杏MAP导航

Tafuta

2025.07.30 Katekesi ya Papa 2025.07.30 Katekesi ya Papa  (@Vatican Media)

Maombi ya Papa Leo XIV kwa ajili ya wakristo wanaoteseka:viongozi wawajibike!

Mwishoni mwa katekesi Baba Mtakatifu amepyaisha wito wake akionesha uchungu wa kina kufuatia na shambulio la kigaidi katika Parokia ya Komanda,huko DRC na kuwashauri wenye madaka ya uwajibikaji kushirikiana ili kuzuia vurugu na mateso dhidi ya waamini.Papa amekumbuka miaka 50 ya mkataba wa tukio la mwisho wa Helsinki:"ni muhimu kuhifadhi Roho ya Helsinki kwa kudumu katika mazungumzo na kuimarisha ushirikiano."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa maelfu na maelfu ya wanahija na waamini waliokuwa wameunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, wengi wao wakiwa ni vijana ambao wanashiriki Jubiei yao  , na ambao walifika kishiriki Katekesi ya kwanza ya Jumatano, mara baada ya mapumziko ya kiangazi, Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe 30 Julai 2025, ameshirikisha hisia zake, matarajio na mitazamo ya hali ya sasa iliyogubika dunia na kujeruhiwa na vurugu.

Kwa njia hiyo mara baada ya Katekesi na salamu, Papa alisema: “Narudia kuonesha tena huzuni yangu kwa shambulio la kikatili la kigaidi lililotokea usiku wa Julai 26-27 huko Komanda, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Wakristo zaidi ya arobaini waliuawa kanisani wakati wa mkesha wa maombi na nyumbani kwao. Baba Mtakatifu aliongeza "Ninapowakabidhi waathiriwa kwa rehema wa upendo ya Mungu, ninawaombea waliojeruhiwa na Wakristo ulimwenguni kote wanaoendelea kuteswa na jeuri na mateso, nikiwataka wale wenye majukumu ya ndani na nje ya nchi washirikiane ili kuzuia majanga kama hayo.”


Papa Leo XIV aidha alijikita kwenye mtazamo wa kumbukizi ya kihistoria barani Ulaya kwamba:“ Tarehe 1 Agosti ni kumbukumbu ya miaka 50 tangu kutiwa saini kwa Sheria ya Mwisho ya Helsinki.  Kwa kuendeshwa na nia ya kuhakikisha usalama katika muktadha wa Vita Baridi, nchi 35 zilianzisha enzi mpya ya kijiografia na kisiasa, na kuhimiza ukaribu kati ya Mashariki na Magharibi. Tukio hilo pia liliashiria shauku mpya katika haki za binadamu, kwa kuzingatia hasa uhuru wa kidini, ikizingatiwa kuwa mojawapo ya misingi ya usanifu wa ushirikiano wa wakati huo wa "Vancouver hadi Vladivostok".

Ushiriki hai wa Vatican katika Mkutano wa Helsinki, Papa LeoXI aliongeza kuwa: “uliowakilishwa na Agostino Casaroli,(Wakati ule alikuwa Mwakilishi wa Kipapa katika Baraza hilo).  ulisaidia kukuza kujitolea kisiasa na kimaadili kwa amani. Huo ulikuwa Mkutano wa Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (CSCE) wa mwaka 1975, ambapo nchi 35 zilishiriki, zikiwemo Marekani, Canada na Muungano wa Kisovieti, pamoja na takriban mataifa yote ya Ulaya. Kwa njia hiyo Papa Leo XIV alisema: “Leo hii  zaidi ya hapo awali ni muhimu kuhifadhi roho ya Helsinki: kudumu katika mazungumzo, kuimarisha ushirikiano, na kufanya diplomasia ambayo ni njia inayopendekezwa ya kuzuia na kutatua migogoro.”

Wito wa Papa baada ya katekesi

 

 

 

30 Julai 2025, 12:01