Papa Leo XIV kwa Wakonvetuali na wa Utatu Mtakatifu:'Kuzungumza mambo ya Mungu'
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV Ijumaa tarehe 20 Juni 2025 alikutana na wajumbe wa Mikutano mikuu ya mashirika ya Ndugu wadogo wakonventuali na Shirika la Utatu Mtakatifu na la watumwa. Katika hotuba yake iliongozwa daima na ishara ya msalaba na Amani iwe nanyi. Papa amewaribisha wote kaka na dada na salamu kwa namna ya pekee kwa wakuu wa mashirika yote ambao walithibitishwa tena na Washauri wao wa mikutano Mikuu hiyo ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa Mashirika hayo ya Tatu na Makundi ya Walei. Aliwashukuru kwa uvumilivu wao. Ili kuweza kuwakaribisha kwa pamoja Wafransiskani na wa Utatu, Papa Leo XIV alisema alivyokumbushwa juu ya picha iliyochorwa ambayo ipo katika Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Laterano, ambayo inaonesha Mkutano unaoweza kuwa mwito tena mzuri. Kiukweli, picha hiyo inaonesha Papa Innocent III akimpokea Mtakatifu Francis na Mtakatifu Juan de Mata pamoja ili kuheshimu uhusiano wao mkubwa wa mapinduzi ya maisha ya kitawa.”
Ni muhimu kugundua kuwa Mtakatifu Francis amechorwa akiwa amepiga magoti huku akiwa na kitabu kikubwa kilichofunguliwa, karibu kutaka kusema kwa Baba Mtakatifu: “ Baba Mtakatifu ninaomba tu kuishi kanuni ya Injili Takatifu”(Test 14-15). Wakati kwa Juan de Mata, alikuwa amesimama na ameshikilia Kanuni ambayo aliandika pamoja na Baba Mtakatifu. Ikiwa Mtakatifu Francis anaonesha unyenyekevu wake kwa Kanisa, akiwasilisha mpango wake sio kama wake mwenyewe, lakini kama zawadi ya kimungu, Mtakatifu Juan de Mata anaonesha maandishi yaliyoidhinishwa, baada ya kusomwa na kufanyiwa utambuzi, kama hitimisho la kazi ya lazima kabisa ili kutambua kusudi ambalo Mungu amevuvia.” Papa Leo XIV aliongeza kusema: “Mitazamo hiyo miwili, mbali na kuwa tofauti na kila mmoja, ingeakisi kila mmoja na ingekuwa mwongozo wa huduma ambayo Kiti Kitakatifu kimetekeleza tangu wakati huo kwa kupendelea karama zote.
Mungu aliwavuvia Watakatifu hawa wawili sio tu njia ya kiroho ya huduma, lakini pia hamu ya kukabiliana na Mrithi wa Petro juu ya zawadi iliyopokelewa kutoka kwa Roho ili kuifanya ipatikane kwa Kanisa. Mtakatifu Francisko alimweleza Papa hitaji la kumfuata Yesu bila kusita, bila malengo mengine, bila utata au usanii. Mtakatifu Juan de Mata alieleza ukweli huu kwa maneno ambayo yataibua baadaye msingi ambapo Mtakatifu Francis atafanya wake. Mfano mzuri utakuwa kuishi "bila kitu chako mwenyewe", bila chochote "kilichofichwa mfukoni au moyoni", kama Papa Francisko alivyosisitiza (Shirika la Roho Mtakatifu 5 Desemba 2024.) Baba Mtakatifu Leo alieleza kuwa “Neno jingine kati ya haya linaonesha hitaji la kujitolea huku kugeuzwa kuwa utumishi, ili aliye mkuu aonekane kuwa mhudumu, yaani, anayejifanya mdogo zaidi, ili awe mtumishi wa wote. Inafurahisha kuona jinsi aya ya Mtakatifu Mathayo (rej. 20:27) umeleta msamiati wa maisha yote ya kitawa, kwa sababu wito wa mtangulizi, mkuu au mhudumu hutengeneza dhana nzima ya mamlaka kama huduma.
