Papa Leo XIV amekutana na James David Vance,makamu Rais wa Marekani
Vatican News.
Jumatatu asubuhi tarehe 19 Mei 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Makamu Rais wa Marekani Bwana James David Vance, mjini Vatican, ambaye mara baada ya mkutano huo alikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya mahusiano na mataifa na mashirika ya kimataifa.
Katika mazungumzo yao kwenye Sekretarieti, walipyaisha mahusiano mazuri yaliyopo kati yao na kubainisha juu ya ushirikiano kati ya Kanisa na Serikali, kama ilivyo pia baadhi ya masuala muhimu ya maisha ya kikanisa na uhuru wa kidini. Hatimaye walibadilishana mitazamo juu ya mada za sasa za kimataifa, kwa matarajio ya kusitishwa kwa migogoro, kuheshimu haki za kibinadamu na haki ya kimataifa na suluhisho la mchakato kati ya sehemu mbili zinazohusika.
Ikumbukwe Makamu Rais wa Marekani Bwana Vance alikutana kwa faragha mnamo tarehe 20 Aprili 2025 katika siku kuu ya Pasaka katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican na Papa Francisko, ambaye walikuwa amepeana salamu za Pasaka, siku moja kabla ya kifo chake. Kabla ya hapo, alikuwa na mkutano na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, ambapo dhamira ya pamoja ya kulinda haki ya uhuru wa kidini ilithibitishwa, na kubadilishana maoni pia juu ya hali ya kimataifa.