杏MAP导航

Tafuta

Papa Leo XIV:Mama wa Mungu atusaidie kutembea pamoja katika njia ya amani

Baba Mtakatifu wakati wa Sala ya Malkia wa mbingu ilifunga Misa ya Jubilei ya Familia alirudia wito wake wa kuomba amani na kushukuru familia ambazo ni makanisa madogo ya nyumbani na Injili inakaribishwa na kupitishwa.Alikumbuka Siku ya uupashanaji habari Ulimwenguni kwa kutoa mwaliko kwa vyombo vya habari kuhakikisha ubora wa maadili ya ujumbe pia watawa waliotangazwa kuwa wenyeheri huko Poland ambao walifia imani yao mwaka 1945.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwishoni mwa ibada ya misa takatifu ninapenda kuwaelekeza kwa salamu a joto kwa wote, washiriki wa Jubilei ya Familia, watoto, Babu na wazee! Mmekuja kutoka kila kona ya Uliwengu, kwa wawakilishi wa nchi 131. Ndivyo Baba Mtakatifu Leo XIV alivyosema mara baada ya misa Takatifu iliyodhuliwa na mamia elfu ya waamini kutoka pande zote za dunia katika fursa ya Jubilei hii iliyaoanza tangu tarehe 30 Mei na kuhitimisha katika kilele chake Dominika tarehe 1 Juni 2025.

Jubilei ya familia,watoto  na wazee
Jubilei ya familia,watoto na wazee   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa: “Ninayo furaha kuwakaribisha watoto wengi, wanaohuisha tumaini letu! Ninawasalimia familia zote ambazo ni makanisa madogo ya nyumbani, mahali ambamo Injili inapokelewa na kusambazwa. Familia, kama alivyokuwa akisema Mtakatifu Yohane Paulo II ina asili kutoka katika upendo ambamo Muumba anakumbatia Ulimwengu aliuouumba(barua ya Gratissimam sane, 2). Imani, matumaini na upendo vinakua daima katika familia zetu.”  Papa Leo XIV  aliendelea kutoa salamu akisema kuwa: “Salamu maalum kwa babu, bibi na wazee. Ninyi ni mfano hai wa imani na kuigwa kwa kizazi cha vijana. Asante kwa kufika kwenu."

Jubilei ya familia, watoto na wazee
Jubilei ya familia, watoto na wazee   (@Vatican Media)

Papa alipanua  salamu zake  kwa wote wanahija waliokuwapo, kwa namna ya pekee kutoka katika majimbo ya Mondovi, huko Piemonte.   kwa kuongeza alisema "Nchini Italia na kama ilivyo Nchi nyingine wanaadhimisha Siku Kuu ya Kupaa kwa Bwana. Ni Siku kuu nzuri ambayo inatufanya tutazama hatima ya safari yetu duniani."

Jubilei ya familia, watoto, babu,bibi na wazee
Jubilei ya familia, watoto, babu,bibi na wazee   (@Vatican Media)

Katika mtazamo huo,  Papa Leo XIV  alikumbuka siku ya Jumamosi tarehe 31 Mei,  huko Braniewo nchini Poland, walitangazwa wenyeheri, Sr Cristofora Klomfass na wenzake 14 wa Shirika la Mtakatifi Catarina, Bikira na Shahidi, waliouwa kunako 1945 na wanajeshi wa Jeshi lililokuwa eneo la sasa la Poland. Licha ya hali halisi ya chuki na ya kutisha dhidi ya imani katoliki, waliendelea kuhudumia wagonjwa na yatima. Kwa maombezi ya wenyeheri wapya mashahidi Papa aliongeza- "tumkabidhi watawa wote ambao katika dunia wanajitoa kwa ukarimu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu."

Siku ya upashanaji habari duniani

Baba Mtakatifu Leo XIV pia akiendelea alikumbusha Siku ya upashanaji Habari Ulimwenguni, iliyoadhimishwa tarehe 1 Juni, na "kuwashukuru wahudumu wa vyombo vya habari ambao kwa kuhakikisha ubora wa kiadili wa ujumbe, wanasaidia familia katika kazi zao za kuelimisha.”

Papa akumbuka siku ya upashanaji habari duniani
Papa akumbuka siku ya upashanaji habari duniani

Familia zilizo kwenye matatizo

Kwa kuhitimisha Papa Leo alisema kuwa: " Bikira Maria abariki familia na kuwasadia katika matatizo yao. Katika hili alifikiria wale ambao wanateseka kwa sababu ya vita, nchi za Mashariki ya Kati, Ukraine na sehemu mbali mbali za Uliwengu. Mama wa Mungu atusaidie kutembea pamoja  katika njia ya amani."

Jubilei ya familia watoto na wazee
Jubilei ya familia watoto na wazee   (@Vatican Media)
01 Juni 2025, 12:52