Kwa mara ya pili ni moshi mweusi!
Katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi,Alhamisi tarehe 8 Mei,makadinali 133 bado hawajamchagua Mrithi wa Petro,mwishoni mwa asubuhi iliyo na kura mbili.Moshi mweusi ulitoka kwenye bomba la Kikanisa cha Sistine saa 5:51 asubuhi masaa ya Ulaya,mbele ya watu wapatao 15,000 waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.Wengi wakiwa wameshikilia simu zao mikononi na huku runinga ulimwenguni zikirekodi moshi ukitoka.
Vatican news
Makardinali wapiga kura kama ilivyokuwa imepangwa katika siku Alhamisi tarehe 8 Mei 2025 walikutana katika Kikanisa cha Pauline huku wakaadhimisha Misa na masifu ya asubuhi, na katika kikanisa cha Sistine walisali msifu ya tatu, kabla ya kuendelea na kupiga kura. Chakula cha mchana kama ilivyoratibiwa katika Nyumba ya mtakatifu Marta, na watarudi tena Jumba la Kitume saa 9.45 alasiri na saa 10.30 katika kikanisa cha sistine ili kuendelea na kura nyingine mbili zaidi.
08 Mei 2025, 11:50