Leo XIV ndiye Papa mpya
Mkutano huo umemchagua Kardinali Robert Francis Prevost kuwa Askofu wa 267 wa Roma. Tangazo hilo lilitolewa kwa umati na Kardinali Shemasi Dominique Mamberti.
Vatican News
Annuntio vobis gaudium magnum: habemus Papam!, “Ninawatangazia kwa furaha kubwa: tunaye Papa!.” Muda mfupi uliopita, kutokea Dirisha la kati la Basilika ya Mtakatifu Petro, Kardinali Shemasi Dominique Mamberti alitangaza matarajio ya kanuni ya kilatini, akitangazia Roma na Ulimwengu wote, jina la Mfuasi wa Kharifa wa Mtume Petro: “Eminentissimum ac Reverendissimum Dominum, Dominum ) Sanctæ Romanæ Ecclesiæ Cardinalem.
Mwadhana Kardinali Robert Francis Prevost wa Kanisa Takatifu la Roma ambaye amejiita jina la Papa Leo XIV.
08 Mei 2025, 18:45