杏MAP导航

Tafuta

2025.05.21  Papa Leo XIV. 2025.05.21 Papa Leo XIV.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV ampigia simu Kardinali Karlic wa miaka 99 baada ya upasuaji

Askofu Mkuu Mstaafu wa Paraná,aliyehusishwa na Shirika la Mtakatifu Agostino,alilazwa hospitalini kwa mshtuko wa moyo na kufanyiwa upasuaji mnamo tarehe 10 Mei 2025.Aliruhusiwa Jumanne Mei 20 na siku hiyo hiyo alipokea simu kutoka kwa Papa Leo XIV ambaye alimhakikishia ukaribu wake na maombi.Kardinali huyo sasa anaendelea kupata unafuu katika nyumba ya makuhani.

Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.

Sauti tulivu na upole ambayo, alasiri ya Jumanne, tarehe 20 Mei 2025, ilinong'ona maneno ya shukrani na msaada kwa Kardinali Estanislao Esteban Karlic, Askofu Mkuu Mstaafu wa Paraná (Argentina), anayepata unafuu baada ya upasuaji tete. Papa Leo XIV alitaka binafsi kueleza ukaribu wake kwa Kardinali, akiwa na umri wa miaka 99 kati ya wazee zaidi Baraza la Makardinali (wa pili kwa mtawa Angelo Acerbi) na kumpigia simu siku hiyo hiyo aliporuhusiwa kutoka hospitalini, akimshukuru, kwa lugha ya Kihispania, kwa huduma yake kwa Kanisa na kumhakikishia maombi yake katika kipindi hiki cha kupona.

Hospitali na upasuaji

Mnamo tarehe 10 Mei 2025 iliyopita, Kardinali Karlic alilazwa hospitalini kutokana na mshtuko wa moyo na siku chache baadaye alifanyiwa upasuaji wa kupandikiza kifaa cha kusaidia moyo(pacemaker.) Baada ya matokeo chanya, aliachiliwa na kuhamishiwa kwenye nyumba ya kikuhani ya Yesu Mchungaji Mwema ili kuendeleza uponaji wake. Kwa hivyo, siku hiyo hiyo, ishara ya upendo ya Papa Leo XIV: “ wakati muhimu sana wa urais na  wa neema kubwa ambayo ilimwacha na amani kuu,” kama inavyofafanuliwa na Askofu Mkuu wa Paraná ambaye kupitia ukurasa wake rasmi wa tovuti ilieneza habari za mazungumzo.

Urafiki wa zamani

Akiwa macho na fahamu lakini bado mdhaifu baada ya kukaa hospitalini, Kardinali Karlic - alielezea Padre Eduardo Tanger, Padre wa  Kanisa Kuu la Jiji kuu kwa vyombo vya habari vya ndani kuwa  hakuweza kuzungumza wakati wa simu lakini alifurahishwa sana na mpango huu wa Papa ambaye anahusishwa na urafiki wa zamani. Tangu mwaka wa 2005, Kardinali amekuwa akihusishwa na Shirika la  Mtakatifu Agostino, ambalo hapo awali Padre Prevost alikuwa Mkuu wa Shirika. Wakati wa safari zake huko Roma, mara nyingi alikaa kwenye Nyumba Kuu ya Waagostiniani ambako alipata fursa ya kukutana na Papa wa baadaye. Kardinali aliyeundwa na Papa Benedikto XVI mnamo 2007, Karlic alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 99 mnamo tarehe 7 Februari 2025 kwenye monasteri ya Mama Yetu wa Paraná, huko Aldea María Luisa, akisindikizwa na watawa wa Benediktini nchini Argentina.

Simu ya Papa Leo XIV
23 Mei 2025, 15:56