杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo XIV:Hamwezi kumwita Mungu Baba ikiwa mnatunza ukatili mioyoni!

Siku zote Bwana hutusikiliza tunapoomba kwake,na ikiwa nyakati fulani anajibu kwa nyakati na kwa njia ambazo ni ngumu kueleweka,ni kwa sababu Yeye hutenda kwa hekima na uelekevu mwingi zaidi na zaidi ya ufahamu wetu.Kwa hiyo,hata katika nyakati hizi,tusiache kuomba kwa uaminifu:ndani yake tutapata mwanga na nguvu daima.Ni katika tafakari ya Papa Leo XIV wakati wa sala ya Malaika wa Bwana,27 Julai 2025 akiwageukia waamini na mahujaji wengi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 27 Julai 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV ameongoza tafakari ya Injili akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume, mjini Vatican kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Akianza tafakari hiyo Papa Leo alisema  "Leo hii Injili inatuwakilisha Yesu ambaye anafundisha mitume wake sala ya Baba Yetu Lc 11,1-13): Sala ambayo inaunagnisha wakristo wote. Katika hiyo Bwana anatualika kumwelekea Mungu tukimwita ‘Abba,’ yaani Baba, kama watoto kwa uraisi(…), imani ya kimwana(…) ari, uhakika wa kuwa wapendwa (KKK 2778). Kwa kufafanua vizuri sana, Katekisimu ya Kanisa katoliki katika mkutadha huo inasema: “Kwa njia ya sala ya Bwana, tulioneshwa sisi wenyewe, wakati anakuja kuonesha Baba, (KKK 2783.)Na ni kweli: kadiri tunavyosali zaidi kwa imani kwa Baba wa Mbinguni, ndivyo tunavyojigundua kuwa wana wapendwa  na zaidi tunatambua kuwa wa upendo (Rm 8,14-17).

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Papa Leo  XVI alindelea kusema kuwa: "Injili ya leo kisha inafafanua hali zote za ubaba wa Mungu kwa njia mbali mbali kama ile ya mtu ambaye anaamka katikati ya usiku ili kumsaidia rafiki amkaribishe mgeni hasiyetarajiwa; au kama yule mzazi ambaye anajishughulisha kutoa vitu vizuri kwa watoto wake.” Na “hii inatukumbusha kuwa Mungu kamwe hatugeuzii kisogo, tunapomwelekea Yeye, na wala ikiwa tutafika tumechelewa kubisha hodi katika mlango wake, labda baada ya makosa, fursa iliyokosekana, kushindwa na hata ikiwa kwamba ili aweze kutkaribisha lazima kutuamsha, watoto wake ambao wamelala katika nyumba(Lk 11,7).

Hakika, katika familia kuu ya Kanisa, Baba hasiti tushiriki katika ishara zake zote za upendo. Sikuzote Bwana hutusikiliza tunapoomba kwake, na ikiwa nyakati fulani anajibu kwa nyakati na kwa njia ngumu kuelewa, ni kwa sababu anatenda kwa hekima na uandalizi mkuu zaidi, kupita ufahamu wetu.

Umati katika Sala ya Malaika wa Bwana
Umati katika Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Kwa hiyo, hata katika nyakati hizi, tusiache kuomba kwa uaminifu: ndani yake tutapata mwanga na nguvu daima. Kwa kusali sala ya  Baba Yetu, hata hivyo, pamoja na kusherehekea neema ya uwana wa kimungu, pia tunadhihirisha kujitolea kwetu kuitikia zawadi hii, kupendana sisi kwa sisi kama ndugu katika Kristo.

Baba Mtakatifu alisisitiza kuwa “Mmoja wa Mababa wa Kanisa, akitafakari jambo hili, aliandika: “Tunapomwita Mungu ‘Baba Yetu,’ ni lazima tukumbuke wajibu wetu wa kuishi kama wana na binti,” na mwingine anaongeza: “Hamwezi kumwita Mungu wa wema wote kuwa Baba ikiwa mnatunza moyoni mwenu ukatili na usio wa kibinadamu; katika hali hiyo, kiukweli, hamna tena ndani yenu chapa ya wema wa Baba wa mbinguni.

Papa Leo XIV akiwabari waamini
Papa Leo XIV akiwabari waamini   (@Vatican Media)

Hatuwezi kumwomba Mungu kama "Baba" na kisha kuwa wagumu na wasiojali wengine. Badala yake, ni muhimu kujiruhusu kubadilishwa na wema wake, subira yake, rehema yake, ili kuakisi uso wake kama kioo chetu. Baba Mtakatifu Leo XIV alihitimisha, akisema kuwa liturujia ya leo inatualika katika sala na katika upendo kujisikia kupendwa na kupenda kama Mungu anavyotupenda: na upatikanaji, busara, ukarimu wa pande zote, bila hesabu. Tumwombe Maria tujue jinsi ya kuitikia wito, kudhihirisha utamu wa uso wa Baba.

Sala ya Malaika wa Bwana Papa Leo XIV

 

27 Julai 2025, 12:30