huko Indianapolis.

 

16 Agosti 2025, 11:30