Salas Casta?eda ni mratibu mpya wa ziara za Papa
Vatican News
“Papa Leone XIV amemkabidhi Monsinyo José Nahúm Jairo Salas Castañeda, Afisa wa Kitengo cha Mambo ya Jumla cha Sekretarieti ya Vatican, Jukumu la kuratibu ziara za Kitume. Tangazo hilo, lilitolewa tarehe 21 Juni 2025 na Askofu Mkuu Edigar Pen?a Parra, Katibu Msaidizi wa Vatican, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana. Ndivyo inasomeka tangazo lililochapishwa kwenye ukurasa wa X wa Sekretarieti ya Vatican “Terza Loggia.”
Kardinali George Koovakad, alianza kujikita na uratibu wa Ziara za Papa Francisko kunako 2021 na Desemba iliyopita aliteuliwa kuwa Kardinali na wakati huo huo tarehe 21 Januari 2025 akateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini.
Wadhifa wake: monsinyo José Nahum Jairo Salas Castañeda alizaliwa mnamo tarehe 11 Julai 1978 huko Mtakatifu Klara kwenye Mkoa wa Durango(Mexico). Alipewa daraja la Upadre kunako tarehe 4 Desemba 2008 kuwa wa jimbo kuu la Durango. Alipata digrii ya Sheria ya Kanoni katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Roma.
Baada ya kuingia kwenye Huduma ya Kidiplomasia ya Vatican kunako tarehe 1 Julai 2023, alitoa huduma katika Uwakilishi wa Kipapa nchini Burundi(2013-2016), Iraq (2016-2019) Hugheria (2019-2023), na kuwa sehemu ya maandalizi ya Ziara mbili za Kipapa za Papa Francisko kunako Septemba 2021 katika fursa ya Kongamano la 52 la Kimataifa na kunako 2023.
Kuanzia tarehe 1 Julai 2023 amekuwa Afisa wa Kitengo cha Mambo ya Jumla cha Sekretarieti ya Vatican, ambapo alifunika hata nafasi ya Mkuu wa Ofisi Kuu ya Takwimu za Kanisa, kusimamia Kitabu cha anuani Mwaka, cha Kipapa na uwekaji wake wa kidijitali.