杏MAP导航

Tafuta

2025.06.04 Uwakilishi wa The National italian American Foundation"(NIAF). 2025.06.04 Uwakilishi wa The National italian American Foundation"(NIAF).  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV,(NIAF):thamini urithi wa kiroho na kiutamaduni wawaliotangulia!

Katika hotuba yake na salamu kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Kitaifa wa Kiitaliano wa Marekani(NIAF),shirika linalofanya kazi katika nyanja za elimu na Upendo ambapo Papa Leo XIV alionesha matumaini kwamba kila familia itaendelea kuhifadhi urithi tajiri wa kiroho na kitamaduni wa mababu zao.Na ni kwa imani na tumaini linalosaidia katika magumu na kufungulia siku zijazo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana tarehe 4 Juni 2025, katika ukumbi mdogo wa Paulo VI, wajumbe Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko Kitaifa wa Kiitaliano wa Marekani,The National Italian American Foundation (NIAF), wakati wa kuadhimisha miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake. Salamu zake, zilizotamkwa kwa Kiingereza, ni kumbukumbu kwa kujitolea kwa muda mrefu kwa shirika hilo, lililoko jijini Washington D.C., ili kukuza uhusiano wa kiutamaduni na upendo kati ya nchi hizo mbili.  Kwa njia hiyo awali ya yote, Baba Mtakatifu alifurahi kukutana nao na aliwaomba samahani kwa kumsubiri na kwamba mfumo wa ratiba wa Vatican humeweka mikutano minne kwa wakati mmoja. Na kwa njia hiyo, kwa bahati mbaya, imembidi wamsubiri hivyo akasema kutoa hotuba fupi rasmi, na kisha kwa furaha ya kuwasalimu wote kibinafsi, ili baadaye kwenye kwenye Katekesi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Papa na wajumbe wa NIAF
Papa na wajumbe wa NIAF   (@Vatican Media)

Kazi ya kuendelea kuelimisha

Baada ya kusema hivyo Papa Leo aliendelea na hotuba yake akiwasalimia wajumbe wakiadhimisha  miaka hamsini yake. Kama wanavyojua, makumi ya mamilioni ya Waamerika wanadai kwa fahari urithi wao wa Italia, hata kama mababu zao walifika Marekani ya vizazi vya zamani. Kazi yao ya kuendelea kuelimisha vijana kuhusu utamaduni na historia ya Kiitaliano, pamoja na kutoa ufadhili wa masomo na usaidizi mwingine wa hisani katika nchi zote mbili, unasaidia kudumisha uhusiano wenye manufaa na thabiti kati ya mataifa hayo mawili.  Alama ya wengi waliohamia Marekani kutoka Italia ilikuwa imani yao ya Kikatoliki, pamoja na mapokeo yao mengi ya uchaji Mungu na ibada ambayo waliendelea kufuata katika taifa lao jipya, Baba Mtakatifu Leo XIV alikazia.

Mkutano wa Papa na Uwakilishi wa NIAF
Mkutano wa Papa na Uwakilishi wa NIAF   (@Vatican Media)

Kupyaisha hisia zao za tumaini na imani

Papa alibainisha kuwa imani hii iliwategemeza katika nyakati ngumu, hata walipofika wakiwa na matumaini ya wakati ujao wenye mafanikio katika nchi yao mpya. Ziara yao ya Vatican inatokea wakati wa Mwaka wa Jubilei, ambayo inalenga matumaini, ambayo "hukaa kama hamu na matarajio ya mambo mema yajayo, licha ya kutojua nini wakati ujao unaweza kuleta"(Spes Non Confundit, 1). Katika zama ambazo zimekumbwa na changamoto nyingi, Papa Leo XIV aliomba wakati wao wakiwa hapo, katika mji ulio na makaburi ya mitume Petro na Paulo pamoja na watakatifu wengi walioliimarisha Kanisa katika kipindi kigumu cha historia, jambo hili lifanye upya hisia zao za tumaini na imani katika siku zijazo. “Ninaomba kwamba kila mmoja wenu na familia zenu daima mtathamini urithi wa kiroho na kiutamaduni ambao mmerithi kutoka kwa wale ambao wamewatangulia.” Na kwa hisia hizo Papa Leo XIV amewapatia kwa furaha Baraka ya Kitume, ambayo kwa hiari ametoa kwa familia zao, kwa wapendwa wao  wote. Papa aliwashukuru.

Papa na ujumbe wa NIAF
Papa na ujumbe wa NIAF   (@Vatican Media)
Papa Leo XIV na Italia na Marekani
04 Juni 2025, 16:43