杏MAP导航

Tafuta

Mkusanyiko wa vijana  “Clameurs” huko Jambville Julai 24-28,2025. Mkusanyiko wa vijana “Clameurs” huko Jambville Julai 24-28,2025.  (AFP or licensors)

Papa Leo XIV kwa Maskauti wa Clameurs,huko Jambville:hifadhi ikolojia fungamani na zuia uharibifu wa mazingira!

Katika Mkusanyiko wa"Clameurs"huko Jambville,uliohitimishwa Julai 28,Papa Leo XIV aliwaandikia maskauti na viongozi wa Ufaransa,akiwahimiza wasikilize kilio cha uumbaji.Elimu ya ikolojia inahitajika kushughulikia upotezaji wa bayoanuwai,inayozidi kutoweka kwa kiasi na ambapo inatia changamoto ya dhamiri zetu lakini pia ukosefu wa usawa wa kimataifa,ukosefu wa maji ya kunywa na upatikanaji wa nishati kwa watu wengi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Baba Mtakatifu Leo XIV alituma kwa Maskauti na Viongozi wa Ufaransa katika ujumbe uliotumwa kwenye hafla ya Mkutano mkubwa wa "Clameurs" huko Jambville, ambao ulianza tangu tarehe 24 Julai na kuhitimishwa tarehe 28 Julai 2025. Mkutano huo ulipangwa kutafakari juu ya ulimwengu wa haki zaidi na endelevu, kwa lengo la kuchangia ulinzi wa mazingira, kuimarisha, kuweka" mawakala wa kawaida wa maskauti, katika huduma ya mabadiliko ya tabianchi. Papa Leo alisema “Wapendwa Skauti na Viongozi wa Ufaransa, ninatoa salamu zangu za dhati kwa hafla ya mkusanyiko wenu mkuu wa "Clameurs". Mmeamua kukutana na kutafakari juu ya ulimwengu wenye haki na endelevu zaidi, mkirejea kilio kinachoinuka kutoka duniani. Nimefurahishwa na mpango huu mzuri kwa sababu mnataka kuwa mawakala wa mabadiliko, kuweka Uskauti katika huduma ya changamoto za hali ya tabianchi.”

Dharura inawaajibisha

Baba Mtakatifu Leo kadhalika alisema kuwa “kuishi katika wakati wenye nguvu na wa pamoja wa michezo, mijadala na tafakari kuhusu masuala ya kijamii na kiikolojia, mngependa kutoa mchango wenu katika ulinzi wa mazingira na kuimarisha kujitolea kwenu kwa manufaa ya wote. Leo tunaalikwa kusikiliza kwa makini kilio cha uumbaji. Dharura hii inawajibisha wanadamu wote, ambao Mungu amewakabidhi kazi yake. Dhamiri zetu zinapingwa vikali na uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa. Dunia itu inakabiliwa na uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, kupotea kwa viumbe hai, kuzorota kwa maisha na uharibifu wa kijamii, ukosefu wa usawa wa kimataifa, ukosefu wa maji ya kunywa na upatikanaji wa nishati kwa watu wengi, elimu ya ikolojia ni muhimu kwa kila mtu kubadili utaratibu wa sasa. Kwa njia hiyo Papa alisema kuwa “Mkutano umewaruhusu kutambua njia na maelekezo mapya ya kulinda nyumba ya kawaida ya pamoja.” Wao ni vijana ambao wamejaa mawazo na shauku na wanataka kuushinda ulimwengu, si kuutiisha, bali kutumikia maisha yanayotoka kwa Mungu. Unyenyekevu, roho ya utumishi, na uhusiano wa kina na Kristo huwawezesha kukita maadili ya Kikristo ndani yao. Uongofu wa mambo ya ndani pekee hufanya iwezekanavyo mabadiliko katika tabia na mawazo, ambayo hutafsiri kuwa njia mpya ya kuishi katika ushirika na mazingira, Papa Leo alikazia.

Kuweni mabalozi wa udugu na amani

Kama maskauti wamezoea kuishi katika asili, kufanya vitu, kutafuta njia yao, na kuandaa michezo na mikesha; hii inawapelekea kuutendea uumbaji kwa heshima. Kwa hivyo, wanaweza kutoa mengi kwa jamii na mtindo wao wa maisha. Papa ana uhakika kwamba nyakati hizi kali wanazopitia zitawaruhusu kujitajirisha zaidi kwa maadili kama vile kukutana na kuwakaribisha wengine katika utofauti wao na ukamilishano. Kwa njia hiyo maskauti hao, Papa Leo XIV aliwaomba wawe mabalozi wa udugu na amani katika maisha yao wenyewe. wanatoka katika tamaduni na asili tofauti za kijamii, wenye miktadha na umri tofauti. Wao wanawasiliana na watu wazima na wazee. Huu ni utajiri, faida ambayo inawawezesha kuona mambo kwa maana kubwa zaidi na kuwazia ulimwengu wenye amani na silaha za Kikristo za imani, ukweli, haki, na Injili ya amani (Taz. Efe 6:11-17). Papa alisema wengi wao wamepokea sakramenti ya Kipaimara leo hii katika fursa hii ambayo ni ishara ya kujitolea kwao kwa Kanisa. Katika sakramenti hiyo, wanapokea kikamilifu Roho Mtakatifu, uwepo wa kimungu ambao unawaongoza, kuangaza, na kuwafariji katika safari yao ya imani. Kwa njia hiyo aliwaalika wamwombe mara kwa mara ili awajaze karama na neema zake.

Jukumu la kutoa ushuhuda wa imani Ulimwenguni

Papa alisema kuwa wao sasa umewekwa wakfu, wamepewa jukumu la kutoa ushuhuda wa imani yao ulimwenguni, kwa kuwa mawakala wa mabadiliko na matumaini katika jamii. Huu ni wajibu wa mfuasi mtendaji wa Kristo, aliyejitolea kutangaza Injili na kuwapenda wengine. Hata hivyo, haya yote yanawezekana tu kupitia maisha ya sala na urafiki na Mungu. Papa Leo XIV aliwahiliza wasonge mbele bila kukata tamaa, kuchoka na kulegea.Wajue kwamba kila mmoja wao ni wa kipekee katika uumbaji, wanapendwa kibinafsi na Bwana. Wasiache kamwe kuamini katika ulimwengu bora na ujio wa ustaarabu halisi wa upendo. Kama Papa Francisko alivyosema, nao pia wawe wajenzi wa madaraja kati ya vizazi, tamaduni na watu. Akiwakabidhi kwa maombezi ya Mtakatifu George, mlinzi wao, na utunzaji wa mama wa Bikira Maria, amewapa kwa moyo mkunjufu Baraka yake ya Kitume, ambayo aliwapatia pia viongozi wao na familia zao.

Papa Leo XIV Ujmbe Ufaransa

 

28 Julai 2025, 15:54