杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo wa XIV anawasihi watawa hao wa kike kutoka Ukraine walioko Roma kwa ajili ya Maadhimisho ya Mikutano yao mikuu sanjari na Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo wakite maisha yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. Papa Leo wa XIV anawasihi watawa hao wa kike kutoka Ukraine walioko Roma kwa ajili ya Maadhimisho ya Mikutano yao mikuu sanjari na Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo wakite maisha yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake.  (ANSA)

Papa Leo XIV Akutana na Kuzungumza na Watawa wa Ukraine: Mashuhuda wa Imani

Baba Mtakatifu Leo XIV aliwakaribisha kwa furaha watawa hao ambao walifika kuhudhuria Mkutano wao mkuu, wengine wakiwa Roma kwa ajili ya hija ya Jubilei. “Katika hali zote mbili mmekuja kwenye kaburi la Mtakatifu Petro ili kufufua upendo wenu kwa Bwana na uaminifu wenu kwa Kanisa. Papa Leo amewataka watawa hawa kuto akipaumbele cha kwanza kwa uwepo wa Mungu katika maisha na utume wao. Amewapongeza kwa kuwa ni mashuhuda wa imani thabiti.

Sarah Pelaji, -Vatican

Baba Mtakatifu Leo XIV hivi karibuni amekutana na kuzungumza na Masista wa Upendo wa Kimungu, Masista wa Mtakatifu Basili Mkuu, Masista Waaugustino wa Amparo na Masista Wafranciskani wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, jijini Vatican.  Papa Leo wa XIV anawasihi watawa hao wa kike kutoka Ukraine walioko Roma kwa ajili ya Maadhimisho ya Mikutano yao mikuu sanjari na Jubilei, wabaki wakitoa mizizi yao kwa Kristo Yesu na kuhakikisha kuwa Mungu kwa kila namna anabaki kuwa kila kitu katika maisha yao! Akirejea Falsafa ya Mtakatifu Augostino juu ya kipaumbele cha Mungu katika maisha ya mkristo, anasema ‘Mungu ni kila kitu chako. Ukiwa na njaa, Mungu ni chakula chako, ukiwa na kiu Mungu ni maji yako; ukiwa gizani, Mungu ni mwanga wako usiozimika, ukiwa uchi, Mungu ni vazi lako la milele.’

Watawa kutoka Ukraine: Mashuhuda wa imani na matumaini
Watawa kutoka Ukraine: Mashuhuda wa imani na matumaini   (ANSA)

Baba Mtakatifu Leo XIV aliwakaribisha kwa furaha watawa hao ambao walifika kuhudhuria Mkutano wao mkuu, wengine wakiwa Roma kwa ajili ya hija ya Jubilei. “Katika hali zote mbili mmekuja kwenye kaburi la Mtakatifu Petro ili kufufua upendo wenu kwa Bwana na uaminifu wenu kwa Kanisa. Mnatoka katika Mashirika yaliyoanzishwa katika nyakati na mazingira tofauti: Masista wa Shirika la Mtakatifu Basili Mkuu, Mabinti wa Upendo wa Kimungu, Masista wa Agostino wa “del Amparo” na Masista Wafrancisko wa Moyo Mtakatifu wa Yesu. Hata hivyo, historia zenu zinaonesha mwendo wa pamoja, ambapo mwanga wa mifano bora ya maisha ya kiroho ya zamani kama vile ya watakatifu: Augustino, Basili, na Francisko kupitia tafakari, ujasiri na utakatifu wa waasisi wenu wa mashirika, uliweza kuchochea na kukuza njia mpya za huduma hasa kwa ajili ya wanyonge: watoto, vijana maskini, yatima, wakimbizi na wahamiaji na baadaye wazee na wagonjwa, pamoja na huduma nyingine nyingi za matendo ya huruma,” alieleza Papa Leo XIV.

Papa Leo XIV: Mungu apewe kipaumbele cha kwanza katika maisha
Papa Leo XIV: Mungu apewe kipaumbele cha kwanza katika maisha   (ANSA)

Katika hali hiyo, Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, ulipokuwa ukizungumzia Mashirika ya kitawa yanayojishughulisha na huduma za matendo ya huruma, ulisisitiza umuhimu wa maisha ya wanashirika wao wote kuchangamshwa na roho ya kitume na kila tendo la kitume kuwa na uzima wa kiroho (rej. Waraka Perfectae caritatis, 8), ili watawa wajibu kwa ukamilifu wito wao wa kumfuasa Kristo Yesu na kumtumikia Kristo katika viungo vyake wakiwa na muungano wa ndani naye.

Watawa ni mashuhuda wa imani, mapendo na matumaini
Watawa ni mashuhuda wa imani, mapendo na matumaini   (ANSA)

Akirejea tafakari ya Mtakatifu Augustino amewataka watawa hao kujiuliza; Je, kwa kiasi gani hili ni kweli kwangu mimi? Ni kwa kiasi gani Bwana anatosheleza kiu yangu ya maisha ya upendo na ya mwanga? Amesema, maswali hayo ni muhimu kwani ndiyo mzizi wa maisha katika Kristo uliowafanya waliotutangulia ambao ni ndugu zetu walifanikiwa kuishi ukamilifu wa maisha hapa duniani ambao sifa zao zimeenea hadi ulimwenguni kote, kama ushuhuda wa uwepo wenu leo. “Kristo akae mioyoni mwenu kwa njia ya imani, mkiwa na mizizi na msingi katika upendo, mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, urefu, kimo na kina cha upendo wa Kristo, na kuujua upendo huo wa Kristo upitao elimu yote, ili mpate kujazwa na utimilifu wote wa Mungu” (Waefeso 3:17-19), amesema Papa Leo XIV. Aliwashukuru kwa kazi na uaminifu wao kwa Kristo Yesu katika maisha na utume wao nchini Ukraine kisha kuwaweka chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria Mama wa Kanisa, akawapa baraza zake za kitume.

Papa Leo XIV Watawa Ukraine
02 Julai 2025, 15:41