Katekesi ya Agosti 13 itafanyika katika Ukumbi wa Paulo VI kutokana na joto kali!
Vatican News
Kutokana na halijoto ya juu inayotarajiwa, Katekesi ya Baba Mtakatifu Leo XIV katika siku ya Jumatano, tarehe 13 Agosti 2025 itafanyika tena katika Ukumbi wa Paul VI, mjini Vatican tena saa 4.00 kamili asubuhi majira ya Ulaya ambapo ni saa 5.00 asubuhi, majira ya Afrika Mashariki na Kati. Kisha Papa atatembelea Basilika ya Vatican(Mtakatifu Petro) ili kusalimia wale ambao hawataweza kupata viti katika Ukumbi na wengine watakuwa wamefuatilia Katekesi kwenye skrini. Skrini kubwa zitawashwa ili kufuatulia katekesi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na mbele ya Ukumbi wa Paulo VI.
Alasiri, Papa Leo XIV anatarajia kwenda hadi Castel Gandolfo kwa kipindi cha pili cha mapumziko kwenye makazi ya( Villa Barberini,) ndani ya Majengo ya Kipapa. Wakati wa kukaa huko, siku ya Ijumaa, tarehe 15 Agosti 2025, katika sherehe ya Kupalizwa kwa Bikira Maria Mbinguni, Papa ataadhimisha Misa Takatifu saa 4:00, asubuhi masaa ya Ulaya katika Parokia ya Mtakatifu Tommaso waa Villanova huko Castel Gandolfo, na saa 6.00 kamili masaa ya Ulaya atasali sala ya Malaika wa Bwana kutokea kwenye mlango wa Ikulu ya Papa katika Uwanja wa Libertà, huko Castel Gandolfo.
Dominika, tarehe 17 Agosti 2025 saa 3:30 asubuhi, masaa ya Ulaya, Baba Mtakatifu Leo XIV ataadhimisha Misa Takatifu katika Madhabahu ya Mtakatifu Maria wa Rotonda huko Albano Laziale, na maskini wanaosaidiwa na Caritas Jimbo na wafanyakazi wao. Saa 6.00 kamili masaa ya Ulaya, atasali Sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Uhuru(Piazza della Libertà,) huko Castel Gandolfo. Hatimaye, atashiriki chakula cha mchana na maskini na wale wanaosaidia wa Caritas Jimbo katika ukumbi wa Borgo Laudato si', ndani ya Majengo ya Kipapa.