杏MAP导航

Tafuta

Ujumbe wa Nia za Papa kwa Mwezi Agosti 2025:kutafuta njia za mazungumzo na kuepuka itikadi za kidini!

Katika ujumbe kwa njia ya video yenye nia ya maombi ya mwezi Agosti 2025,Papa Leo XVI anatualika kusali ili jamii ziepuke majaribu ya migogoro.Papa anatuhimiza pia kujibu migogoro kwa ishara za udugu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ulimwengu ambao kama alivyowaambia Wamisionari wa kikatoliki wa kidijitali kwamba, umevurugwa na uadui na vita, wakati wa woga na migawanyiko, katikati ya mtazamo wa jumla wa ubinafsi wenye nguvu na kama kuta zinazotutenganisha sisi kutoka kwa mtu mwingine, badala ya madaraja yanavyojengwa, Baba Mtakatifu Leo XIV alitoa ombi la watu wote wasikubali majaribu la migogoro. Na, hasa katika jamii ambazo pamoja kunaonekana kuwa ngumu zaidi, na kuepuka mizozo  kwa misingi ya kikabila, kisiasa, kidini au kiitikadi. Ni katika ujumbe kwa njia ya video uliochapishwa tarehe 29 Julai 2025 ambapo  tunachapisha mandishi kamili  kupitia Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni kote, kwa kuongozwa na mada ya: “Kuishi Pamoja: Tuombe kwamba jamii ambazo kuishi pamoja zinaonekana kuwa ngumu zaidi zisikubali kushindwa na majaribu ya migogoro kwa misingi ya kikabila, kisiasa, kidini au kiitikadi.”

Tuombe jamii ili ziishi vizuri na kuepuka majaribu

Katika ujumbe huo kwa njia ya Video Baba Mtakatifu Leo XIV amebaninisha kuwa: “Tuombe kwamba jamii ambazo katika kuishi pamoja kunaonekana kuwa mgumu zaidi zisikubali kushindwa na majaribu ya makabiliano kwa sababu za kikabila, kisiasa, kidini au kiitikadi.” Yesu, Bwana wa historia yetu, Rafiki mwaminifu na uwepo hai, Wewe ambaye huchoki kuja kukutana nasi, Sisi hapa, tunahitaji amani Yako. Tunaishi katika nyakati za hofu na migawanyiko. Wakati mwingine tunafanya kama tuko peke yetu, Kujenga kuta zinazotutenganisha sisi kwa sisi, Kusahau kwamba sisi ni kaka na dada." Ututumie Roho wako, Bwana, Ili kuwasha upya ndani yetu shauku  ya kuelewana, kusikiliza, kuishi pamoja kwa heshima na huruma. Utupe ujasiri wa kutafuta njia za mazungumzo, kujibu migogoro na ishara za udugu, kufungua mioyo yetu kwa wengine bila hofu ya tofauti. Utufanye kuwa wajenzi wa madaraja, ili kuweza kushinda mipaka na itikadi. Kuwa na uwezo wa kuona wengine kupitia macho ya moyo, na kutambua katika kila mtu hadhi isiyoweza kuharibika.”

Tushinde kiburi, majivuno na maneno ya kuudhi

Kwa mujibu wa maelezo ya Padre Cristóbal Fones, mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Maombi ya Papa Ulimwenguni kote alisema kuwa: “Sote tunaweza kukuza kuishi pamoja kwa amani.  Ili kufikia hilo, kwanza, ni lazima tujishughulishe wenyewe ili kuondoa kutoka mioyoni mwetu kiburi, majivuno, na maneno ya kuudhi ambayo yanaumiza na kuua. Kama vile Papa Leo XIV anavyotufundisha, amani hujengwa kutoka moyoni." Mjesuit huyo Padre Fones aliendelea kueleza: “Pili, ni lazima kuweka kando ubaguzi na kukabiliana na hofu ya wale ambao ni tofauti: Lazima tuwaendee wengine kwa heshima, tukiwasikiliza, ambao daima wana kitu cha pekee cha kutoa.  Kupitia mazungumzo, tunaweza kutafuta kile kinachotuunganisha na kufungua njia za ushirikiano kwa manufaa ya wote."

Kwa kuhitimisha Padre Fones alikumbuka kwamba: " Papa Leo XIV pia alisisitiza kwamba serikali lazima zifanye kazi ili kujenga jumuiya za kiraia zenye uwiano na amani. Hii inaweza kupatikana kwa kuwekeza katika familia; kulinda utu wa watu wote, haswa wale walio dhaifu na wasio na kinga; kutenda haki; kutafuta kurekebisha usawa; na kutetea ukweli, ambao ndio msingi wa kujenga uhusiano wa kweli."

Nia za maombi agosti 2025
29 Julai 2025, 19:19