杏MAP导航

Tafuta

2025.06.16Washiriki katika Shule ya Majira ya kiangazi ya Elimu ya Snga iliyohamasishwa na Uchunguzi wa Vatican wa kinajimu. 2025.06.16Washiriki katika Shule ya Majira ya kiangazi ya Elimu ya Snga iliyohamasishwa na Uchunguzi wa Vatican wa kinajimu.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV kwa wanafunzi wa unajimu:Kila mmoja ni sehemu ya jumuiya kubwa zaidi

Baba Mtakatifu akikutana na wasomi vijana 24 wa elimu ya nyota ambao,tangu tarehe 1 Juni hadi 27,wako katika Kituo cha Uchunguzi cha Castel Gandolfo,wakifuatilia mafunzo yaliyaoandaliwa kwa mada:"Kuchunguza Ulimwengu kwa Darubini ya Anga ya James Webb:"Katika shughuli yao"wote tunafaidika na kile wanachofanya."Papa amewahimiza wawe "wakarimu katika kushirikisha kile wanachojifunza na kile wanachopitia kwa uwezo wao."

Na Angella Rwezaula – Vatican.


Hotuba ya Baba Mtakatifu Leo XIV kwa Washiriki katika Shule ya Majira ya kiangazi ya Vatican ya Unajimu alizungumza kwa kiingereza akianza na salamu na kuwakaribisha huku akionesha furaha ya kupata fursa hiyo kuwasalimu wote, wanafunzi na wasomi kutoka sehemu mbalimbali za dunia wanaoshiriki katika Shule hiyo. Matashi mema ya Papa Leo XIV ni kwamba “uzoefu huu wa kuishi na kusoma pamoja hautaboresha kielimu na kibinafsi tu, bali pia kusaidia kukuza urafiki na aina za ushirikiano ambazo zinaweza tu kuchangia maendeleo ya sayansi katika huduma ya familia yetu moja ya kibinadamu.”

Shule ya Majira ya kiangazi ya mwaka huu, Papa aliongeza kuwa a imejikita kwa ajili ya mada, ya “Kuchunguza Ulimwengu kwa Darubini ya Anga ya James Webb na akauliza kama ni kweli. Hakika, huu lazima uwe wakati wa kusisimua kuwa Mnajimu! Shukrani kwa chombo hicho cha ajabu sana, kwa mara ya kwanza tunaweza kuchungulia kwa kina angahewa ya sayari za nje ambapo uhai unaweza kuwa unasitawi na kujifunza nebula ambapo mifumo ya sayari yenyewe inafanyizwa. Kwa upande wa Webb, tunaweza hata kufuatilia nuru ya zamani ya galaksi za mbali, ambayo inazungumza juu ya mwanzo kabisa wa ulimwengu wetu.

Papa na wasomi wa kinajimu
Papa na wasomi wa kinajimu   (@Vatican Media)

Waandishi wa Maandiko Matakatifu, walioandika karne nyingi zilizopita, hawakupata faida ya upendeleo huu. Hata hivyo mawazo yao ya kishairi na ya kidini yalitafakari jinsi wakati wa uumbaji ulivyopaswa kuwa, wakati “nyota ziling’aa katika zamu zao na kushangilia, Muumba wao akawaita, wakasema, Sisi hapa, ziking’aa kwa furaha kwa ajili ya yeye aliyeziumba” (Baruku 3:34 ). Katika siku zetu wenyewe, je, picha za James Webb hazitujazi mshangao, na kiukweli furaha ya ajabu, tunapotafakari uzuri wao wa hali ya juu? Timu ya sayansi ya Darubini ya Anga imejitahidi kufanya picha hizi zipatikane kwa umma kwa ujumla, jambo ambalo sote tunaweza kushukuru.

“Ingawa hivyo, kwa njia ya pekee ninyi nyote mnaoshiriki katika Shule ya Majira ya kiangazi mmepewa ujuzi na mafunzo yanayoweza kuwawezesha kutumia chombo hiki cha ajabu ili kupanua ujuzi wetu wa ulimwengu ambao sisi ni sehemu yake ndogo lakini yenye maana. Bila shaka, hakuna hata mmoja wenu ambaye amefikia hatua hii peke yake. Kila mmoja wenu ni sehemu ya jumuiya kubwa zaidi.”

Papa na wanafunzi wa kinajimu
Papa na wanafunzi wa kinajimu   (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV alisisitiza kwamba “tufikirie watu wote katika kipindi cha miaka thelathini iliyopita ambao walifanya kazi ya kujenga Darubini ya Anga na vyombo vyake, na wale waliofanya kazi ili kuendeleza mawazo ya kisayansi ambayo iliundwa ili kuyajaribu. Pamoja na mchango wa wanasayansi wenzao, wahandisi na wanahisabati, pia ilikuwa kwa msaada wa familia yao na marafiki zao wengi ambao wameweza kufahamu na kushiriki katika biashara hii nzuri, ambayo imetuwezesha kuona ulimwengu unaotuzunguka kwa njia mpya” Kwa hiyo Papa alihimiza “wasisahau kamwe kwamba wanachofanya kinakusudiwa kutunufaisha sisi sote. Wanapaswa kuwa wakarimu katika kushiriki kile wanachojifunza na kile wanachopitia, kadiri wawezavyo na vyovyote wawezavyo.”

Hawa pia Papa alieleza kuwa “Wasisite kushiriki furaha na mshangao uliotokana na tafakari yao ya "mbegu" ambazo, kwa maneno ya Mtakatifu Agostino, Mungu amepanda katika upatanisho wa ulimwengu (taz. De Genesis ad Litteram, V, 23, 44-45). Papa aliongeza kusema “Kadiri unavyoshiriki furaha zaidi, ndivyo unavyounda furaha zaidi, na kwa njia hii, kupitia kutafuta kwao maarifa, kila mmoja wao anaweza kuchangia katika kujenga ulimwengu wenye amani na haki zaidi.” Kwa mawazo hayo katika hitimisho Papa Leo alirudia tena kutoa shukrani zake kwa ziara yao na kuwahakikishia maombi yake kwa ajili yao, familia zao na kazi zao na juu yao wote kwa hiari aliomba baraka za Mungu za hekima na ufahamu, za furaha na amani. Mungu wakubariki.

Papa Leo na wanajimu
16 Juni 2025, 15:28