杏MAP导航

Tafuta

2025.06.05 Wakuu na Maafisa wa Sekreatarieti ya Vatican wakutana na Papa Leo XIV. 2025.06.05 Wakuu na Maafisa wa Sekreatarieti ya Vatican wakutana na Papa Leo XIV.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Papa aipongeza kazi ya Sekretarieti ya Vatican!

Baba Mtakatifu Leo XIV,alikutana na Sekretarieti ya Vatican,tarehe 5 Juni 2025.Papa amezindua upya juu ya Praedicate Evangelium.Akimnukuu Papa Paulo VI alihimiza kutojiruhusu kuchafuliwa na tamaa na uadui,bali kuwa jumuiya ya imani.Papapa anatmbua kazi yao inavyohitajika sana na wakati fulani, huenda zisieleweke vyema.Kwa hivyo,alipenda kutoa ukaribu wake kwao na zaidi ya yote,shukrani zake za dhati.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV amehutubia Wakuu na Maafisa wa Sekretarieti ya Vatican Alhamisi tarehe 5 Mei 2025 kwa mara ya kwanza katika Ukumbi wa Clementina. Katika hotuba yake kwanza kabisa alimshukuru Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin kwa maneno yake ya utangulizi na kwa ushirikiano anaoendelea kumpatia akiwa katika hatua zake za mwanzo wa Upapa wake. Papa aliongeza “Nimefurahiya sana kuwa pamoja nanyi, mnaotoa huduma ya thamani kwa maisha ya Kanisa kwa kunisaidia kutekeleza utume niliokabidhiwa. Kwa hakika, kama Praedicate Evangelli inavyosema: Sekretarieti ya Vatican, kama Sekretarieti ya Kipapa inayoongozwa na Katibu wa Vatican inamsaidia kwa karibu Papa wa Roma  katika utekelezaji wa utume wake mkuu  (Ibara 44-45).” Baba Mtakatifu Leo kwa njia hiyo ameeleza anavyo farijiwa na ujuzi kwamba “siko peke yangu na kwamba ninaweza kushiriki wajibu wa huduma yangu ya ulimwengu wote pamoja nanyi.”

Papa akutana na wakuu na maafisa wa Sekretarieti ya Vatican
Papa akutana na wakuu na maafisa wa Sekretarieti ya Vatican   (@Vatican Media)

Papa alisema kuwa historia ya Taasisi hii ilianza, kama tunavyojua, hadi mwisho wa karne ya 15. Baada ya muda, imechukua sura ya ulimwengu mzima na imepanuka kwa kiasi kikubwa, na kuongezeka kwa maendeleo, kupata kazi za ziada, kutokana na mahitaji mapya katika nyanja ya kikanisa na katika mahusiano na Mataifa na mashirika ya kimataifa. Hivi sasa karibu nusu yenu ni waamini walei. Na wanawake, walei na watawa  ni zaidi ya hamsini.” Baba Mtakatifu Leo aliendelea kusema kuwa “Maendeleo haya yamemaanisha kuwa Sekretarieti ya Vatican  leo inaakisi sura ya Kanisa. Ni jumuiya kubwa inayofanya kazi pamoja na Papa: kwa pamoja tunashiriki maombi, shida, changamoto na matumaini ya Watu wa Mungu waliopo duniani kote. Tunafanya hivyo kwa kueleza kila mara vipimo viwili muhimu: umwilisho na ukatoliki. Tumefanyika mwili katika wakati na historia, kwa sababu ikiwa Mungu amechagua njia ya wanadamu na lugha za wanadamu, Kanisa pia linaitwa kufuata njia hii, ili furaha ya Injili iweze kufikia kila mtu na kupatanishwa katika tamaduni na lugha za sasa”.

Papa akutana na sekretarieti ya Vatican
Papa akutana na sekretarieti ya Vatican   (@Vatican Media)

Na, wakati huo huo, Papa Leo alisisitiza “sisi daima tunajaribu kudumisha mtazamo wa Kikatoliki, wa ulimwengu wote, ambao unaruhusu sisi kuthamini tamaduni tofauti na hisia. Kwa njia hiyo  tunaweza kuwa msukumo unaojitolea kufuma ushirika kati ya Kanisa la Roma na Makanisa mahalia, pamoja na mahusiano ya urafiki katika jumuiya ya kimataifa.”Katika miongo ya hivi karibuni, vipimo hivi viwili - kuwa mwili kwa wakati na kuwa na mtazamo wa ulimwengu wote - vimezidi kuwa msingi wa kazi ya Curia. Tumeelekezwa kwenye njia hii na mageuzi ya Kanisa la Roma yaliyofanywa na Mtakatifu Paulo VI ambaye, akiongozwa na maono ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican, aliona kwa dhati udharura wa Kanisa kuwa makini na changamoto za historia, kwa kuzingatia “wepesi wa maisha ya leo” na “hali iliyobadilika ya nyakati zetu” (Regimini Ecclesiae universae August 1967, 1965).

