杏MAP导航

Tafuta

Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, kamwe mwanadamu hapaswi kuzoea vita! Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, kamwe mwanadamu hapaswi kuzoea vita!  (ANSA)

Papa Leo XIV Azungumzia Kuhusu Madhara ya Vita Duniani

Baba Mtakatifu Leo XIV anasema: Kwa hakika Kanisa limevunjika na kupondeka moyo kutokana na kilio na maumivu yanayotokea sehemu mbalimbali zilizoathirika kwa vita na hasa: Ukraine, Iran, Israeli pamoja na Ukanda wa Gaza. Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, kamwe mwanadamu hapaswi kuzoea vita na kwamba, kuna haja ya kukataa na hatimaye kushinda kishawishi cha kukimbilia silaha zenye nguvu na za hali ya juu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya Katekesi yake Jumatano tarehe 18 Juni 2025 ameonesha masikitiko yake makubwa kutokana na madhara na ukatili wa vita vinavyoendelea sehemu mbalimbali za dunia. Kwa hakika Kanisa limevunjika na kupondeka moyo kutokana na kilio na maumivu yanayotokea sehemu mbalimbali zilizoathirika kwa vita na hasa: Ukraine, Iran, Israeli pamoja na Ukanda wa Gaza. Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, kamwe mwanadamu hapaswi kuzoea vita na kwamba, kuna haja ya kukataa na hatimaye kushinda kishawishi cha kukimbilia silaha zenye nguvu na za hali ya juu.

Papa Leo XIV Watu wasizoee vita
Papa Leo XIV Watu wasizoee vita   (ANSA)

Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanasema kwamba bahati mbaya vita bado havijang’olewa katika maisha ya binadamu. Vita vya hivi karibuni vinaendelea kuleta uharibifu mkubwa: kiroho na kimwili bila kusahau maangamizi makubwa na hasa zaidi, zinapotumika silaha za kisayansi za kila aina, tabia mbaya sana ya vita inatishia kuwapelekea wapiganao kwenye unyama unaozidi wa enzi za zamani. Rej. Gaudium et Spes, 79). Baba Mtakatifu Leo XIV katika jina la utu, heshima na haki msingi za binadamu sanjari na sheria za Kimataifa amerudia tena kuwataka wale wote walio katika nafasi za uwajibikaji, onyo la mara kwa mara la Hayati Baba Mtakatifu Francisko:   Vita daima ni kushindwa!  Na ile ya Papa Pius XII: “Hakuna kinachopotea kwa amani. Kila kitu kinaweza kupotea kwa njia ya vita.”

Madhara ya Vita
18 Juni 2025, 15:01