Papa akutana na Rais Mattarella wa Italia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ijumaa tarehe 6 Juni 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, ambapo mara baada ya Mkutano huo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na Monsinyo Miros?aw Wachowski, Katibu Msaidizi wa Vatican wa Mahuhusiano,Ushirikiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa za Vyombovya habari Vatican zimebainisha kuwa: “Wakati wa majadiliano mazuri katika Sekretarieti ya Nchi, kuridhika kulioneshwa kwa mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili. Mtazamo ulikuwa katika masuala ya kimataifa, na kipaumbele maalum kwa migogoro inayoendelea katika Ukraine na Mashariki ya Kati. Mazungumzo yaliendelea na baadhi ya masuala ya kijamii, kwa kurejeea kwa namna ya pekee mchango wa Kanisa katika maisha ya nchi.”
Walipofika mjini Vatican, muda mfupi kabla ya saa 3.00 asubuhi, kwa gari, akiingia kutokea nia ya Arco delle Campane, baada ya kuvuka Njia ya Conciliazione, ambayo ilikuwa imefungwa kwa umma tangu asubuhi.
Walioandamana na rais kwenye Jumba la Kitume walikuwa binti yake Laura na watoto wake wengine wawili, pamoja na wenzi wao wa ndoa na wajukuu watano. Na Wajumbe waliofuatana naye, miongoni mwa wengine, ni Waziri wa Mambo ya Nje na Makamu Rais wa Baraza laMawaziri Italia, Bwana Antonio Tajani, Balozi wa Italia katika Mji wa Vatican Francesco Di Nitto, na Katibu Mkuu wa Ikulu ya Rais Bwana Ugo Zampetti.
Wakati wa kusubiriwa kwenye uwanja wa Mtakatifu Damas alikuwa Mwakilishi Mkuu wa Mji wa Vatican wa nyumba ya Kipapa, Monsinyo Leonardo Sapienza, pamoja na Kikosi cha kijadi cha Walinzi wa Uswiss uliotumwa pamoja wahudumu wa Baba Mtakatifu. Mabadilishano ya salamu, kubadilishana Nyimbo za Kitaifa, kisha Rais Mattarella akafikia Loggia ya pili kwa lifti katika mkutano na Papa Leo XIV katika Maktaba ya Jumba la Kitume.