Padre Fusarelli:Kutoka kwa Drancis hadi Francisko watu wawili katika huduma ya binadamu
Na Padre Massimo Fusarelli,OFM.
Hatima ya jina. Mtoto wa Pietro di Bernardone aliitwa Giovanni lakini hakupaswa kubaki na jina hili. Baba yake aliamua tofauti na hivyo kwetu sisi sote kubaki na Francis wa Assisi. Hili halijawahi kuwa jina la Askofu wa Roma, wa Papa wa Kanisa Katoliki. Na bado, ilitokea. Wanaume wawili kwa miaka yenye umbali wa mia nane, wanaohusishwa na mshangao wa jina na juu ya yote kwa njia iliyofunguliwa mbele yao, isiyotarajiwa na na ya kipekee. Francis wa Assisi daima atabaki amefungwa katika uongozi asili wa jina lake, kwamba mpaji ambaye baba yake alilipenda kwa sababu lilikuwa limemfungulia njia mpya, na sio tu kwa ajili ya biashara. Jorge Mario Bergoglio, pengine katika muda mchache wa uzito wa siku zijazo, alikaribisha jina hilo sio tu kama hatima bali kama mlango wazi wa njia ambayo bado ni ya kutembea. Mtu hajipi jina la Francis wa Assisi kirahisi. Kwa sababu linadai. Nani angeweza kustahimili kulinganisha? Kiukweli, Francisko wa karne ya 21 hakutaka kuwa nakala ya karne ya 13. Alitiwa moyo, alikaribisha baadhi ya vipengele na kujaribu kuvitafsiri katika nafasi ya kipekee ambayo aliitwa kuishi: Roma na Ulimwengu, Kanisa Katoliki na wanaume na wanawake wengi wenye mapenzi mema, wa kila rangi, lugha na watu.
Njia ya kufuata
Ikiwa baada ya miaka mia nane bado si rahisi kuelezea sura kamili na halisi ya Ndugu Francis, tufikirie jinsi gani isivyowezekana kwa Papa Francisko siku chache baada ya kifo chake. Au kutafuta karibu njia ya kufanana kati ya hao wawili. Kutotulia kwa Francis kulimfungulia njia mpya na kwa wengi baada yake ambazo zimefungua siku zijazo na kuendelea kufanya hivyo. Vivyo hivyo kwa Baba Mtakatifu Francisko, ambaye ametuachia, pamoja na maisha yake na mafundisho yake, kufungua njia kwenye njia ya kufuata, sio kuiiga bali kuifasiria na kuiacha itoe mawazo mapya, hatua na chaguo. Ninaamini kwamba mshtuko wa kwanza ambao Papa Francisko aliwapatia Wafransiskani wa ulimwengu, haukuwa kufikiria karama yao kama kitu ambacho kimepangwa kurudiwa na kuhifadhi, bali kama uhalisi ulio hai na wenye nguvu unaoendelea kuchukua maisha na mwanga katika kuwasiliana na historia, na ukweli, pamoja na miito ya kila zama. Papa Francisko ameturudisha barabarani, ametusukuma tusitishe tafsiri ambayo mara zote inahatarisha kuwa ya kiakiolojia, ya kimapenzi au isiyojulikana sana. Askofu wa Roma Fransisko ametufanya tushughulike na ukweli wa Ndugu Fransis na uthabiti wa chaguzi zake. Mikutano, nyuso, mikono ya kugusa, miili ya kuinamia na hali ya kutokimbia: uthabiti huu wa umwilisho, ambao kwa Mtakatifu Francis ulikuwa kiini cha maisha yake ya imani, umerudishwa kwetu na Baba Mtakatifu Francisko.
Mti ambao tunaweza kupata kivuli
Kwa hakika tangu mwanzo ilionekana kuwa ajabu sana kwetu kwamba Mjesuit, na zaidi ya hayo ambaye alikuwa Papa, wa kuchukua jina la maskini Francis. Lakini Ndugu Francis na karama yake kwa hakika si mali ya kipekee ya Wafransiskani wa kike na kiume. Mbegu ya Injili na ya ubinadamu ambayo Ndugu Francis alipanda katika matuta ya wakati wake na mara nyingi baada yake imekua, kama Injili inavyosema, mti ambao wote wanaweza kukimbilia na kupata kivuli. Karama hii iko wazi, inapumua na kupata nguvu tena katika sehemu zake zote, tamaduni na lugha tofauti. Pia huenda zaidi ya mipaka inayoonekana ya Kanisa Katoliki. Tunaweza kufikiria ni kiasi gani kimeweza kukaribishwa na kuoneshwa pia na Jorge Mario Bergoglio. Alituonesha kwamba karama ya Fransis inaishi tu kwa kuiishi, kujiachilia kuguswa na kuhusika. Pamoja na mawazo ni muhimu kuishi, kutembea, na kuthubutu. Pengine Papa Francisko hakujua maandishi yote na mafunzo changamano ya Ufranciskani kwa moyo, lakini alikuwa angavu wa moyo ambao aliunganisha na malezi yake ya Mtakatifu Ignatius. Kitovu ni Yesu na Injili na kwa hivyo mwili wa Kristo ambaye ni mwanadamu, hasa maskini. Haya yote yaliishi katika Kanisa na kwa wanadamu leo hii, mara nyingi sana kwenye njia za kutoroka, vurugu na vita.
Kuongozwa Francis wawili
Papa Francisko alitukumbusha Wafransiskani mambo haya muhimu ya hali yetu ya kiroho yaani tasaufi. Hakuzichosha au kuzitafsiri kwa ukamilifu, kwa njia kamili kwa kila mtu. Alifungua njia, akafuata onyo, shukrani ambayo alihisi sana wakati wetu na akashika tasaufi hiyo. Kwa sababu hiyo, Mtakatifu Francis, mtu wa udugu, amani na wa kazi ya uumbaji mzuri wa Mungu, alizungumza mara moja na moyo wake na kumruhusu kuungana na mawimbi tata yaliyo mengi ya wakati huu na ambayo bado ni baraka daima. Nakiri kwamba ilikuwa ngumu kakaa nyuma yake hata sisi Wafranciskani. Alipendekeza kwetu baadhi ya vipengele vya Ndugu Francis kwa njia ya papo hapo na pengine wakati mwingine kuhisiwa na sisi kuwa mbaya. Kwa sababu hii alitugusa. Ninaamini kwamba sasa wakati mpya unafunguliwa, ambao tunaweza kukaribisha uzoefu huu tena, kusoma tena zawadi hii na sio uchovu wa kurudishwa barabarani, mara nyingi vumbi, wakati wetu na ubinadamu mkubwa unaokaa ndani yake. Shukrani kwa Francisko wote wawili na kwa wale ambao bado wanakubali kufuata kwa haraka maongozi ya kwanza, kwa ujasiri na hekima thabiti ya pili.