杏MAP导航

Tafuta

Misa ya kuanza kwa utume wa Papa Leo XIV  tarehe 18 Mei 2025. Misa ya kuanza kwa utume wa Papa Leo XIV tarehe 18 Mei 2025.  (@Vatican Media) Tahariri

Leo, na Kanisa “chachu kidogo" ya umoja na upendo!

Maneno ya mahubiri ya Askofu wa Roma ambaye anaanza huduma yake kwa ndugu.

Andrea Tornielli

"Nimechaguliwa bila mastahili yoyote na, kwa hofu na kutetemeka, ninakuja kwenu kama ndugu ambaye anataka kuwa mtumishi wa imani yenu na furaha yenu, nikitembea nanyi kwenye njia ya upendo wa Mungu, ambaye anataka sisi sote tuungane katika familia moja." Hivi ndivyo Papa Leo XIV, Askofu mmisionari, mpwa wa wahamiaji, Askofu wa 267 wa Roma anavyojitambulisha. Maneno mepesi na mazito ya mahubiri ya misa kwa ajili ya mwanzo wa huduma yake, yanawakilisha mpango unaozungumza nasi juu ya mambo mengine na mtindo.

Kuanza kwa huduma ya Mtume Petro ya Papa Leo XIV
Kuanza kwa huduma ya Mtume Petro ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Hayo mengine, kwa sababu katika Ulimwengu wetu ulio na vita, chuki, vurugu, migawanyiko, neno la unyenyekevu la Mrithi wa Petro linatangaza Injili ya upendo, umoja, huruma, udugu, ya Mungu anayetaka tuwe familia moja. Na mengine kwa sababu anakusudia kutoa ushuhuda wa upendo, mazungumzo, kuelewana, kushinda chuki na vita vinavyoanzia moyoni mwa mwanadamu, awe  anayechukua silaha dhidi ya ndugu yake au kumsulubisha kwa kiburi cha maneno yanayoumiza kama mawe. Na ni mtindo, kwa sababu Papa Leo XIV alikumbusha kwamba huduma ya Petro inapaswa kuwa servus servorum Dei. Mtindo wake ni huduma ya upendo na ya kutoa maisha kwa ajili ya ndugu zake: "Kanisa la Roma linalosimama kwa upendo na mamlaka yake ya kweli ni upendo wa Kristo."

Kwa hivyo kamwe sio suala la "kukamata wengine kwa dhuluma, propaganda za kidini au njia za nguvu", kwani katika kila zama tunajaribiwa kufanya, kupitia dhamana, miundo, umbelembele, soko la kidini, na mikakati iliyopangwa mezani. Badala yake, “daima ni juu ya kupenda kama Yesu alivyofanya." Kwa sababu hiyo, Petro “lazima alichunge kundi bila kujitia katika majaribu ya kuwa kiongozi peke yake au chifu aliyewekwa juu ya wengine, akijifanya kuwa bwana wa watu waliokabidhiwa kwake.” Kinyume chake, anaombwa kupenda zaidi. “Anaombwa kuitumikia imani ya ndugu zake, akitembea nao.”

Papa Leo XIV ameanza huduma yake
Papa Leo XIV ameanza huduma yake   (@Vatican Media)

Katika maneno haya ya mwisho tunaweza kuona picha ya Mchungaji Mwema ambayo Papa Francisko alipendekeza mara nyingi. Ni sura ya mchungaji anayetembea mbele ya kundi ili kuliongoza; katikati ya kundi kulisindikiza, bila kujiona kuwa bora au kujitenga; na pia nyuma ya kundi, ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayepotea na kuwa na uwezo wa kukusanya wale wa mwisho, wale waliochoka zaidi katika safari.

Kuanza kwa huduma ya Papa Leo XIV
Kuanza kwa huduma ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Askofu mmisionari ambaye leo hii anakaa katika Kiti cha Petro anatualika kutangaza Injili ya upendo, “bila kujifungia katika kundi letu dogo au kujiona kuwa bora zaidi ulimwenguni.” Kanisa ni watu wa wadhambi waliosamehewa, wanaohitaji huruma daima, ambao kwa sababu hiyo hiyo wanapaswa "kupata chanjo" dhidi ya utata wowote wa ubora, kama wafuasi wa Mungu aliyechagua njia ya udhaifu na kujishusha kwa kukubali kufa msalabani ili kutuokoa. "Tumeitwa kutoa upendo wa Mungu kwa wote", alisema Papa Leo, kuwa katika unga wa ulimwengu, "chachu ndogo ya umoja, ya ushirika,  ya udugu" na hivyo kutupia mtazamo wa mbali, ili kukabiliana na maswali, mahangaiko na changamoto za leo hii.

Kuanza kwa huduma ya Papa Leo XIV
Kuanza kwa huduma ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)
18 Mei 2025, 15:00