“ Na Amani iwe“katika kitabu cha LEV kuhusu mada za kwanza za mafundisho ya Papa Leo XVI
Vatican News.
Tarehe 26 Agosti 2025, Nyumba ya Vitabu ya Vatican(LEV), imechapisha taarifa kuhusu kuchapishwa kwa kitabu kimoja kitakachopatikana kuanzia tarehe 27 Agosti 2025, chenye Kichwa: “Na Amani Iwe: Maneo kwa Kanisa na Ulimwengi ili kujua vizuri Papa Leo XIV, kupitia hotuba zake.” Kwa njia hiyo kitabu hicho kitapatika katika Nyumba ya vitabu hicho kuhusu Papa chenye kurasa 160 kinachouzwa kwa Euro 15, ya Papa Leo XIV kilichochapishwa kwa lugha ya Kitaliano, Kiingereza na kispanyola.
Kuanzia mara ya kwanza alipojitokeza mbele ya Ulimwengu mzima, Papa Leo XIV aliwaelekea wote, matashi ya amani ya “kutokuwa na silaha na kupokonya silaha”, ile ambayo alikuwa tayari ameandikia hata Christian de Chergé, Mkuu wa Tibhirine: tarehe 8 Mei, siku ya kuchaguliwa kwa Robert Prevost katika kiti cha upapa, kumbukumbu ya kiliturujia ya mashahidi wa Algeria iliadhimishwa. Katika hotuba zake za kwanza, Papa kutoka Amerika Kaskazini aliwasilisha kwa kila mtu baadhi ya vipaumbele vyake: “ukuu wa Mungu, ushirika katika Kanisa, kutafuta.”