Francisko na Leo XIV na dharura ya kusikiliza
Alessandro Gisotti
"Mtu anapozungumza na wewe, subiri mpaka amalize ili umuelewe vizuri na kisha nisikie akisema kitu. Lakini cha muhimu ni kusikiliza." Siku chache baada ya kifo chake, video fupi ya Papa Francisko iliyorekodiwa mwezi Januari uliopita iliwekwa wazi. Chini ya dakika moja, imefupishwa kwa maneno tuliyoripoti mwanzoni. Kusikiliza kama dharura ya maisha (video ililenga vijana), lakini pia kama ushuhuda bora wa Papa ambaye katika miaka 12 amesikiliza kila mtu na hasa wale walio mbali zaidi, wasio na furaha, waliotupwa katika ulimwengu huu. Kwa kifupi, wale ambao tunapendelea kutowasikiliza kwa sababu, mara nyingi, maneno yao, historia zao zinatusumbua, hutufanya tukose raha. Papa Fransisko aliweka umuhimu wa kusikiliza kanuni kuu ya mawasiliano, iwe ni ya wataalamu katika tasnia hiyo, au kama alizingatia mawasiliano baina ya watu, yale ambayo yanaendana na uhusiano na ambayo hatimaye ndiyo chumvi ya kila uhusiano wa kibinadamu. Sikiliza, kwa hiyo, kisha useme. Kusikiliza kama kitendo cha kwanza cha mawasiliano. Kusikiliza, kuona na kugusa kwa mikono yako mwenyewe kabla ya kujulisha, juu ya yote, juu ya majeraha mengi ya kina ambayo hugusa mwili wa ubinadamu wetu. Vitenzi ambavyo pia vinaakisiwa katika fursa ya Siku ya 59 ya Upashanaji Habari Duniani, ambayo imeadhimishwa tarehe 1 Juni.
Kwa hakika kwenye mada pana ya kuwasiliana, Bergoglio na Prevost (hata kabla ya kuchaguliwa kuwa katika Kiti cha Petro) wote walisisitiza kwa usadikisho mkubwa umuhimu wa kusikiliza katika mawasiliano. Haja ya kutoa muda na nafasi kwa mwingine kukutana naye kimya kimya hata kabla ya neno. Kama inavyojulikana, Papa Francisko - mtangazaji wa kile alichokiita "matibabu ya kusikiliza" na "utunzaji wa sikio" - mara kwa mara alimnukuu Poverello Mtakatifu wa Assisi ambaye aliwaomba mapadre wake "kutega sikio la moyo." Kauli inayolingana na yale ambayo Askofu wa Hippo (Mtakatifu Agostino) alikuwa tayari amethibitisha mapema karne nane kuwa: "Msiwe na moyo masikioni mwenu, bali masikio katika mioyo.” Muagostino Robert Francis Prevost alitoa kanuni hii kuwa mtindo wa maisha na kisha mbinu ya utendaji wa kichungaji. Hakuna rafiki, mshirika katika miaka ya Peru na wakati ule alipokuwa Mkuu wa Shirika duniani wa awali kwa Waagostiniani na hatimaye kama Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu ambaye hajaacha kusisitiza kwanza sifa hii kuwa: "Yeye ni mtu anayesikiliza." Akihojiwa kuhusu Papa mpya na Gazeti la Ossservatore Romano, Kardinali Luis Antonio Tagle alisisitiza kwamba Papa Leo XIV "amejaliwa uwezo wa kusikiliza kwa kina na kwa subira. Kabla ya kufanya uamuzi, anajitolea kusoma kwa makini na kutafakari. Anaelezea hisia zake na matakwa yake bila kutaka kulazimisha.
Leo, kwa bahati mbaya, tunaishi katika ulimwengu ambapo inaonekana kwamba mtu aliye na uzito, na umuhimu, ndiyo anasikilizwa tu, lakini ikiwa ana "neno la mwisho." Na hii hakika pia katika bara la kidijitali, ambapo jaribu la kufunga mazungumzo na chapisho la kupendeza huelekea kutusahaulisha kuwa katika mawasiliano haipaswi kuwa na mshindi na mshindwa, lakini utajiri wa kawaida hata (na labda juu ya yote) wakati hatufikirii kwa namna sawa. Kwa hivyo, kusikiliza kama umakini kwa ubinadamu wa wengine. Kwa upekee wake. Ni ni Papa Leo XIV alijifunza tangu ujana wake: katika familia ya wana wa Mtakatifu Agostino na hata kabla ya kuwa katika familia yake mwenyewe, huko Chicago. Akisimulia katika mahojiano kama Kardinali, alipokuwa anakaribia kuingia katika unovisi alikuwa na mazungumzo marefu na baba yake. "Hata kama ningewasikia waelimishaji wangu mara mia - aliniambia - baba yangu alipozungumza nami kwa njia ya kibinadamu sana, ya kina sana, nilijiambia: ‘Kuna mengi ya kusikiliza hapa, kuna mengi ya kufikiria kuhusu alichoniambia.’”
Kuna haja ya wanawake na wanaume wenye uwezo wa kusikiliza. Na kadiri kiwango chao cha uwajibikaji kilivyo juu, ndivyo wema huu unavyohitajika zaidi. Leo, baada ya yote, machafuko makubwa zaidi yanayotesa ulimwengu hutokea kwa usahihi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kila mmoja, "kujiweka katika nafsi ya wengine." Wakati wa janga la Uviko-19, kipindi kibaya lakini ambacho tulipaswa kujifunza mafunzo kadhaa, tulilazimika kurudi kwenye kiini cha mawasiliano ambacho ni mazungumzo na jirani zetu na hata kabla ya hapo na sisi wenyewe, na hali yetu ya ndani isiyo kamili. Kama daktari wa magonjwa ya akili Eugenio Borgna alivyobaini, wakati wa karantini kuhusu "hamu isiyo na kikomo ya kusikilizwa"kuwa ilikua. Shauku ambayo daima itaambatana nasi. Na kwamba hakuna Akili Nunde(AI) itaweza kukidhi. Hata teknolojia ya juu zaidi ya kompyuta, kiukweli, itaweza kujibu moja ya maswali yetu. Lakini hakuna kitakachoweza kufanya hivyo mbele ya ukimya wetu na hitaji letu la kwanza la kuwa karibu nasi moyo unaotusikiliza.