Papa Leo XIV na uchungu kwa Gaza:gharama kubwa ni watoto na wagonjwa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Katekesi ya kwanza siku ya Jumatano tarehe 21 Mei 2025 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu Leo XIV aliwaomba waamini wote kusali Rozari kwa ajili ya amani. Amekuwa na wazo kwa Papa Francisko mwezi mmoja baada ya kifo chake ambapo alisema: "Tunamkumbuka kwa shukrani nyingi." Papa alieleza hali ya Ukanda wa Gaza inayozidi kuwa ya wasiwasi na ya kuumiza kwamba: "Ninarudia ombi langu la kutoka moyoni kuruhusu kuingia kwa misaada ya kibinadamu yenye hadhi na kukomesha uhasama, ambao gharama yake kubwa inalipwa na watoto, wazee na wagonjwa." Hili ni eneo la Gaza, ambalo kwa mwaka mmoja na nusu limegubikwa na kifo, ghasia, uharibifu, njaa, ngome ambayo kwa sasa imezingirwa na kuharibiwa na "Magari ya Gideoni", operesheni kubwa ya kijeshi ya Israeli inayoendelea.
Kupanda tumaini katika ulimwengu uliojeruhiwa na chuki
Tayari Dominika wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu mwishoni mwa Misa ya kuanza kwa Upapa wake, tarehe 18 Mei 2025 Baba Mtakatifu Leo alishutumu ukweli kwamba katika Ukanda huo watoto, familia, na wazee walionusurika wamepunguzwa na njaa. Kwa njia hiyo alirejea kunyanyapaa vurugu hizi zinazozuia kufikiwa kwa amani ya kupokonywa silaha na maneno ambayp aliyatoa hata tangu kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye Baraka. “Katika ulimwengu uliogawanyika na kujeruhiwa na chuki na vita, tunaitwa kupanda matumaini na kujenga amani!”
Mwaliko wa kusali Rozari
Papa Leo XIV alielekeza wito wake kwa walio na majukumu ya kisiasa na serikali kuchukua hatua za haraka, na kuwaomba waamini ulimwenguni kusali sana, sala kama silaha. “Katika mwezi huu wa Maria, ningependa kurudia mwaliko wa Bikira wa Fatima: Tusali rozari kila siku kwa ajili ya amani'." Pamoja na Maria, tunaomba kwamba watu wasijifungie wenyewe kwa zawadi hii ya Mungu ndani ya mioyo yao."
Kumbukumbu ya Papa Francisko
haya yalikuwa ni maneno yanayokumbusha mialiko endelevu ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye hakuwahi kuacha kusali kwa ajili ya amani. Kwa njia hiyo Papa Leo XIV amefanya kumbukumbu ya mtangulizi wake, ambaye aliaga dunia tarehe 21 Aprili 22025. Wakati wa kumtaja yalifuatana na makofi ya waamini elfu 40 waliokuwapo. Papa alisema: "Na hatuwezi kuhitimisha mkutano wetu huu bila kukumbuka kwa shukrani kubwa mpendwa Papa Francisko, aliyerejea nyumbani kwa Baba mwezi mmoja tu uliopita.”
Salamu mbali mbali kwa mahujaji
Salamu nyingine kwa mahujaji waliofika kutoka Ulimwenguni kote ambapo aliwakaribisha hata wanahija wanaozungumza kiingereza na wageni hasa wale wanaotoka England, Ireland, Hungary, Norway, Nigeria, Senegal, Tanzania, Australia, New Zealand, India, Indonesia, Malaysia, Mongolia, Philippines, Korea Kusini, Vietnam, Canada, na Marekani. Aliwasalimia kwa namna ya pekee Watawa wa Mtakatifu Yosefu wa Annecy, Wapallottine, Watawa wamisionari wa Mituke, Mabinti wa Mtakatifu Jerome Emiliani, Wanandoa wa Kikundi cha Kristo, wanahija kutoka Jimbo la Kerry, na kikundi cha Vijana cha kujitolewa cha Kituo cha Mtakatifu Cassian. Papa Leo XIV aliwatakia: "Jubilei hii ya matumaini kwao na familia neema na upyaishwaji wa kiroho, huku nikiwaombea juu furaha na amani ya Bwana Yesu."
Hudumieni Mungu kwa furaha ya kupenda jirani kwa roho ya kiinjili
Kwa upande wa lugha ya kiitaliano Baba Mtakatifu aliwakaribisha wanahija wote kutoka Italia. Kwa namna ya pekee Mapadre wa Seminari ya kipapa ya Lombardo na Kanda ya Kristo na kuwashauri wasimike maisha yao kwa Yes una juu ya mwamba wa Neno ili wawe wajasiri, watangazaji kwa watu wa wakati wetu.Salamu kwa watawa wa Mtakatifu Yesefu wa Annecy na Wamonaki wa Mateso ya Yesu Kristo, ambao wanaadhimisha wote wawili Mikutano Mikuu. Papa Leo aliwambia kuwa anawasindikiza kwa sala zake ili jitihada yao ya kitume iwe na matunda. Papa Leo XI amewakaribisha kwa upendo makundi ya kiparokia na kuwatia moyo waendelee kwa uaminifu wa Inili, ili kuwa wakristo wa dhati katika familia na katika kila mazingira yoyote. Papa Leo alieleza wazo lake hatimaye kwa vijana, wagonjwa na wenye ndoa wapya, akiwatakia kila mmoja kuhudumia Mungu daima kwa furaha na kupenda jirani kwa roho ya kiinjili. Na wote aliwabariki.