杏MAP导航

Tafuta

2025.07.27 Sala ya Malaika wa Bwana. 2025.07.27 Sala ya Malaika wa Bwana.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:kwa Vijana,Jubilei iwe fursa ya kukutana na Yesu na kuimarishwa imani!

Leo tunaadhimisha Siku ya Vya Mababu na Wazee Ulimwenguni,yenye kaulimbiu:Heri wale ambao hawajakata tamaa.Tuwatazame Babu na Bibi na wazee kama mashuhuda wa matumaini,wenye uwezo wa kuakisi njia ya vizazi vipya.Tusiwaache,bali tufanye agano la upendo na maombi pamoja nao.Ni maneo ya Papa baada ya Sala ya Malaika wa Bwana ambapo amekumbuka pia watu wanoteseka na vuguru duniani kote kwa namna ya pekee Thailand na Cambodia,Siria Kusini na Gaza.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume, huku akiwageukia waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 27 Julai 2025, alisema: " Kaka na dada leo tunaadhimisha Siku ya Tano ya Mababu na Wazee Ulimwenguni, yenye kaulimbiu: "Heri wale ambao hawajakata tamaa." Tuwatazame babu na Bibi  na wazee kama mashuhuda wa matumaini, wenye uwezo wa kuakisi njia ya vizazi vipya. Tusiwaache, bali tufanye agano la upendo na maombi pamoja nao.

Baba Mtakatifu Leo aidha aielekeza kwenye vurugu za vita kwamba “ Moyo wangu unawaendea wale wote wanaosumbuliwa na migogoro na vurugu duniani kote. Hasa, ninawaombea wale waliopatikana katika mapigano kwenye mpaka kati ya Thailand na Kambodia, hasa watoto na familia zilizohamishwa. Mfalme wa Amani awatie moyo wote kutafuta mazungumzo na upatanisho.”Kadhalika Papa alisema “ anasali kwa ajili ya wathirika wa vurugu kusini mwa Siria.”

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Ninafuatilia kwa masikitiko makubwa hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza, ambapo raia wamekandamizwa na njaa na wanaendelea kukabiliwa na ghasia na vifo. Ninarudia ombi langu la kutoka moyoni la kusitisha mapigano, kuachiliwa kwa mateka, na kuheshimu kikamilifu sheria za kibinadamu.” Kwa kuongeza Papa alisema “ Kila mwanadamu ana heshima ya asili aliyopewa na Mungu mwenyewe: Ninawasihi wahusika katika mizozo yote kutambua heshima hii na kusitisha kitendo chochote kinyume chake. Niwasihi wajadili mustakabali wa amani kwa watu wote na kukataa chochote ambacho kinaweza kuhatarisha. Ninamkabidhi Maria, Malkia wa Amani, wahanga wasio na hatia wa migogoro na viongozi wa serikali wenye uwezo wa kuimaliza.”

Papa Leo ametoa salamu kwa Radio Vatican /Vatican News ambao ili kuwa karibu na waamini na mahujaji wakati wa Jubilei, Vatican imezindua kituo kidogo chini ya nguzo ya Bernini, pamoja na Osservatore Romano. Asante kwa huduma yanu katika lugha nyingi, ambayo hubeba sauti ya Papa ulimwenguni. Na asante kwa waandishi wa habari wote wanaochangia mawasiliano ya amani na ukweli.”

Kituo cha Matangazo cha Radio Vatican katika nguzo za Bernini
Kituo cha Matangazo cha Radio Vatican katika nguzo za Bernini

Baba Mtakatifu Leo XIV  aliendelea kutoa salamu mbali mbali: "Nawasalimu ninyi nyote, kutoka Italia na sehemu nyingi za dunia, hasa babu na bibi kutoka Mtakatifu Cataldo, mapadre vijana Wakapuchini kutoka Ulaya, Wanafunzi wa Kipaimara kutoka Grantorto-Carturo, vijana kutoka Montecarlo ya Lucca, na Skauti wa Licata."

Katika lugha ya Kiingereza aidha alitoa "salamu za upendo wa pekee kwa vijana kutoka nchi mbalimbali, waliokusanyika mjini Roma kwa ajili ya "Jubilei ya Vijana," inayoanza kesho(28 Julai 2025)." Papa alisema: "Ninatumaini kwamba itakuwa kwa kila mmoja wenu fursa ya kukutana na Kristo na kuimarishwa naye katika imani yenu na katika kujitolea kwenu kumfuata Yeye daima.” Maneno hata aliyarudia hata kwa lugha ya Kihispania. Wakati huo huo aliwasalimia wengine:  “Ninawasalimu waamini kutoka Kearny (New Jersey), kikundi cha Tuzo za Muziki wa Kikatoliki na Chuo cha Majira cha EWTN. 

Kituo cha Matangazo cha Radio Vatican/ Vatican News/ Osservatore Romano
Kituo cha Matangazo cha Radio Vatican/ Vatican News/ Osservatore Romano

Bikira Maria wa Fiumarola

Papa alisema: "Usiku wa leo, kutakuwa na maandamano ya Mama Maria wa "Fiumarola" yatafanyika kwenye kadno ya ziwa Tiber: wale wanaoshiriki katika mapokeo haya mazuri ya Maria wajifunze kutoka kwa Mama wa Yesu ili kutekeleza Injili katika maisha yao ya kila siku! Nawatakia wote Dominika  njema!

Bikira Maria wa Fiumarola
Bikira Maria wa Fiumarola
Maria wa Fiumarola
Maria wa Fiumarola
PAPA LEO BAADA ANGELUS JULAI 27
27 Julai 2025, 12:45