杏MAP导航

Tafuta

2025.06.19 Padre Robert Francis Prevost siku yake ya kupewa daraja la Upadre, akiwa pamoja na ndugu zake wawili 2025.06.19 Padre Robert Francis Prevost siku yake ya kupewa daraja la Upadre, akiwa pamoja na ndugu zake wawili  

Miaka 43 iliyopita Padre Robert alipata daraja la upadre,hatua mbili kutoka Vatican

Papa Leo XIV anafanya kumbukizi tangu kupewa daraja la ukuhani katika kikanisa cha Mtakatifu Monica,kinachotazama Uwanja wa Ofisi Takatifu na kunako 2023 alikuwa amekabidhiwa kama Kanisa la ukardinali.

Andrea Tornielli

"Kwangu mimi, kuwalisha ninyi nyote mkate wa kawaida ni kitu ambacho siwezi kufanya. Lakini Neno hili ni sehemu yenu. Ninawalisha kutoka kwenye meza moja inayonilisha. Mimi ni mtumishi wenu." Maneno haya, ambayo yanaeleza wazo lililooneshwa na Mtakatifu Agostino katika mahubiri ya 339, yalijikita wazi katika utangulizi wa kadi ya ukumbusho wa kuwekwa wakfu wa Upadre wa Padre Robert F. Prevost, mnamo tarehe 19 Juni 1982. Picha iliyochaguliwa ilikuwa ya Karamu ya mwisho, iliyooneshwa katika Picha ya Kirusi ya karne ya 15.

Miaka arobaini na tatu iliyopita, Papa Leo XIV alikuwa kuhani, katika kikanisa cha Mtakatifu  Monica jijini Roma, umbali hata wa kutupa jiwe hadi  Vatican na kutoka Uwanja wa Ofisi Takatifu ambapo Papa anaishi kwa sasa. Kusimikwa huko kulifanywa na Askofu mkuu Jean Jadot wa Ubelgiji, wakati huo akiwa makamu Rais wa Sekretarieti ya Wasio Wakristo,  baada ya kuwa mjumbe wa kitume na msaidizi wa Asia, Afrika na hatimaye Marekani. Wakati wa kupewa daraja, Padre Robert Francis Prevost alikuwa na umri wa miaka 27 na tayari alikuwa amesoma Sheria ya Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas wa Aquinas. Alikuwa amejiunga na Shirika la Mtakatifu Agostino miaka miano kabla na alifunga  nadhiri zake mwaka 1981. Mwaka 1985 alitumwa kama mmisionari nchini Peru, akihudumu katika utume wa Chulucanas, Piura.

Kifungu kilichochaguliwa kwa ajili ya kadi ya ukumbusho kinakumbuka vifungu vingine kutoka kwa Mtakatifu Agostino, na hasa maelezo ya Zaburi (103, III, 9): “Wewe ni mtumishi mwema wa Kristo,” aliandika  Mwana wa Hippo “ikiwa unawatumikia wale ambao Kristo amewatumikia… Jua kuwapenda waja wako, lakini kwa jina la Mungu wako Mlezi. Na atujalie tuifanye huduma hii vizuri, kwa sababu, kwa kupenda au kutopenda, sisi ni watumishi; lakini tukiwa kwa mapenzi yetu wenyewe, hatutumiki kwa lazima, bali kwa upendo.” Maneno haya kuhusu kuwa watumishi, juu ya kuwa mali ya Mungu na hivyo kuwa katika huduma ya watu wake, yanaungwa mkono kwa namna fulani pia katika mahubiri ya kwanza ya kutoa Daraja la Upadre iliyoongozwa na Askofu mpya wa Roma katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, tarehe 31 Mei 2025, alipotoa daraja la upadre kwa mashemasi kumi na moja wa Jimbo la Roma.

“Wapendwa watarajiwa wa daraja,” Papa alisema, “bebeni  mimba katika njia ya Yesu! Kuwa wa Mungu—watumishi wa Mungu, watu wa Mungu, kunatuunganisha na dunia: si kwa ulimwengu bora, bali kwa ulimwengu halisi. Kama Yesu, wale ambao Baba anawaweka kwenye njia yenu ni watu wa mwili na damu. Jiwekeni wakfu kwao, bila kujitenga, bila kujitenga wenyewe, bila kufanya zawadi kupokea aina ya upendeleo… ‘Upendo wa Kristo kiukweli unatumiliki,’ kaka na dada wapendwa! Ni milki inayotukomboa na kutuwezesha kutomiliki mtu yeyote. Kukomboa, sio kumiliki. Sisi ni wa Mungu: hakuna mali kubwa zaidi ya kuthamini na kushiriki. Na utajiri pekee ambao ukishirikishwa huongezeka.” Cheo cha Kikanisa la Mtakatifu Monica, mahali pa kuwekwa wakfu mwaka 1982, kilikabidhiwa kama diakonia (ushemasi )na Papa Francisko kwa Kardinali mpya Robert Prevost kunako tarehe 30 Septemba 2023.

19 Juni 2025, 09:31