Papa Leo XIV akutana na wakuu wa Harakati ya Neokatekumenali
Vatican News
Furaha na shukrani. Hizi ndizo hisia ambazo timu ya kimataifa ya Harakati ya Neokatekumenali, ukweli wa kikanisa ulioenea katika mabara matano, ulioneshwa kwa Baba Mtakatifu Leo XIV katika Mkutano wa kwanza wa faragha uliofanyika tarehe 5 Juni 2025 katika Jumba la Kitume mjini Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alipewa nakala ya Picha ya Bikira wa Njia, ambayo iko katika Kanisa Kuu la Madrid nchini Hispania, ambapo ina maneno yaliongoza utume wa safari ya imani yaliyoandikwa: "Lazima tuunde jumuiya kama Familia Takatifu ya Nazareti, wanaoishi kwa unyenyekevu, urahisi na sifa. Mwingine ni Kristo.” Papa pia alipewa nakala nyingine ya kitabu kilichochapishwa hivi karibuni, chenye kichwa: “Cuore indiviso, missione e verginità”, yaani, " Moyo usiogawanyika, Utume na usafi,” ambacho kina nukuu zaidi ya 400 kuhusu wanawake na mwanzilishi Carmen Hernández.
Uhusiano na Mama Yetu wa Pompei
Mwanzilishi wa Harakati hiyo, Bwana Kiko Argüello kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Harakati hiyo inaarifu kwamba alisema alivyofurahi sana kwamba Papa alikuwa mmisionari, kuhusiana na chapa yenye nguvu ya kimisionari ya Harakati ya Neokatekumenali. Papa, aliyechaguliwa mnamo tarehe 8 Mei 2025 ambayo ilikuwa ni siku ya Sala kwa Mama Yetu wa Rozari wa Pompei, aliambiwa juu ya dhamana ya kina ya Harakati ya Neokatekumenali na maadhimisho haya. Bwana Kiko Argüello na Carmen Hernández walipofika Roma mwaka wa 1968, kwa hakika, walikwenda Pompei kumwomba Bikira wa Rozari kulinda na kuunga mkono utume wao. Hasa mnamo tarehe 8 Mei 1974, kwa mara ya kwanza, mwishoni mwa Katekesi ya Papa Paulo VI aliwasalimu mapadre na walei waliohudhuria wa Harakati ya Neokatekumenali, "akituambia maneno ya kinabii ambayo yalikuwa ya msaada mkubwa kwa Harakat hii," Kiko alikumbuka.
Kuanzishwa kwa Kikristo katika majimbo na parokia
Katika mkutano huo, "karibu sana", taarifa kwa vyombo vya habari inaendelea, "Timu iliweza kumsasishia Papa kuhusu shughuli nyingi ambazo Harakati inafanya katika Kanisa, kwa njia ya Ratiba ya Ukristo inayotolewa kwa Parokia na Majimbo, kusaidia familia katika kukabiliana na changamoto ya ulimwengu mamboleo, kuishi wito wao, kufungua maisha katika utimilifu, kutoa fursa kwa vijana wengi kukutana na Yesu Kristo.”
Uinjilishaji duniani
Timu ya Kimataifa ya Harakati hiyo ilipata fursa ya kumjulisha Papa Leo XIV kuhusu kazi ya uinjilishaji ambayo wasafiri wengi wanaifanya katika majimbo mengi, kuhusu “idadi kubwa ya familia ambazo, kwa kumshukuru Bwana, zimejitolea kusaidia utume wa Kanisa katika maeneo maskini na magumu zaidi duniani.” Kuhusu “kuwapo kwa Harakati hiyo katika nchi 138” na kuhusu “idadi ya seminari za Redemptoris Mater (Mama wa Mkombozi) zinazofunguliwa sasa katika majimbo zaidi ya mia moja kwenye mabara 5 yenye waseminari wengi wanaojiandaa kuwa mapadre.” Taarifa ilibanisha kuwa Papa aliwahimiza “kuendelea na utume huu adhimu kwa maisha ya Kanisa.”