杏MAP导航

Tafuta

Baba Mtakatifu Leo XIV amelipongeza Gazeti la kila mwezi la “l’Osservatore di Strada” kwa kutimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 29 Juni 2022. Baba Mtakatifu Leo XIV amelipongeza Gazeti la kila mwezi la “l’Osservatore di Strada” kwa kutimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 29 Juni 2022. 

Papa Leo XIV: Kumbukizi ya Miaka Mitatu ya Jarida la "L'Osservatore di Strada"

Papa Leo XIV amewapongeza wote waliotumia karama na vipaji vyao kuandaa gazeti hilo la kipekee ambao kila Dominika wanaligawa gazeti hilo bure kwa mahujaji waliopo katika viwanja vya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican wakishiriki katika Sala ya Malaika wa Bwana na matukio mengine makubwa ya Kanisa yanayofanyika katika viwanja hivyo. Amesema wahudumu hao katika unyenyekevu wanamsaidia Baba Mtakatifu katika huduma ya uinjilishaji wa kina.

Na Sarah Pelaji, -Vatican

Baba Mtakatifu Leo XIV amelipongeza Gazeti la kila mwezi la “l’Osservatore di Strada” kwa kutimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 29 Juni 2022. Amewashukuru wafanyakazi wote wanaohudumu katika gazeti hilo kwamba wanafanya utume wenye maana kubwa katika Kanisa. “Ninataka kuungana nanyi katika sherehe hii kwa maneno machache yanayojumuishwa katika neno moja: ‘Asanteni sana.’ Asanteni nyote ambao kwa miaka mitatu mmekuwa mkiendeleza uzoefu huu mdogo lakini wenye maana kubwa katika Kanisa. Asanteni kwa jarida hili ambalo, kama alivyosema mtangulizi wangu Hayati Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 29 Juni miaka mitatu iliyopita, “walio wa mwisho wanakuwa wa kwanza tena ndiyo wahusika wakuu,” amesema Papa Leo XIV.

Jarida la L'Osservatore di Strada ni chombo cha uinjilishaji
Jarida la L'Osservatore di Strada ni chombo cha uinjilishaji   (AFP or licensors)

Amewapongeza wote waliotumia karama na vipaji vyao kuandaa gazeti hilo la kipekee ambao kila Dominika wanaligawa gazeti hilo bure kwa mahujaji waliopo katika viwanja vya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican wakishiriki katika Sala ya Malaika wa Bwana na matukio mengine makubwa ya Kanisa yanayofanyika katika viwanja hivyo. Amesema wahudumu hao katika unyenyekevu wanamsaidia Papa katika huduma ya uinjilishaji.

Kumbukizi ya Miaka mitatu ya Jarida la L' di Strada
Kumbukizi ya Miaka mitatu ya Jarida la L' di Strada

“Kazi yenu ni muhimu, kwa sababu inatukumbusha kuwa dunia inapaswa kutazamwa pia kutoka mitaani, kwa ujasiri wa kubadili mtazamo, kuvunja mifumo na mazoea ambayo mara nyingi hutuzuia kuona kwa undani zaidi na kumsikiliza yule asiye na sauti. Hongereni basi, na moyo wa ujasiri! Tuendelee mbele pamoja kwa imani, tukiendelea kuleta ndani ya miji ya wanadamu pia vipande vya mji wa Mungu, asanteni,” amesema Papa Leo XIV.

L'Osservatore
07 Julai 2025, 14:54