Papa Leo XIV,vijana:mtapata nguvu ya kuwa matumaini na nuru ya Ulimwengu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Habari za jioni! Good evening! Yesu anatuambia: ‘Ninyi ni chumvi ya dunia. Ninyi ni nuru ya ulimwengu," hayo yalikuwa ni maneno ya Papa. Kwa mshangao, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwasili katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mwishoni mwa Misa ya ufunguzi wa Jubilei ya Vijana, iliyoongozwa na Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji na mwenye jukumu la kuandaa Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya Matumaini 2025, ambapo baada ya Baraka alitangaza kufika kwake Papa akiwaomba mahujaji kutulia bila kuondoka ili Papa apate kuwasalimu.
Baada ya mzunguko mrefu wa kuzungukia uwanja na nje ya uwanja wa Mtakatifu Petro akiwa juu ya 杏MAP导航mobile, yaani kigari cha kipapa kati ya watu zaidi ya 120,000 ambao pia walijaza Uwanja wa Pio XII na Njia ya Conciliazione, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwasalimu watoto na vijana wote. Kiukweli umati wa watu ulilipuka kwa kusherehekea Papa alipowasili kwa gari lake lililo wazi juu.
Wengi walikusanyika kwenye vizuizi ili kumwona akipita na kumsalimia huku wakipiga picha au hata Clip za video kwa shangwe kuu. Wengine waliimba nyimbo, wakiinua simu zao kupiga picha za kumbu kumbu ya wakati muhimu na wengine hata kurusha zawadi. Papa kwa njia hiyo alisema:"Tunatumaini kwamba nyote siku zote mtakuwa ishara za matumaini ulimwenguni!" Baba Mtakatifu alisali baada ya kufikia hatua chache za Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, akiwahutubia vijana kwa lugha ya Kiitaliano ambao "walitoa maoni" kwa kila neno lake alilosema kwa vifijo na nderemo. "Leo tunaanza,” Papa alisema.
“Katika siku zijazo, mtapata fursa ya kuwa nguvu inayoweza kuleta neema ya Mungu, ujumbe wa matumaini, nuru kwa jiji la Roma, Italia, na ulimwengu mzima,” aliongeza Papa Leo XIV. Na kwa njia hiyo alitoa mwaliko kwamba: "Tutembee pamoja na imani yetu katika Yesu Kristo. Kilio chetu lazima pia kiwe kwa ajili ya amani duniani." Kisha Papa aliwaomba watu katika uwanja huo kurudia kusema: "Tunataka amani duniani." Kila mtu alijibu: "Tunataka amani duniani!”
Papa Leo XIV hakuishia hapo bali alikazia kusema: "Tuombe amani. Tunaomba amani. Sisi ni mashuhuda wa amani katika Yesu Kristo." Kama hiyo haitoshi aliongeza kuzungmza kwa lugha ya Kihispania: “Sisi ni mashuhuda wa amani ya Yesu Kristo, ya upatanisho, nuru hii ya ulimwengu ambayo sisi sote tunatafuta.”
“Kaka na dada, Bwana yu pamoja nasi, msaada wetu u katika jina la Bwana. Jina la Bwana na libarikiwe.” Kisha, baada ya kuwapa baraka, aliahidi kwamba: “Tutaonana. Tutakutana huko Tor Vergata. Muwe na juma jema!"