Mshikamano wa Papa Leo XIV na Waathirika wa Kimbunga cha Danas, Nchini Taiwan
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Hivi karibuni kimbunga kiitwacho Danas kiliikumba nchi ya Taiwan, na kusababisha vifo vya watu wawili na zaidi ya majeruhi 500 ambao wanatibiwa. Baba Mtakatifu Leo XIV ametaarifiwa kuhusu madhara makubwa yaliyosababishwa na kimbunga hivi.
Baba Mtakatifu Leo XIV amewakumbuka na kuwaombea wahanga wa madhara ya kimbunga cha Danas na amewaelekeza viongozi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo kuwaonesha waathirika mshikamano wa wa huruma na upendo kwa kuwasaidia kwa hali na mali. Hayo yamebainishwa na Dr. Matteo Bruno, Msemaji mkuu wa Vatican. Zaidi ya watu 3, 000 wamehamishwa kutoka kwenye maeneo ya hatari na kupelekwa walau kwenye maeneo yenye usalama zaidi. Ukanda wa Budai ndio ulioathirika zaidi, kiasi cha kuharibu miundo mbinu na kwamba, sekta ya kilimo imeathirika zaidi.