Papa akutana na Waziri Mkuu wa Australia
Vatican News.
Jumatatu 19 Mei 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican, na Waziri Mkuu wa Jumuiya ya Madola ya Australia, Mheshimiwa Anthony Albanese, ambaye baadaye alikutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Wakati wa mazungumzo ya dhati yaliyofanyika katika Sekretarieti ya Vatican, shukrani za dhati zilioneshwa kwa uhusiano mzuri wa nchi mbili kati ya Vatican na Australia, pamoja na mchango wa Kanisa Katoliki katika huduma kwa jamii, hasa katika nyanja ya elimu.
Kisha mabadilishano ya maoni yalifanyika kuhusu hali ya kijamii na kisiasa ya nchi, yakilenga hasa mada zenye maslahi kwa pande zote mbili, zikiwemo ulinzi wa mazingira, maendeleo fungamani ya binadamu na uhuru wa dini.