Kuratibu kwa Papa Leo katika Kanisa la Italia
Andrea Tornielli
Tangazo muhimu, utunzaji wa kichungaji kuhusu mada ya amani, tafakari hai juu ya mwanadamu katika enzi ya kidijitali na akili Nunde, na kukuza utamaduni wa mazungumzo. Huo ndiyo uratibu ambao Papa Leo XIV aliuonesha kwa Kanisa la Italia na yote yakiwakilisha kielelezo chenye thamani, kilichokita mizizi katika Injili na kuzama katika changamoto za wakati huu. Papa anajua kwamba Kanisa nchini Italia lazima lishughulikie mambo ya kidunia, kutopendezwa na imani na kushuka kwa kiwango cha kuzaliwa kwa watoto na alitaka kunukuu maneno ya mtangulizi wake Papa Francisko kukumbusha kwamba "ujasiri unaombwa kwetu ili kuepuka kuzoea hali ambazo zina mizizi ya kina sana ambayo inaonekana kuwa ya kawaida au isiyoweza kushindwa".
Miongoni mwa "umakini wa kichungaji" ambao wanapaswa kuwa nao Papa, Leo XVI alionesha kwamba tangazo hilo, kama inavyooneshwa na Evangelii gaudium, Waraka wa kitume kutoka miaka kumi na miwili iliyopita ambao bado unangojea kusimikwa kamili: Papa anaomba: "Kumpeleka Kristo katika mishipa ya ubinadamu," akifikiria jinsi ya kuwazuia wale walio mbali zaidi na kupyaisha lugha.
Jambo la pili, muhimu zaidi ni juu ya amani. Papa Leo anatumaini kuwa katika kila Jimbo, kozi za elimu juu ya kutotumia nguvu, mipango ya upatanisho katika migogoro ya ndani, na mipango ya kukaribisha itahamasishwa. Kwa sababu, ikiwa ni kweli kwamba vita vinaanzia moyoni mwa mwanadamu, amani lazima pia iwe na mizizi katika kiwango sawa na ni ahadi ya kila siku ya "kiufundi" ambayo inahusu kila mtu. Mtazamo wa tatu ni juu ya changamoto zinazoletwa na Akili Nunde na mazingira ya kidijitali: katika zama ambazo utu wa binadamu unahatarisha kubanwa na kusahaulika, Papa Leo anatumaini kwamba Makanisa ya Italia yatajumuisha "tafakari hai" juu ya mwanadamu, ili imani isiwe na hatari ya "kutengwa".
Umuhimu pia ni mwaliko wa mwisho wa Papa kwa maaskofu wa Italia kubaki na umoja na kufanya sinodi kuwa "mawazo", katika michakato ya kufanya maamuzi na njia za kutenda, daima kukuza utamaduni wa mazungumzo. Kinachoshangaza zaidi katika hotuba ya Leo XIV kwa Maaskofu wa Italia ni uhusiano wa karibu na wa moja kwa moja kati ya utangazaji wa Injili katika kiini chake, na matokeo yake kujitolea kwa amani na mazungumzo, kwa utu wa binadamu, iliyowekwa hatarini kwa nguvu nyingi za teknolojia mpya, kwa maskini. Hivi si uwanja wa vita kwa watu wa ndani au kazi za shirika fulani maalum. Badala yake, ni eneo ambalo Wakristo wanaulizwa leo kushuhudia uzuri wa Injili.