Moshi kuashiria Papa mpya!
Kutoka kwenye bomba la Sistine,ambapo makadinali 133 wamekusanyika Mkwenye mkutano mkuu tangu Jumatano tarehe 7 Mei 2025,moshi mweupe ulitoka saa 12.07 jioni huku kukiwa na shauku ya umati wa watu,karibu elfu 20,waliofika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro kumkaribisha Papa mpya,wakipeperusha bendera kutoka sehemu mbalimbali za dunia,kutoka Hispania hadi Argentina,Argentina,Kenya.Milio ya kengele inasikika katika Uwanja huo,ishara ya furaha kwa uchaguzi.
08 Mei 2025, 18:35