Papa aliwageukia wanashirika la Utatu kwa kuzungumza kihispania alisema kwamba “Ili kuweza kuweka zawadi hiyo kwa sasa, wao walitaka kujikita juu ya lengo la Shirika lao : kupeleka faraja kwa wote ambao hawezi kuishi imani yao kwa uhuru. Katika miezi hii wameweza kubadilisha shauku hiyo kwa sala, kwa kufuata maneno ya Mtakatifu Paulo “ tumeteswa, lakini hatujaachwa; tumepigwa lakini hatukuuawa (2Kor 4,9) ambayo inauhusiha kauli mbiiu ya Mkutano Mkuu wao. Baba Mtakatifu ameungana nao katika sala hiyo na kuomba hata Mungu wa utatu ambaye kwa hilo ni moja ya matunda ya mkutano wako na kwamba wasiache kukumbuka katika sala zao na katika shughuli zao za kila siku wale wote ambao wanateswa kwa sababu ya imani yao.
Sehemu hii ya tatu ambayo inatazama wanaoteswa, kulingana na mafundisho ya Mtakatifu Agostino ni sehemu ya Mungu na ni ile ambayo inaguswa wito wa kukombolewa kwa watu wake. Zaidi ya mivutano kuelekea wajumbe wa Kanisa ambao wanateseka zaidi, atavutia mtazamo wa miito, waamini na watu wenye mapenzi mema katika hali halisi hii, na atadumisha katika wao uwezekano kwenye huduma ya mipaka ambayo wanajikita nayo katika Penisula ya Arabia, Mashariki ya Kati, Afrika na katika ndani ya Bara la Hindi.
Baba Mtakatifu Leo aliendelea kusema kuwa “Kipengele kingine muhimu cha kusudi la la Ndugu Wadogo Wafransiskcan(OFMConv)imekuwa, katika Mkutano Mkuu huu wa kutekeleza utambuzi juu ya kanuni za Mikutano mkuu wa Kanda , kwa sababu ndani yake "wanazungumza mambo ya Mungu." Si maslahi yetu binafsi ambayo yanapaswa kutusukuma, bali yale ya Kristo; ni Roho wake ambaye ni lazima kwanza tusikilize, ili "kuandika yajayo katika sasa" - kama kauli mbiu ya Mkutano wao Mkuu isemavyo. Msikilize kwa sauti ya ndugu, katika utambuzi wa jumuiya, katika uangalifu wa alama za nyakati, katika miito za Majisterio.” “Wapendwa wana wa Mtakatifu Francis wa Assisi, katika miaka mia nane ya utunzi wa Cantico delle Creature - Wimbo wa Sifa kwa Viumbe” au wa Fratello Sole - Ndugu Jua,”- Papa Leo XIV aliwasihi “ wawe kwa, kila mmoja binafsi na katika kila udugu, ukumbusho hai wa ukuu wa sifa ya Mungu katika maisha ya Kikristo.”
Katika hilo Papa hakusahau juu ya Wakonventuali wanasherehekea ukumbusho wa uwepo wenu upya katika nchi za Mashariki ya Mbali. Kwa kuhitimisha Mkutano huo Baba Mtakatifu Leo XIV altoa Sifa ya Mungu aliyejuu, kama ilivyoandikwa na Mtakatifu Francis kwamba: “Wewe ni mtakatifu, Bwana, Mungu wa pekee, utendaye mambo ya ajabu. Wewe ni hodari, Wewe ni mkuu, Wewe uliye juu sana, Wewe ni mfalme mwenyezi, Wewe, Baba Mtakatifu, Mfalme wa mbingu na nchi." (Chanzo cha kifransiskani, 261). Amewashukuru na kwamba Mungu awabariki.