杏MAP导航

Tafuta

2025.05.05 Ziara ya Papa Paolo VI katika Nchi Takatifu 1964. 2025.05.05 Ziara ya Papa Paolo VI katika Nchi Takatifu 1964.  Tahariri

Ubaba wa Petro

Katika maneno ya Papa Paulo VI katika muktadha mgumu zaidi wa huduma ya Askofu wa Roma:“ Ninahisi kuwa baba wa ubinadamu wote.”

Andrea Tornielli

Katika masaa machache ya kina ambayo yanafuatiwa na mwanzo wa Mkutano mkuu unaolikwa kumchagua Mfuasi mpya wa Mtume Petro, ni vizuri zaidi kukumbuka muktadha misingu wa huduma ya Askofu wa Roma, kwa namna ya pekee unaotambuliwa na watu wa Mungu kama ubaba. Milioni ya watu, katika wakati usiotarajiwa wa tangazo la kifo cha Francisko walihisi kuwa yatima wa baba. Katika uzoefu wa ubaba alitafakari Papa Paulo VI akizungumza na rafiki Mfalsafa Jean Guitton, baada ya kurudu kutoka safari yake nchini India kunako Desemba 1964. Papa alikuwa amemsalimia barabarani wakati wa kufika kwake akisalimiwa na watu zaidi ya milioni wanatoka katika dini zote. Mkumbatio usiosahulika. Watu wengi walikuwa wamevamia barabara, wakizunguka gari la Papa Paulo VI ambalo baadaye alitoa zawadi kwa Mama Teresa wa Kalkuta.

Safari ya Papa Paulo VI nchini India
Safari ya Papa Paulo VI nchini India

Kwa masaa mawili bila hata kusimama, Papa Montini aliwasalimia na kuwabariki. Kwa kumumbuka mkutano ule na umati, Papa alisema kwa Guitton: Ninaamini kwamba hadhi zote za Papa, zile za kutamaniwa zaidi ya ubaba. Ilijitokeza kumsindikiza Papa Pio XII katika maadhimisho makuu. Alikuwa akijitupa katika umati kama vile kisima cha Betsaida. Walimsonga na kurarua nguo zake. Na yeye alikuwa angavu. Alikuwa akipata nguvu tena. Lakini kati ya kuwa shuhuda wa ubaba na kuwa mtu baba wa kawaida kuna kitu kama bahari. Ubaba ni hisia ambayo inagusa roho na moyo, ambayo inatusindikiza kwa kila sasa ya siku, ambayo huwezi kuipunguza, lakini inakua, kwa sasabu inakuwa idadi ya watoto.” Hii siyo sana kama ubaba. Na uwezi kuacha kuwa baba… Ninahisi kuwa baba wa ubinadamu wote… Aliongeza Paulo VI “Nahisi hii katika dhamiri ya Papa daima ni mpya na hai daima, na wakati huo huo ikiwa inazaliwa, huru daima na inauhisha. Ni hisia ambayo haisumbuki, na ambayo haichoki, na ambayo inapumzia kwa kila uchovu.”

Papa Paulo VI nchini India
Papa Paulo VI nchini India

Haikutokea kamwe muda wowote ambao nilihisi kuchoka, wakati niliamsha mkono kubariki. Hapana, sitochoka kamwe kubariki au kusamehe. Wakati nilipofika Bombay, kulikuwa na safari ya kilomita 20 ili kufikia Makao ya Mkutano. Umati mkubwa,sana , kimya, bila mwendo, walitengeneza barabara - umati wa watu wa kiroho na maskini, wale wenye hamu, waliojaa, wasiovaa nguo, umati wa makini ambao mtu hunaona tu nchini India. Nilikuwa ninaendelee kuwabariki. Nafikiri kuhani ambaye alikuwa karibu nami, ninaamini kwamba karibu na mwisho alikuwa ashikirie mkono wake, kama Mtumishi wa Musa. Pamoja na hayo mimi sijisikii kuwa mkuu, bali kaka mdogo wa wote kwa sababu ninabeba uzito wa wote.” Mfuasi wa Petro ni kaka, “mdogo wa wote” kwa sababu anabeba uzito wa wote. Miezi kadhaa kabla ya uzoefu ule wa India, Papa Paulo VI alikuwa tayari amejaribu nini maana ya “kumezwa” na mikumbatio ya watu. Ilikuwa ni Mwezi Januari 1964, wakati wa ziara yake ya kwanza ya kitume katika Nchi Takatifu. Safari moja ya nguvu aliyoitaka Papa Montini.

Papa Paulo VI huko Nchi Takatifu
Papa Paulo VI huko Nchi Takatifu

Huko Yerusalemu karibu na Mlango wa Damasko, kulikuwa na umati mkubwa ambao ulikuwa mkubwa kiasi cha kuzuia hatua ya za kufikia  mpango uliokuwa umepangwa. Gari lenyewe la Papa lilikuwa likiyumba yumba kama mtumbwi na lilifanikiwa kwa ugumu na kulindwa na maaskari wa Mfalme Hussein na kuweza kupita tu katika Mlango wa Damasko bila uwezekano wa washirika wake kumfuatilia pembeni. Papa Paulo VI kupitia njia yote ya uchungu kati ya wingi wa watu hadi kufikia njia ya zamani ya Mji Mtakatifu. Wakati mwingine ilifananishwa na kuishia kumezwa na umati.  Uso wake ulibaki daima kuwa mtulivu na mwenye kutabasamu, wakati alikuwa anaamsha mikono yake kubariki. Padre Giulio Bevilacqua, rafiki binafsi wa Papa, jioni ile ataibua katika kikundi cha waandishi wa habari waliokuwa wamekusanyika nje ya Uwakilishi wa kitume wa Yerusalemu ambao miaka mingi kabla ya Yohane Battista Montini alikuwa amewambia: “Ninaota Papa anayeishi huru bila fahari ya mahakama na magereza ya itifaki. Hatimaye peke yake kati ya mashemasi wake.” Ndiyo maana alikuwa amehitimisha Bevilacqua kuwa: “Ninaamni kuwa leo hii, licha ya kukumbwa na umati, yeye alikuwa na furaha kubwa zaidi ya kushukushwa katika Kanisa kuu la  Mtakatifu Petro akiwa juu ya kiti kichoinuliwa na wabeba kiti hicho…”

Papa Paulo VI nchi Takatifu
Papa Paulo VI nchi Takatifu
Papa Paulo VI nchini Nchi Takatifu
Papa Paulo VI nchini Nchi Takatifu
Tahariri ya Tornielli kuhusu ziara ya Papa Montini Nchini India na Nchi Takatifu
05 Mei 2025, 15:04