Saidia hatua za Papa Leo XIV,toa mchango wa Sadaka ya Mtakatifu Petro
Vatican News
Kuwa mkono unaosaidia mkono wa Papa katika kutenda mema. Kusimama karibu yake katika kutangaza ujumbe wa Kikristo, ili kuchangia upendo wake kwa wale wanaoishi maisha yasiyofaa, na kumsaidia kukuza amani. Hii ndiyo maana ya Sadaka ya Mtakatifu Petro ambayo ni desturi ya karne nyingi ya mshikamano katika kuunga mkono Mapapa ambayo ina mizizi yake katika Maandiko Matakatifu yenyewe.
Siku ya kiutamadini ya mkusanyo huko ni tarehe 29 Juni katika, siku kuu ya Watakatifu Petro na Paulo, ambayo kwa mwaka huu itakuwa ni Dominika ya mwisho ya mwezi huu. Kwa hiyo ni njia madhubuti ya kumuunga mkono Papa Leo XIV katika utume wake kwenye huduma ya Kanisa la Ulimwengu wote.
Ili kuunga mkono mpango huo, Sekretarieti ya Uchumi ya Kiti Kitakatifu na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Vatican zimetayarisha nyenzo za kuelimisha na kupitia vyombo vya habari ili kuelezea maana yake.
Katika Tovuti rasmi yaani ya mchango huo, unaweza kuchingia, kwa kutoa sadaka yako()kupitia chaneli za kidijitali zenye uhakika.
Kama ilivyo kwa kila mwaka mchango mdogo au mkubwa utamsaidia Baba Mtakatifu katika huduma yake na katika shughuli zake za upendo katika kujibu hali halisi ya dharura na mahitaji ya Ulimwengu mzima.
Asante kwa kusoma makala hii. Ikiwa inataka kusasishwa habari zetu tunakualika ujiandikishe kwenye jarida kwa kubonyeza hapa: cliccando qui