Mexico:mamiaelfu ya vijana wasikiliza kwa mara nyingine sauti ya Francisko
Vatican News
Zaidi ya vijana 100,000 wameunganika katika Zócalo ya mji wa Mexico, uwanja mkuubwa sana wa taifa la Amerika Kusini kwa ajili ya kusheherekea tamasha la maisha (Viate fes) na hasa kwa ajili ya jitihada za kuhamasisha amani na maridhiano katika watu ulimwenguni. Katika fursa ya onesho la kisanii ndani yake ambao kwa namna ya pekee limewapa hisia kali ni lile wa kuwawekea ujumbe wa video ambao Papa Francisko aliyefariki siku kumi nanne zilizopita(21 Apeili) alikuwa amerekodi kwa ajili ya tukio hilo mouhimu katikati ya mwaka 2024.
“Ninajua kwamba mmeunganika katika Zócalo. Na mmeunganika ili kupokea na kutoa. Hamko pale kukaa kimya, bali kwa ajili ya kupaza sauti, kusongesha vitu mbele, kwa furaha, kwa ajili ya kupokea ujumbe na kuueneza ujumbe huo. Ninawashukuru kwa utashi wenu huu wa kutenda. Kwa sababu, kuna mambo mengi mabaya, katika ulimwengu na tunapaswa kuutuliza. Lakini pia kuna mambo mazuri na ni ninyi ambao mko hapo mmeunganika, kwa sababu mnatamani kitu zaidi.” Ndiyo maneno ya Papa Francisko
Tumaini kwa ajili ya Ulimwengu
Katika mwaka ambao Kanisa Katoliki linaadhimisha Jubilei ya Matumaini(2025), wale wote waliokusanyika katika tamasha hili walikuwa wamevaa leso vyeupe, ishara ya kuchangamka kwa vijana na shauku ya pamoja ya kurudisha uwezo wa kuzungumza kwa ajili ya kijenga jamii ya ududu zaidi na mshikamano. Kwa njia hiyo Papa Francisko alikuwa amesema:
"Msisahau kamwe leso nyeupe ambayo mnaona, ambayo inazungumza juu yenu: leso nyeupe ni tumaini daima lawadhambi wote, kama sisi. Na Mungu awabariki na Bikira wa Guadalupe awalinde na msisahau kusali kwa ajili yangu. Asante,” alihitimisha ujumbe wake.