Papa Leo XIV:Upendo ni chanzo na nguvu inayosukuma utangazaji wa Injili!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika tafakari ya Papa Leo XIV kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta, jioni tarehe 20 Mei 2025, alipokwenda kutoa heshima kwenye Kaburi la Mtakatifu huyo Mtume wa Watu alianza kusema kuwa kifungu cha kibiblia kilichosikika ni mwanzo wa barua nzuri sana ambayo Mtakatifu Paulo aliyowaelekeza Wakristo wa Roma ambamo ujumbe unazungukia mada kubwa tatu: neema, imani na haki. Wakati tukikabidhi kwa maombezi ya Mtakatifu wa watu, mwanzoni mwa Papa mpya tutafakari pamoja ujumbe wake. Mtakatifu Paulo anasema awali ya yote kuwa alipokea kutoka kwa Mungu neema ya kuitwa (Rm 1,5). Anatambua kwamba kukutana kwake na Kristo na huduma yake vinaunganishwa na upendo ambao Mungu alitangulia kumuita na kukataa upya wakati alikuwa bado yuko mbali na Injili akitesa Kanisa.
Papa Leo XIV alisema kuwa Mtakatifu Agostino, hata Yeye aliyeongoka, anazungumza uzoefu huo sawa akisema: "Tunaweza kuchagua nini ikiwa sisi wenyewe hatujachaguliwa kwanza? Hakika, ikiwa hatujapendwa kwanza, hatuwezi hata kupenda"(Hotuba 34, 2). Mzizi wa kila wito kuna Mungu: huruma yake, wema wake, ukarimu kama ule wa mama (Is 66,12-14) ambao kwa kawaida, kwa njia mwili wake wenyewe, unamwilisha mtoto wake ambaye bado hana uwezo wa kula mwenyewe (Mt. Agostino, tafakari ya Zaburi 130, 9). Paulo lakini wakati huo huo, anazungumza hata juu ya utii wa imani (Rm 1,5) na hapa anashirikisha hata kile alichokiishi.
Bwana kwa hakika, kwa kumtokea katika njia ya Damasko(Mdo 9,1-13), hakumyima uhuru wake, lakini alimuachia uwezekano wa kuchagua, wa kutapata tunda la ugumu la mapandano ya ndani na ya nje, ambayo yeye alikubali kukabiliana nayo. Wokovu hauji kwa kwa viini macho, lakini kwa fumbo la neema na imani, wa upendo unatoka kwa Mungu na kukubali kwa imani na uhuru kwa upande wa binadamu (2Tm 1,12).
Wakati tunamshukuru Bwana kwa wito ambao alibadilisha maisha ya Sauli, tumuombe kujua hata sisi namna ya kujibu miito yake kwa namna sawa, kwa kuwa mashuhuda wa upendo, ambao ulimiminwa katika mioyo yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye alitupatia (Rm 5,5).".Tumuombe kujua kukuza na kueneza upendo wake, kwa kuwa karibu na mmoja na mwingine(Mahubiri Papa Francisko katika Siku kuu ya Mtakatifu Paulo 25 Januari 2024), katika ushindani wenyewe kiukweli ambao, kutoka katika mkutano na Kristo alijua kusukuma mbali mateso ya kizamani na kujifanya kuwa karibu kwa wote hadi kufikia kifodini. Kwa namna hiyo, hata kwetu sisi kama Yeye katika udhaifu wa mwili alijionesha nguvu ya imani katika Mungu ambaye tulipewa sisi(Rm 5,5).
Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea: “Kwa karne nyingi, Basilika hii imekabidhiwa kutunzwa na Jumuiya ya Wabenediktini. Hatuwezi kutokumbuka, basi, tunapozungumza juu ya upendo kama chanzo na nguvu inayosukuma utangazaji wa Injili, maombi ya msisitizo ya Mtakatifu Benedikto, katika Kanuni yake, kwa upendo wa kidugu katika monasteri na ukarimu kwa wote (Kanuni, sura ya LIII; LXIII)? Lakini ningependa kumalizia kwa kukumbuka maneno ambayo, zaidi ya miaka elfu moja baadaye, Benedikto mwingine, Papa Benedikto wa kumi na sita, aliwaambia vijana: “Marafiki wapendwa - alisema - Mungu anatupenda.
Huu ndio ukweli mkuu wa maisha yetu na unaotoa maana zaidi ya kila kitu kingine […]. Katika asili ya kuwepo kwetu kuna mpango wa upendo kutoka kwa Mungu”, na imani inatuongoza “kufungua mioyo yetu kwa fumbo hili la upendo na kuishi kama watu wanaojitambua kuwa wanapendwa na Mungu” (WYD Madrid, 20 Agosti 2011). Huu hapa ni mzizi rahisi na wa kipekee wa kila utume, ikiwa ni pamoja na wangu, kama mrithi wa Petro na mrithi wa bidii ya kitume ya Paulo. Bwana anipe neema ya kuitikia wito wake kwa uaminifu."