Papa Leo XIV wakati huo huo alisisitiza tena kuwa, hitaji la huduma inayoonesha ukatoliki wa Kanisa, na kwa kusudi hili aliamuru kwamba "wale waliopo katika Kiti cha Kitume kutawala, waitwe kutoka sehemu zote za ulimwengu.” Umwilisho, kwa hiyo, unarejea uthabiti wa ukweli na mada maalum na mahususi, zinazoshughulikiwa na viungo tofauti vya Curia; huku ulimwengu mzima, ukikumbuka fumbo la umoja wenye sura nyingi wa Kanisa, kisha unaitaka kazi ya upyaisho ambayo inaweza kusaidia utendaji wa Papa. Na kiunganishi na muhtasari ni Sekretarieti ya Vatican hasa. Kwa hakika, Papa Paulo VI - mtaalam wa Curia Romana - alitaka kuipatia Ofisi hii muundo mpya, na kuifanya iwe kama sehemu ya uhusiano na, kwa hiyo, kuisimamisha katika jukumu lake la msingi la uratibu wa Mabaraza ya Kipapa na Taasisi nyingine za Kiti cha Kitume. Jukumu hili la uratibu la Sekretarieti ya Vatican linachukuliwa tena katika Katiba ya Kitume Praedicate Evangelium ya hivi karibuni, kati ya kazi nyingi zilizokabidhiwa kwa Kitengo cha Mambo ya Jumla, chini ya uongozi wa Katibu msaidizi kwa usaidizi wa Mtathmini (taz. vifungu 45-46).

Mkutano wa Papa na Sekretarieti ya Vatican
Mkutano wa Papa na Sekretarieti ya Vatican   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV aidha alisema “kando na kitengo cha Mambo ya Jumla, Katiba hiyo hiyo inabainisha Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, kinachoongozwa na Katibu wa Vatican kwa msaada wa Makatibu Wasaidizi wawili, ambao wanahusika na mahusiano ya kidiplomasia na kisiasa ya Vatican na Mataifa na masuala mengine ya sheria za kimataifa katika hatua hii ya mabadiliko ya historia. Kitengo cha Wanadiplomasia pamoja na Katibu na Katibu Msaidizi wake, badala yake wanafanya kazi ya kuwahudumia Wawakilishi wa Kipapa na Wanachama wa Makundi ya Kidiplomasia hapa Roma na duniani kote. Papa alisema anavyotambua kwamba kazi hizi ni za kuhitajika sana na, wakati fulani, huenda zisieleweke vyema.

Kwa hivyo, alipenda kutoa ukaribu wake kwao na, zaidi ya yote, shukrani zake za dhati. “Asante kwa ujuzi mnaoufanya upatikane kwa Kanisa, kwa kazi yenu, karibu kila mara iliyofichwa na kwa roho ya kiinjili inayoitia msukumo.” Papa Leo XIV aliomba aruhusiwe, hasa kwa sababu ya shukrani zake hizo, azungumzie ushuri kwao akirejea tena kwa Mtakatifu Paulo VI: “mahali hapa pasiwe na unajisi kwa tamaa au uadui; badala yake, iwe jumuiya ya kweli ya imani na mapendo, "ya ndugu na wana wa Papa", wanaojitolea kwa ukarimu kwa ajili ya manufaa ya Kanisa (taz. Hotuba kwa Curia Romana, 21 Septemba 1963). Ninawakabidhi nyote kwa maombezi ya Bikira Maria, Mama wa Kanisa, na huku nikiwashukuru kwa sababu ninajua kwamba mnaniombea kila siku, ninawabariki kila mmoja wenu kutoka moyoni mwangu, wapendwa wenu na kazi zenu.”

Papa akutana na Sekretarieti ya Vatican
Papa akutana na Sekretarieti ya Vatican   (@Vatican Media)
Papa kwa sekretarieti
05 Juni 2025, 17:20