杏MAP导航

Tafuta

Papa Pio XII Papa Pio XII 

Maneno yale ya Papa Pacelli ya kusitisha vita

Mnamo 1939,Papa Pio XII alizindua wito wake maarufu kupitia radio wakati ulimwengu ulikuwa ukingoni mwa Vita vya Pili vya Dunia. Maneno ya Papa,ambayo yalikuwa hayasikiki wakati huo,yamezinduliwa tena na Papa Leo XIV, mwishoni mwa Katekesi yake ili kuomba amani katika hali ya sasa ya mvutano na vurugu.

Andrea Tornielli

Papa Leo XIV, katika ombi lake la amani mwishoni mwa Katekesi, alinukuu kwa kiasi kikubwa kifungu kutoka kwenye Ujumbe wa Radio uliotolewa Alhamisi, tarehe 24 Agosti  1939 na Papa Pio XII. Wakati huo ulimwengu ulikuwa ukingoni mwa Vita vya Pili vya Dunia kwamba: "Hakuna kinachopotea kwa amani. Kila kitu kinaweza kupotea kwa vita." Huu ndio muktadha wa maneno ya Papa Pacelli, aliyechaguliwa miezi michache mapema kama mrithi wa Pio XI baada ya kuwa Katibu wake wa Vatican kwa miaka tisa: "Ni kwa nguvu ya akili, si kwa silaha, kwamba Haki hufanya njia yake.

Na himaya zisizo na msingi wa Haki hazibarikiwi na Mungu. Siasa huru bila maadili huwasaliti wale wanaotaka iwe hivyo. Hatari iko karibu, lakini bado kuna wakati. Hakuna kinachopotea kwa ajili ya amani. Lakini kila kitu kinaweza kupotea kwa vita. Watu warudi kuelewana. Waache waanze tena mazungumzo. Kwa kujadiliana kwa nia njema na kwa kuheshimu haki za pande zote mbili, watatambua kwamba mazungumzo ya dhati na yenye ufanisi hayazuiwi kamwe na mafanikio ya heshima.

Ujumbe wa Radio ulitolewa saa 1:00 jioni,  masaa ya Ulaya kunako tarehe 24 Agosti, kutokea Castel Gandolfo, baada ya Papa kupata habari za mapatano kati ya Ujerumani ya Wanazi na Umoja wa Kisovyeti. Katika hafla hiyo, Papa Pio XII alichagua moja ya rasimu nne ambazo zilikuwa zimewasilishwa kwake na Sekretarieti ya Vatican. Nakala iliyochaguliwa ilikuwa imetayarishwa na Katibu Msaidizi Giovanni Battista Montini, (Papa wa baadaye)na Papa alikuwa amefanya masahihisho kwa mkono wake mwenyewe. Wakati Papa akiwasilisha wito huo  Montini alibaki upande wake kumsaidia. Kama inavyojulikana, wito wa Papa Pacelli kwa bahati mbaya ilipuuzwa. Mnamo tarehe 1 Septemba  1939, Askari wa Ujerumani walivuka mpaka wa Poland, na Vita vya Pili vya Ulimwengu vikaanza.

19 Juni 2025, 12:01