杏MAP导航

Tafuta

2025.05.10 Papa Leone XIV  huko Genazzano Katika Madhabahu ya Mama wa Shauri jema. 2025.05.10 Papa Leone XIV huko Genazzano Katika Madhabahu ya Mama wa Shauri jema. 

Papa Leo XIV amefika Genazzano katika madhabahu ya Mama wa Shauri Jema kusali!

Jumamosi tarehe 10 Mei 2025 Papa Leo XIV,alikwenda nje ya mji wa Roma kutembea kwa faragha katika madhabahu yanayohudimiwa na Wanashirika wa Agostiniani,ambapo picha ya Mama Maria wa Shauri Jema kutoka Albania imehifadhiwa.Papa aliwasalimia watu uwanjani na kusali mbele ya picha ya Bikira:"Nilitaka sana kuja hapa katika siku hizi za kwanza za Huduma mpya ambayo Kanisa limenipatia,ili kuendeleza utume kama Mrithi wa Petro.

Vatican News

"Alasiri ya leo, muda mfupi baada ya saa 10:00,jioni, masaa ya Ulaya,  Papa Leo XIV alifika kwenye Madhabahu ya Mama wa Shauri Jema  huko Genazzano kwa ziara ya faragha. Katika Madhabahu hiyo inayohudumiwa na Watawa wa Shirika la Mtakatifu Agostino, inahifadhi picha ya zamani ya Bikira Maria na pendwa sana kwa Shirika kwa ajili ya kumbukumbu ya Papa Leo XIII." Ndivyo ililipotiwa na ofisi ya vyombo vya habari Vatican. 

Picha ya Bikira Maria wa Shauri Jema huke Genazzano
Picha ya Bikira Maria wa Shauri Jema huke Genazzano

Kwa njia hiyo inakuwa kwa mara ya kwanza na mshangao, ambapo Papa Leo XIV alichagua mahali pa mfano, katika Madhabahu ya Mama Maria, inayopendwa sana na Wanashirika wa Mtakatifu Agostino ambao wamekuwepo hapo tangu mwaka 1200: yaani katika Madhabahu ya Mama wa Shauri Jema huko Genazzano nje ya jiji la Roma.

Ziara ya Papa  Leo XIV huko Gezzano
Ziara ya Papa Leo XIV huko Gezzano

Papa mpya alikwenda huko alasiri ya Jumamosi tarehe 10 Mei 2025 muda wa saa kumi jioni, kwa ziara fupi ya faragha. Madhabahu hiyo inayohudumiwa na wanashirika wa Mtakatifu Agostino inatunza Picha ya kale ya Bikira, kutoka Scutari (Albania), ambayo  ni mpendwa  sana na Shirika hilo na kwa ajili ya kumbukumbu ya Leo XIII, Papa ambaye hakuwahi kufanikiwa kutembelea madhabahu hiyo,  lakini ambaye mnamo mwaka 1903 aliipa hadhi ya kuwa Basilika ndogo.

Kuwasili kwa Papa katika madhabahu ya Genazzano
Kuwasili kwa Papa katika madhabahu ya Genazzano

Mapapa wengine waliokuwa wamekwenda katika madhabahu hiyo ya Mama wa shauri jema alikuwa ni Papa Yohane XXIII mnamo mwaka 1959 na Yohane Paulo II mnamo mwaka 1993. Hata hivyo,  Papa Leo XIV ambaye kama Kardinali, mnamo tarehe 25 Aprili 2024, alikuwa ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Madhabahu hiyo wakati wa Siku kuu ya kumbukizi ya “Kuja” kwa picha hiyo ya Mama wa Shauri Jema. Katika mahubiri yake, Kardinali Prevost wa wakati huo alionesha kujitolea ibada kwake kwa Bikira, huku akiwahimiza waamini kupata msukumo kutoka kwa Maria ili kueneza amani na maridhiano katika Ulimwengu.

Sala ya Papa mbele ya Maria wa Shauri jema
Sala ya Papa mbele ya Maria wa Shauri jema

Salamu kwa watu na sala kwa mama Maria

Papa Leo aliwasili kwa gari aina ya Volkswagen Multivan, akiwa ameketi kiti cha mbele; alipokelewa na umati wa watu waliokuwa wakishangilia wa mamia ya watu waliokusanyika uwanjani au kuegemea madirishani na kwenye balcony. Wengi walipiga kelele "Leone, Leone" na mitaa ya karibu ikajaa polepole. Baada ya kuingia kanisani, ambapo alisalimia watawa, na waamini Papa Leo XIV alipiga magoti kusali, kwanza mbele ya madhabahu na kisha mbele ya picha ya Bikira. Pamoja na wale waliokuwepo, alisali sala ya Mtakatifu Yohane Paul II kwa Mama  Maria wa wa Shauri Jema.

Salamu za Papa kwa waamni wa Genazzzano
Salamu za Papa kwa waamni wa Genazzzano

Mwishoni, baada ya kusali sala ya “Salamu Maria” na kuimba Salamu Malkia,  Papa Leo XIV alihutubia wale waliokuwa kanisani, huku akiwasalimia pia watu wa Genazzano waliokusanyika nje kuwa: “Nilitaka sana kuja hapa katika siku hizi za kwanza za Huduma mpya ambayo Kanisa limenipatia, ili kuendeleza utume huu kama Mrithi wa Petro”. Na akikumbuka ziara iliyofanywa baada ya kuchaguliwa kwake kama mkuu wa awali wa Shirika la Mtakatifu Agostino, na chaguo la "kutoa maisha yake kwa Kanisa", Papa Leo XIV alisisitiza "imani yake kwa Mama wa Shauri jema", msindikizaji wa nuru, hekima na maneno yaliyoelekezwa na Maria kwa watumishi siku ya Harusi ya Kana, iliyoripotiwa katika Injili ya Yohane kwamba: "Fanyeni chochote atakachowaambia." Kwa hiyo akiwa na jumuiya, Papa alikwenda kwenye chumba cha ndani kwa ajili ya mkutano wa faragha.

Madhabahu ya Maria wa Shauri jema
Madhabahu ya Maria wa Shauri jema
10 Mei 2025, 17:48