杏MAP导航

Tafuta

Kanisa Kuu la Notre Dame nchini Ufaransa. Kanisa Kuu la Notre Dame nchini Ufaransa. 

Papa Leo,Jubilei ya Mapadre wa Ufaransa:simikeni mizizi ya maisha yenu katika Kristo

Papa XIV alituma ujumbe kwa makuhani wa kikanisa wa Paris.Ujumbe ulisomwa katika Kanisa Kuu la Notre Dame na Askofu Blanchet,wa Créteil, aliwatia moyo kuwa na huduma inayosimikwa mizizi katika upendo mkarimu na bila kujibakiza kwa ajili ya jumuiya,iliyo na ukaribu,huruma,upoke,unyenyekevu na urahisi,kama alivyokumbusha mara nyingi na hayati Papa Francisko.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Jubilei ya Mapadre na miaka 60  ya Katiba ya (), daraja la Mapadre mahali ambapo makuhani wanajikita kutafakari, Papa Leone XIV alituma ujumbe wake tarehe 5 Juni 2025,  uliosomwa na Askofu Dominique Blanchet, wa jimbo wa Créteil kwa  mapadre wa Majimbo ya Kikanisa ya Paris. Baba Mtakatifu katika ujumbe huo aliwatia moyo wa  kujikita katika maisha na huduma katika Yesu.  Baba Mtakatifu Leo XIV alianza kwa salamu kwa  Askofu Mkuu Laurent Bernard Marie Ulrich Askofu Mkuu wa Paris, kama ilivyo kwa maaskofu wote. Aliwasalimia wapendwa makuhani waliounganika katika Kanisa Kuu la Notre-Dame(Mama Yetu) kwa kutafakari kwa kina juu ya yao wenyewe.

Upole, unyenyekevu na urahisi

Ilikuwa  furaha yake Papa kuwaonesha upendo wake wa ubaba na huku akiwatia moyo kwa ajili ya kuendelea na huduma yao kwa huduma ya Watu wa Mungu ambao walikabidhiwa. Pia Papa alibainisha , aliwashauri kuwa ili  kuondokana na ugumu ambao mara nyingi huchosha  hali za kikanisa na kijamii wanazoishi, wanapaswa kujikita  maisha yao na huduma yao katika upendo wenye nguvu zaidi, wa kibinafsi na wa kweli kwa Yesu, ambaye amewafanya wao “kuwa marafiki zake na kuwaweka kwake kwa umilele; na katika upendo wa ukarimu na usio na kikomo kwa jumuiya zao,  upendo uliojaa ukaribu, huruma, upole, unyenyekevu na urahisi, kama Baba Mtakatifu Francisko alivyokumbusha mara nyingi.”

Roho Mtakatifu awapyaishe zawadi ya ukarimu

Papa Leo XIV kwa njia hiyo, alisema kuwa “wao wataaminika hata kama wao bado si watakatifu, na watagusa mioyo ya watu walio mbali zaidi, utashinda imani yao na utawaongoza kwenye kukutana na Yesu.” Papa Leo aliwaalika kukuza udugu wa kipadre kati yao, kudumisha kifungo cha karibu cha upendo na maaskofu wao na kusali bila kukoma kwa ajili ya umoja wa Kanisa. Roho Mtakatifu akusaidie kufanya upya kila siku zawadi ya ukarimu uliyojitolea kwa Bwana siku ya kuwekwa kwako. “Nikiwaombea kila mmoja wenu ulinzi wa Mama Yetu na maombezi ya mapadre watakatifu na maaskofu wote wa Paris waliowatangulia, ninawapeni kwa moyo mkunjufu Baraka ya Kitume.”

06 Juni 2025, 10:19