Papa Leo XIV:tumieni karama ya ukuhani,unyenyekevu,upole,uwezo wa kusikiliza&ukaribu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Shughuli zozote mtazokabidhiwa, popote mtakapojikuta duniani, Papa lazima awe na uwezo wa kuwategemea mapadre ambao, katika sala na kama kazini, hawajizui kupeleka ukaribu wake kwa watu na Makanisa pamoja na ushuhuda wao. Kwa hakika haya na mengine ni maneno ya Baba Mtakatifu Leo XIV aliyowaelekea mapadre wanafunzi wahitimu wa Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Kikanisa ambao wamehitimisha uzoefu wa mwaka wa kimisionari, aliokuana nao Ijumaa tarehe 20 Juni 2025, katika Jumba la Kitume mjini Vatican.
Miaka mia tatu ya mafunzo ya wanadiplomasia wa kipapa
Taasisi hiyo ilianzishwa mnamo mwaka 1701 na Papa Clement XI kwa lengo la kutoa mafunzo, kwa kozi ya masomo maalum, ya kikanisa kwa vijana kwa ajili ya huduma ya kidiplomasia ya Vatican na hivyo inakaribia miaka 325. Mnamo mwezi 2020, Papa Francisko alirekebisha mchakato wa mafunzo wa Chuo cha Kikanisa kwa kuanzisha, kupitia barua yake ya Motu Proprio ili kujumuisha katika mtaala wa wanafunzi "mwaka uliowekwa kikamilifu kwa ajili ya huduma ya kimisionari"katika Makanisa ya Asia, Afrika na Amerika ya Kusini.
Mwaka huu wa kimisionari, kwa lengo la Papa Fransisko, ulipaswa kupangwa kama aina ya mafunzo, yenye lengo la kupanua ujuzi, na wanadiplomasia wa kipapa wa baadaye, wa ukweli tofauti wa kikanisa duniani. Kukamilika kwa Kozi ya mafunzo ambayo Papa Leo XIV mwenyewe alisisitiza "matumizi ya elimu kwao kama ilivyokuwa katika mkutano wa Juma moja lililopita kwa wenzenu wa Alma Mater, ni thamani ya uvumbuzi huu wa malezi ulioanzishwa na mtangulizi wangu anayeheshimiwa Papa Francisko," alisema Papa Leo XIV.
Kulinda Makanisa yote, duniani kote
Papa Leo XIV aidha alisisitiza wajibu wa wanadiplomasia wa Vatican ya "kuwa wachungaji wa dhati" kama Papa Francisko alivyoandika kwa mkono wake kuhusu huduma ya Petro (Chirograph , ya kujitolea kwa usahihi kusasisha programu ya mafunzo ya Chuo cha Kipapa cha Kikanisa kwamba ni "jicho la kutazama na uzuri wa Mrithi wa Petro juu ya Kanisa na ulimwengu.” Papa alisema kuwa “Utunzaji wa mahangaiko hayo kwa Makanisa yote, sawa na huduma niliyokabidhiwa, mnahitaji huduma ya uaminifu na isiyoweza kubadilishwa ya Sekretarieti ya Vatican na Wawakilishi wa Kipapa, ambao hivi karibuni wataanza kushirikiana nao”, alisema Papa Leo XIV.
Na hatimaye Baba Mtakatifu akiwasalimia mapadre waliosindikizwa na msimamizi wa Chuo hicho, Monsinyo Salvatore Pennacchio, aliwashukuru kwa bidii ya umisionari iliyooneshwa katika mwaka wa mazoezi ambao wameisha hivi karibuni: “Ninawashukuru tena kwa unyenyekevu na kutokuwa na ubinafsi ambao mmejitolea katika mazingira tofauti zaidi katika mwaka huu uliopita na ninawabariki kwa moyo wote mwanzoni mwa huduma yenu katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican.”