杏MAP导航

Tafuta

2025.05.08 Moshi mweupe 2025.05.08 Moshi mweupe  (@Vatican Media)

Moshi mweupe! Makardinali wamemchagua Papa wa 267 wa Kanisa zima baada ya kura ya nne

Kutoka kwenye bomba la Sistine,ambapo makadinali 133 wamekusanyika Mkeenye mkutano mkuu tangu Jumatano tarehe 7 Mei 2025,moshi mweupe ulitoka saa 12.07 jini huku kukiwa na shauku ya umati wa watu, karibu watu elfu 20, waliofika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro kumkaribisha Papa mpya, wakipeperusha bendera kutoka sehemu mbalimbali za dunia,kutoka Hispania hadi Argentina, kutoka Hispania hadi Argentina. Milio ya kengele inasikika katika Uwanja huo, ishara ya furaha kwa uchaguzi.

Vatican News

Tusubiri sasa kunaongezeka kwa jina la Papa mpya ambaye atafichuliwa kwa ulimwengu kutokea katikati ya Kanisa kuu la Vatican. Tangazo hilo litatolewa na Kardinali shemasi  Dominique Mamberti. Baada ya siku mbili za kupiga kura, akidi ya 2/3 muhimu kwa uchaguzi imefikiwa. Bado tunapaswa kusubiri kumjua Mrithi wa Petro.

08 Mei 2025, 18:28